Thursday, June 30, 2016


WAZIRI MKUU Kassim Majaliwa amesema Halmashauri zitaelekezwa kwa waraka ni vyanzo vipi vitahitaji kutumia wawakala wa ukusanyaji mapato kwani siyo kila chanzo cha mapato ya Halmashauri kitakusanywa kwa ufanisi kwa kutumia au kwa kutotumia mawakala.

Waziri Mkuu ametoa agizo hilo leo mchana (Alhamisi, Juni 30, 2016) wakati akitoa hoja ya kuhitimisha mkutano wa tatu wa Bunge la 11 la Jamhuri ya Muungano wa Tanzania kwenye ukumbi wa Bunge mjini Dodoma.

Amesema katika ukusanyaji wa mapato, baadhi ya vyanzo vitapaswa kukusanywa na Halmashauri zenyewe kwa kuzingatia miongozo iliyotolewa na Serikali. “Moja ya miongozo hiyo ni kwamba kuanzia sasa, iwe kwa kutumia mawakala au Halmashauri zenyewe ni lazima fedha zinazokusanywa ziwekwe kwenye akaunti ya Halmashauri na kutumia mifumo ya kielektroniki ili kupunguza au kumaliza kabisa masuala ya kutumia malipo kwa fedha taslimu (cash transactions),” alisema.

Amesema katika kutekeleza agizo hilo, Halmashauri itabidi zikubaliane na wakala ni kiasi gani cha asilimia ya makusanyo kitalipwa kwa wakala na malipo yafanyike baada ya kukusanya na kuingizwa kwenye akaunti ya Halmashauri.

Amesema Sheria ya Fedha ya Serikali za Mitaa Sura ya 290, inazipa uwezo Mamlaka za Serikali za Serikali za Mitaa kutoza na kukusanya kodi, ushuru na ada mbalimbali kama vyanzo vya mapato vya Mamlaka za Serikali za Mitaa.

“Sheria hiyo pia inazipa mamlaka hizo kuteua mawakala wa kukusanya mapato hayo kwa niaba ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuzingatia sheria, kanuni na taratibu. Lakini Serikali imebaini changamoto za kiufundi katika kufanya tathmini ya vyanzo vya mapato; ugumu katika kupata mawakala wenye weledi katika ukusanyaji mapato na kubuni vyanzo vipya vya mapato, na wakati mwingine watumishi wenyewe kujipa uwakala kinyume na taratibu zinazomzuia mtumishi kufanya biashara na taasisi yake,” alisema.

Amesema hatua ya Mamlaka za Serikali za Mitaa kutumia mawakala ni miongoni mwa mikakati ya kuboresha ukusanyaji mapato na pia kutoa muda mwingi zaidi kwa watumishi wa mamlaka hizo kushughulika na majukumu ya msingi ya Halmashauri na hasa utoaji wa huduma kwa wananchi na usimamizi wa miradi ya maendeleo.

“Pamoja na dhamira nzuri ya hatua hizo, tunayo mifano ya baadhi ya Halmashauri kama vile Nzega ambayo baadhi ya wahusika wameshinikiza wakitaka zabuni zote wapewe madiwani. Jambo hili halikubaliki na tena ni kinyume cha maadili ya utumishi,” alisisitiza.

Katika hatua nyingine, Waziri Mkuu ameziagiza Halmashauri zote nchini kwamba kuanzia Julai Mosi, 2016 zihakikishe zinatumia mifumo ya kielektroniki katika kukusanya mapato, katika kulipa, kuweka na kutekeleza kikamilifu mikakati madhubuti ya kuboresha makusanyo iwe yanakusanywa na Halmashauri au na wakala.

Amesema Mamlaka za Serikali za Mitaa zina wajibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya Serikali pamoja na michango ya wananchi licha ya kuwa uzoefu unaonesha kuwa mamlaka hizo zina tatizo la kukaa na fedha kwa muda mrefu kabla ya kuzielekeza kwenye matumizi yaliyokusudiwa.

“Kuchelewesha kutoa fedha zilizotengwa kwa shughuli zilizopangwa ni kuchelewesha kufikisha huduma muhimu kwa wananchi. Napenda kuhimiza uzingatiaji wa utaratibu wa kutoa taarifa kwa wananchi kuhusu mapato na matumizi ya fedha za Serikali katika ngazi zote ili kuongeza uwazi na uwajibikaji katika sekta ya umma,” aliongeza.

Mkutano huo wa tatu wa Bunge ulioanza Aprili 19, 2016 ulikuwa mahsusi kwa ajili ya kujadili na kupitisha bajeti ya kwanza ya Serikali ya Awamu ya Tano pamoja na Makadirio ya Mapato na Matumizi kwa mwaka wa fedha 2016/2017. Bunge limeahirishwa hadi Septemba 6, mwaka huu litakapokutana tena mjini Dodoma.



Meneja wa kituo cha kusimamia wasanii ‘Mkubwa na Wanae’ Said Fella ameelezea ndani ya miaka mitano kituo chake kimefanya kitu gani kwenye tasnia ya Bongo Fleva na mabadiliko yaliyoonekana.
‘Mpaka sasa hivi Mkubwa na wanae ina miaka mitano na kuna vitu vingi vilivyofanyika na watu wanaona,  nimekuwa na kituo ambacho kinakuza wasanii na watu wananipa hongera, kikubwa kwenye suala la kukusanya wasanii mpaka kuwaongeza lazima kutakuwa na changamoto cha msingi kujua wapi pa kuanzia na pa kuelekea’- Mkubwa Fella

Klabu ya wekundu wa Msimbazi Simba leo June 30 imetangaza rasmi kupitia kurasa zake za mitrandao ya kijamii kuingia mkataba na kocha raia wa Cameroon Joseph Omog, Simba wametangaza kuingia mkataba na Omog bila kuweka wazi mambo kadhaa kwa kigezo kuwa taarifa rasmi itatoka kesho July 1.
Simba wameingia mkataba na Omog ambaye amewahi kuifundisha klabu ya Azam FC na kuipatia Ubingwa wa Ligi Kuu Tanzania bara msimu wa 2013/2014 kwa mara ya kwanza, Omog kwa sasa ana umri wa miaka 44 na anatajwa kuwa kesho ndio atatambulishwa rasmi kujiunga na Simba.
mnnn
Rapper kutoka Bongoflevani, Darasa anayetamba na wimbo uitwao Kama  Utanipenda aliyomshirikisha Rich Mavoko , sasa leo June 30, 2016 alikutana na waandishi wa habari kwaajili ya kuzinduzi single yake mpya iitwayo Too Much.
Wimbo huo mpya umeandaliwa kwenye kipindi cha miezi sita iliyopita kupitia studio ya Mr. T Touch na kwenye upande wa video mikono ya director Hanscana imehusika.
Akizungumza mbele ya waandishi wa habari alisema…’Kila iitwayo leo katika kazi zangu nikiifanya bora zaidi ya jana nashukuru watanzania wamenielewa kazi zangu, sasa leo niwaletea kitu kipya cha ‘Too Much’ ambacho nimefanyia hapa bongo, nimefanikiwa kuufanya muziki wangu kuwa wa tofauti katika ladhaa zake, mtihani wangu ndiyo huu kwa shabiki’ – Darasa


ENGLAND inatafakari uwezekano wa kumteua Gareth Southgate awe Meneja wa Muda wa England kufuatia kuondoka kwa Roy Hodgson mara baada ya England kutupwa nje ya EURO 2016 kwenye Hatua ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 na Iceland huko France.
Southgate, ambae sasa ndie Bosi wa Timu ya Taifa ya England ya Vijana chini ya Miaka 21, U-21, anaweza kuteuliwa ili kuisimamia Timu hiyo ikianza kampeni yake ili kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2018 huko Russia.

Wakiongea na Wanahabari, Mtendaji Mkuu wa FA, Chama cha Soka England, Martin Glenn, akiwa pamoja na Roy Hodgson hapo Jana, alidokeza kuwa kumsaka Meneja mpya kunaweza kuchukua Miezi kadhaa.

Hivi sasa huko England Majina kadhaa yamekuwa yakitajwatajwa n ahata Meneja wa Arsenal, Arsene Wenger, ambae sasa yuko kwenye Mwaka wa mwisho wa Mkataba wake na Arsenal, anatajwa mno kufaa kuwa Meneja mpya wa England.

Alipoulizwa moja kwa moja kama Southgate anaweza kuiongoza Timu kwa ajili ya Mechi yao ya kwanza ya kufuzu Fainali za Kombe la Dunia za 2018 hapo Septemba dhidi ya Slovakia, Glenn alijibu: “Tutaona. Tunataka tumpate kabla ya hiyo michujo ya Kombe la Dunia lakini kama hatukumpata tuna mipango ya muda. Hatuzungumzii Majina lakini hilo lake lipo wazi!”

Mchakato wa kumpata Meneja mpya wa England utasimamiwa na Glenn mwenyewe pamoja na Mjumbe wa Bodi ya FA, David Gill, na Mkurugenzi wa Ufundi wa FA, Dan Ashworth.

Wednesday, June 29, 2016

Mkali wa Bongo fleva, Harmonize ambaye ni msanii wa kwanza kusainiwa kwenye lebo ya Diamond Platnumz (WCB), amekaa kwenye interview hii na Millard Ayo na amezungumzia kuhusu kujiendeleza zaidi katika masuala ya lugha, Harmonize amesema…
>>>’Kuna mwalimu pale ofisini WCB anafundisha lugha lakini kuiongea lugha kabla haujaijua vizuri si kitu kizuri kiiungwana, kuna mwalimu pale special kabisa  kwa sababu msanii yoyote wa WCB kwa sababu tunahitaji kutanua mziki wetu ufike tuwe na market ya nje pia’
>>>’hatuwezi kuwa na biashara ya nje, unawezaje kuwa na biashara nje na wakati international language hauwezi kuiongea, inakuwa ni vigumu kwa hiyo tunajaribu na management ililiona hilo mapema na likaishughulikia kuna mwalimu pale anatufundisha lugha vizuri tu‘- Harmonize


Liverpool wamekamilisha kumsaini Sadio Mane kwa Dau la Pauni Milioni 34 kutoka Southampton na kumpa Mkataba wa Miaka Mitano.
Dau hilo linaweza kupanda na kufikia Pauni Milioni 36 likizidi lile la Mchezaji alienunuliwa na Liverpool kwa ghali kupita yeyote walipotoa Pauni Milioni 35 kumnunua Andy Carroll Mwaka 2011.
Dili hii imemfanya Mane, anaetoka Senegal, kuwa ndie Mchezaji wa Bei ghali kupita yeyote katika Historia akilipiku lile la Januari 2015 ambalo Man City walilipa Pauni Milioni 28 kwa Swansea City kumnunua Wilfried Bony.

Mane, ambae alifunga Bao 21 katika Gemu 67 za Ligi Kuu England alizochezea Southampton tangu ahamia hapo kutoka Salzburg Mwaka 2014, anakuwa Mchezaji wa Tatu kusainiwa na Meneja Jurgen Klopp katika kipindi kufuatia Kipa wa Germany Loris Karius na Beki wa Cameroon Joel Matip. Mane anafuata mlolongo wa Wachezaji kadhaa wa Southampton walionunuliwa na Liverpool tangu 2014 na wengine ni Adam Lallana, Dejan Lovren, Rickie Lambert na Nathaniel Clyne.

waliotembelea blog