Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii
imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari,
Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika
hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam. Akiongea wakati wa
kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF
kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa
chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza
vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.
0 maoni:
Post a Comment