Sunday, November 29, 2015


Schweinsteiger aliisawazishia bao Man United katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko sare ya 1-1.
Kipindi cha kwanza dakika ya 24 Vardy anaipa bao la kuongoza Timu yake Leicester City na kuongoza bao 1-0 dhidi ya Man United.VIKOSI:
Leicester City wanaoanza XI:
Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy
Akiba: De Laet, King, Schlupp, Ulloa, Dyer, Schwarzer, Inler
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, McNair, Carrick, Schweinsteiger, Young, Mata, Martial, Rooney
Man Utd akiba: Depay, Romero, Fellaini, Schneiderlin, Rashford, Jackson, Andreas Pereira

Manchester United wametoka Sare 1-1 huko King Power Stadium walipotoka 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Man City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England.
Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje Rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu England.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger na walistahili kushinda kwenye Kipindi cha Pili kwa jinsi walivyotawala lakini tatizo lao sugu la kutokuwa na Wachezaji wenye kasi na Wafungaji liliwakisha.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog