Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akiongea na wananchi wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya
Zanzibar ambapo alisema mbali za jitihada zilizofanywa na serikali hiyo
katika kuinua maisha ya wazanzibar ameahidi kuendelea kusimamia
rasilimali ili zitumike kwa maslahi ya wananchi wote.
2-Makamo
wa Pili wa Rais Zaznzibar Balozi Seif Ali Idd akiongea na wananchi
wakati wa sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar ambapo alisema
serikali ya mapinduzi ya Zanzibar itaendelea kuweka jitihada ili
kuendelea kujenga uchumi za Zanzibar kwa maslahi ya wananchi.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akiwasalimia wananchi walijitokeza katika sherehe za miaka 53 ya
mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akiimba wimbo wa Taifa katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya
Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akikagua gwaride katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar
zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Rais
wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein
akisalimiana na viongozi wastaafu wa Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa
Tanzania na Serikali ya Mapinduzi ya Zanzibar katika sherehe za miaka
53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani,
Zanzibar.
Vikundi
mbalimbali, Asasi za Kiraia,Vyama vya Siasa,Mikoa,Wizara na Taasisi za
Serikali wakipita mbele Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la
Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe za miaka 53 ya mapinduzi
ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Vikosi
mablimbali vya Jeshi la Polisi vikipita mbele Rais wa Zanzibar na
Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt. Ali Mohamed Shein katika sherehe
za miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa
Amani, Zanzibar.
Vijana
vya halaiki wakiwa katika umbo linaloonesha miaka 53 ya mapinduzi ya
Zanzibar katika sherehe zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
Kikosi
cha Kwata la KimyaKimya wakionesha onesho wakati wa sherehe za miaka 53
ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani,
Zanzibar.
Komando
wa Jeshi la Wananchi Tanzania akishuka katika kamba katika sherehe za
miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani,
Zanzibar.
Kikosi
cha Makomandoo wa Jeshi la Wananchi Tanzania wakionesha onesho wa namna
ya kuakibiana na vikwazo mbalimbali wawapo kazini katika sherehe za
miaka 53 ya mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani,
Zanzibar.
Askari
wa Kikosi cha Mbwa, akionesha namna mbwa anavyoweza kuruka vikwazo
mbalimbali katika kukabiliana na wahalifu katika sherehe za miaka 53 ya
mapinduzi ya Zanzibar zilizofanyika katika uwanja wa Amani, Zanzibar.
………..
ZANZIBAR
imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu huku ikiwa imepiga hatua
mbalimbali za kimaendeleo na utoaji wa huduma bora za kijamii.
Hayo
yamebainishwa na Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi
Dkt. Ali Mohamed Shein wakati akihutubia wananchi katika sherehe za
maadhimisho ya Mapinduzi leo katika uwanja wa Amani, Unguja, Zanzibar.
Dkt.
Sein amesema kuwa siku ya Mapinduzi ni muhimu sana katika historia ya
Zanzibar kwani ndiyo siku ambayo Wazanzibar walipokuwa huru katika nchi
yao na kuweza kufanya shughuli mbalimbali za kujiletea maaendeleo.
“Tukiwa
tunasherehekea miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ni vyema
tukajivunia maendeleo yaliyopatikana na yanayoendelea
kupatikana.”Alisema Dkt. Shein.
Akitaja
baadhi ya mafanikio yaliyopatikana tangu Mapinduzi Matukufu yatokee
tarehe 12 Januari 1961, Dkt. Shein amesema kuwa mafanikio makubwa
yamepatikana katika sekta za elimu kwa kuwa na ongezeko la shule kutoka
shule 752 mwaka 2015 hadi kufikia 843 mwaka 2016.
Ongezeko
hilo limeenda sambamba na ongezeko la udahili wa wananfunzi ambapo
umeongezeka kutoka wanafunzi 384,000 hadi kufikia 424,000 mwaka 2016.
Katika
sekta ya afya kumekuwa na mafanikio ya kuongezeka kwa vituo vya afya
kwa asilimia 13.4 ambapo mwaka 2015 kulikuwa na Vituo vya Afya 134 hadi
kufikia sasa jumla ya Vituo 152 vimepatikana.
Mafanikio
mengine ni pamoja na upatikanaji wa ajira 2658 zilizotokana na miradi
mbalimbali iliyozindulia katika kipindi hiki cha maadhimisho ya siku ya
Mapinduzi, kukua kwa Sekta ya Utalii kwa ongezeko la watalii kwa
asilimia 13 huku ikichangia pato la taifa kwa asilimia 27.
Huduma
za kijamii zimezidi kuboreshwa huku upatikanaji wa maji safi na salama
umeendelea kutatuliwa ambapo miradi ya maji imeekuwa ikitekelezwa
ikiwemo kuchimba visima vipya 9 na kuvifanyia ukarabati visima vya
zamani.
Kwa
upande wake Makamu wa Pili wa Rais wa Serikali ya Mapinduzi Zanzibar,
Balozi Seif Ali Idd amesema kuwa Mapinduzi haya yamekuwa chachu ya
kuleta maendeleo kwa kuwa yamewaweka Wazanzibar kuwa huru katika
kutekeleza shughuli zao za kujiletea maendeleo.
Zanzibar
imeadhimisha miaka 53 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar huku ikiwa
imepiga hatua kubwa za kimaendeleo ambapo katika shamra shamra za
maadhimisho haya jumla ya miradi 32 ya maendeleo imezinduliwa huku
mingine 16 ikiwekwa jiwe la msingi tayari kwa utekelezaji wake, hayo
yote ni matunda yatokanayo na Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar ambayo
baadaye yalizaa Muungano wa Tanganyika na Zanzibar.
0 maoni:
Post a Comment