Tuesday, January 5, 2016



Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza katibu mkuu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani Jerome Valcke asimamishwe kujihusisha na mchezo wa soka kwa miaka tisa.
Katibu huyo anadaiwa kutumia vibaya pesa ikiwemo uuzaji wa tiketi za kombe la duniani lililopita pamoja na kukiuka sheria za Shirikisho hilo.
Awali kamati ya nidhamu alimsimamisha katibu huyo kwa siku 90 kutojihusisha na mchezo wa soka ambapo adhabu yake imemalizika leo lakini ameongezewa adhabu kwa siku nyingine 45 wakati uchunguzi ukiendelea.
Jerome ataungana na viongozi wengine Sepp Blatter aliyekuwa Rais wa FIFA pamoja na makamu wake Michel Platini ambao wote wamesimamishwa tangu mwezi uliopita kwa miaka nane baada ya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kukamilika.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog