
8:12 AM

Unknown
MENEJA
wa Liverpool Jurgen Klopp yupo hatua za mwisho kukamilisha usajili wake
wa kwanza wa Mchezaji mpya na huyo ni Marko Grujic.
Grujic, mwenye
Miaka 19, Leo ametua Anfield kwa upimwaji wake wa afya ili kukamilisha
Dili ya Pauni Milioni 5.1 kutoka Red Star Belgrade.
Inatarajiwa
baada ya kukamilika kwa Uhamisho wake kwenda Liverpool, Kinda huyo
atarudi kuichezea kwa Mkopo Red Star hadi mwishoni mwa Msimu na kujiunga
na Liverpool kwa ajili ya Msimu ujao.
Liverpool imelazimika kufanya
uamuzi wa kumnunua Grujic hivi sasa kwa sababu alikuwa akiwindwa pia na
Klabu za Russia, CSKA Moscow na Zenit St Petersburg, ambazo zilitoa Dau
kubwa, ikiaminika kuwa ni zaidi ya Pauni Milioni 7.
Lakini
Kijana huyo aliamua mwenyewe kujiunga na Liverpool baada ya Msaidizi wa
Klopp, Zeljko Buvac, ambae anatoka Serbia, kuingiliwa kati na kuleta
ushawishi mkubwa kumchota Kijana huyo anaechezea Timu ya Taifa ya Serbia
ya U-21.
0 maoni:
Post a Comment