Saturday, January 9, 2016


Kuna mengi huwa yanaandikwa mitandaoni na kwenye magazeti kuhusu soka mtu wangu wa nguvu, Jumamosi ya January 9 naomba nikusogezee TOP 5 ya headlines stories zilizoandikwa sana mitandaoni Jumamosi ya January 9.
Klabu ya Real Madrid ya Hispania imeingia katika mbio za kuwania saini ya beki wa klabu ya Everton ya Uingereza John Stones, beki huyo alikuwa anawaniwa na klabu ya Chelsea ya Uingereza na dirisha la usajili wa wakati wa majira ya joto Chelsea walijaribu kutuma ofa tatu kwa Everton lakini zilikataliwa.
John-Stones-592491
John Stones
Manchester United inatajwa kuwa katika mipango ya kumshawishi kocha wa klabu ya Paris Saint Germain ya Ufaransa Laurent Blanc ajiunge na klabu yao, kwani bado hawana imani sana na kocha wa sasa wa Man United Louis van Gaal ambaye mkataba wake unamalizika 2017. Blanc aliwahi kuichezea Man United katika kipindi cha mwaka 2001 hadi 2003.
Paris Saint-Germain coach Laurent Blanc gives a press conference at the Parc des Princes stadium in Paris on November 26, 2013, on the eve of the UEFA Champions League football match against Olympiakos. After failing to get the job done in their last group game, Paris Saint-Germain will seek the draw required to qualify for the Champions League last 16 when they host a Kostas Mitroglou-inspired Olympiakos. AFP PHOTO / FRANCK FIFE (Photo credit should read FRANCK FIFE/AFP/Getty Images)
Laurent Blanc
Kocha mpya wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Zinedine Zidane ameweka wazi kuwa hawana mpango wa kumuuza staa wa kimataifa wa Ureno Cristiano Ronaldo kwenda katika klabu yoyote, hivyo hiyo ni taarifa ya kuvikatisha tamaa vilabu vya Man United na PSG vinavyohusishwa kumuhitaji nyota huyo “Ronaldo ni zaidi ya kusema hauzwi, roho yake ipo Real Madrid, ikiwa mimi nipo hapa na uhakika kuwa hawezi kwenda popote”
FILE - In this Sept. 16, 2014 file photo, Real Madrid's Cristiano Ronaldo reacts after missing a chance during a Champions League Group B soccer match against Basel at the Santiago Bernabeu stadium in Madrid, Spain. Christopher Renzi, of Rhode Island, had until November 2014, to notify the Portuguese soccer star of a lawsuit in a dispute over an underwear line, but Ronaldo's team refused to accept the legal papers. A U.S. judge has extended the deadline till March 2015. (AP Photo/Daniel Ochoa de Olza, File)
Ronaldo
Klabu ya Arsenal kupitia kwa kocha wake Arsene Wenger imetajwa kuthibitisha kuwa ipo karibu kukamilisha usajili wa kiungoa wa Basle Mohamed Elneny siku kadhaa zijazo “Bado mpango wake ni mgumu kukamilika, lakini tunaweza kukamilisha naweza kusema ndani ya siku mbili au tatu”
Mohamed-Elneny
Mohamed Elneny
Mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015 Pierre Emerick Aubameyang amemaliza uvumi wa yeye kuwa katika mpango wa kujiunga na Arsenal na kusema kuwa hana mpango wa kuondoka Borussia Dortmund kwa hivi karibuni.
Pierre-Emerick-Aubameyang-award1
Aubameyang



Mshambuliaji wa kimataifa Gabon ambaye anaichezea klabu ya Borussia Dortmund ya Ujerumani Pierre-Emerick Aubameyang ameingia kwenye headlines mara mbili tofauti. Headlines kubwa ya staa huyo ni juu ya ushindi wake wa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa mwaka 2015, lakini ya pili ni kuhusu Yaya Toure anavyoamini kuwa Pierre hakustahili tuzo hiyo.
Toure ambaye ni mshindi mara nne mfululizo wa tuzo ya mchezaji bora Afrika, alikuwa na matumaini ya kutwaa tuzo hiyo kwa mara ya tano ila anashangazwa na shirikisho la soka barani Afrika kudharau mafanikio yake ya kutwaa taji la mataifa ya Afrika na kumpa tuzo Aubameyang, kwani anaamini Kombe hilo halithaminiki.
237606
Pierre -Emerick Aubameyang akikabidhiwa tuzo na rais wa CAF
“Nimesikitishwa sana sana na jambo hili ni aibu kuona Afrika tunavyoichukulia, hatutoi kipaumbele kwa mashindano yetu ya ndani. Nafikiri tumeitia aibu Afrika. Tumeifanya Afrika isionekane muhimu mbele ya macho yetu, tunathamini mafanikio ya nje ya Afrika kuliko ndani ya bara letu”>>> Yaya Toure
Kiungo huyo mwenye umri wa miaka 32 ameongea hayo baada ya kufanya mahojiano na kituo cha radio cha RFI, nakueleza kushangazwa na ushindi wa Aubameyang katika tuzo hiyo na yeye kupotezewa, licha ya kuwa ametwaa taji la mataifa ya Afrika kama nahodha wa Ivory Coast.

Friday, January 8, 2016


Mwanasoka raia wa Tanzania   anayechezea TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo Mbwana Ally Samatta amenyakua tuzo ya mwanasoka bora wa Afrika anachezea ndani ya bara la Afrika.
Tuzo ya mwanasoka bora barani Afrika imemwendea Pierre-Emerick raia wa Gabon anayesakata kambumbu katika klabu ya Borussia Dotmund nchini Ujerumani.
Tuzo hizo za kila mwaka zinazotolewa na Shirikisho la soka barani Afrika almaarufu kama CAF zimetolewa usiku wa kuamkia Ijumaa mjini Abuja nchini Nigeria.
Timu bora kwa wanaume kwa mwaka uliopita ni kutoka Ivory Coast.
Kwa upande wa timu ya wanawake ya mwaka tuzo imekwenda kwa timu ya Cameroon


Kocha bora wa mwaka ni – Herve Renard, kutoka Ivory Coast, tuzo ambayo ameishinda kwa mwaka wa pili mfululizo.
Klabu bora ya soka barani Afrika ni TP Mazembe, kutoka DR Congo
Mwanasoka bora wa kike Afrika ni Gaelle Enganamouit kutoka Cameroon
Mwamuzi bora wa mwaka ni Bakary Gassama kutoka nchini Gambia
Tuzo hizo zilipambwa na shamra shamra za kila aina kutoka kwa wasanii maarufu pamoja na wanenguaji walitumbuiza akiwemo mwanamuziki nguli kutoka nchini Mali, Salif Keita pamoja na mwanamuziki kutoka Nigeria Omowumi.

FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini na ni Kombe kongwe kabisa Duniani, litaanza kurindima Ijumaa Usiku huko England kwa Mechi pekee huko Mjini Exeter kati ya Exeter City FC na Liverpool.
Huu ni mwanzo wa Mechi za Raundi ya 3 FA CUP, inayoshirikisha jumla ya Timu 64, ambayo Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la chini yake, The Championship, huanzia kampeni zao na nyingine hufuzu toka Raundi zake za awali kabisa.
Exeter City, Timu ya Ligi 2, ambayo ni Daraja la 4 kwa Mfumo wa England, wamefanikiwa kutinga Raundi ya 3 na sasa ni Wenyeji wa Klabu kigogo Liverpool.

Raundi hii ya 3 imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe na moja ya hizo ni ile Mechi tamu huko White Hart Lane ambako Tottenham watawavaa ‘Maajabu’ ya Ligi Kuu England Leicester City ambao wako Nafasi ya Pili katika Msimamo wa Ligi hiyo. Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, Jumamosi watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumapili wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
Siku ya Jumamosi Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.

FA CUP
Raundi ya 3
Ijumaa Januari 8

22:55 Exeter v Liverpool

Jumamosi Januari 9
15:45 Wycombe v Aston Villa
[Mechi kuanza Saa 12:00 Jioni]
Arsenal v Sunderland
Birmingham v Bournemouth
Brentford v Walsall
Bury v Bradford
Colchester v Charlton

Doncaster v Stoke
Eastleigh v Bolton
Everton v Dag & Red
Hartlepool v Derby
Huddersfield v Reading
Hull v Brighton
Ipswich v Portsmouth
Leeds v Rotherham
Middlesbrough v Burnley
Newport v Blackburn
Northampton v MK Dons
Norwich v Man City
Nottm Forest v QPR
Peterborough v Preston
Sheff Wednesday v Fulham
Southampton v Crystal Palace
Watford v Newcastle
West Brom v Bristol City
West Ham v Wolves
20:30 Man United v Sheffield United

Jumapili Januari 10
15:00 Oxford United v Swansea
17:00 Carlisle v Yeovil
17:00 Chelsea v Scunthorpe
19:00 Tottenham v Leicester
21:00 Cardiff v Shrewsbury



THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4

Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016

Raundi ya 6-Robo Fainali

Jumamosi 12 Machi 2016

Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016


www.bukobasports.comBelgium imebaki Nambari Wani kwenye FIFA Listi ya Ubora Duniani iliyotolewa Leo huku Tanzania ikipanda Nafasi 6.
20 Bora imebaki vilevile bila mabadiliko huko Mabingwa wa Dunia, Germany, wakiwa Nafasi ya 4.
Tanzania sasa ipo Nafasi ya 126 baada ya kupanda Nafasi 6 toka Mwezi uliopita.
Kwa Afrika, Timu ya juu kabisa kwenye Listi ya Ubora ni Ivory Coast ambayo ipo Nafasi ya 19.

"TOP 20" BORA:
1. Belgium
2. Argentina
3. Spain
4. Germany
5. Chile
6. Brazil
7. Portugal
8. Colombia
9. England
10. Austria
11. Uruguay
12. Switzerland
13. Ecuador
15. Italy
16. Romania
17. Wales
18. Croatia
19. Côte d'Ivoire
20. Hungary

Thursday, January 7, 2016



Bado saa zinasogea na kila mpenda soka macho na akili yake kaelekeza Abuja Nigeria kusubiri nini kitatokea, Mbwana Samatta atafanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa Afrika anayecheza Ligi ya ndani? lakinia vipi kwa upande wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa jumla nani atatwaa Pierre Emerick, Yaya Toure? Andrew Ayew? Naomba nikusogezee vitu 7 ambavyo huenda hufahamu kuhusu tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla ambapo wachezaji wanaowania hii ni Yaya Toure, Andrew Ayew na Pierre-Emerick Aubameyang .
1- Emanuel Amuneke ambaye ni winga wa zamani wa Nigeria ndio mchezaji pekee aliyekuwa anacheza ndani ya Afrika aliwahi kutwaa tuzo hiyo. Amuneke aliwahi kutwaa tuzo hiyo mwaka 1994 akiwa na klabu ya Zamalek ya Misri. Hii ndio list ya washindi wa tuzo hiyo kuanzia mwaka 1994 – 2014
1994 Emmauel Amuneke (Zamalek/Misri)
1995 – George Weah (PSG/AC Milan)
1996 – Nwankwo Kanu (Ajax/Inter Milan)
1997 – Victor Ikpeba (AS Monaco)
1998 – Mustapha Hadji (Deportivo La Coruña)
1999 – Nwankwo Kanu (Arsenal)
2000 – Patrick Mboma (Parma/Cagliari)
2001 – El Hadji Diouf (RC Lens)
2002 – El Hadji Diouf (RC Lens/Liverpool)
2003 – Samuel Eto’o (Marlloca)
2004 – Samuel Eto’o (Marlloca/Barcelona)
2005 – Samuel Eto’o (Barcelona)
2006 – Didier Drogba (Chelsea)
2007 – Frédéric Kanouté (Sevilla)
2008 – Emmanuel Adebayor (Arsenal)
2009 – Didier Drogba (Chelsea)
2010 – Samuel Eto’o (Inter Milan)
2011 – Yaya Toure (Manchester City)
2012 – Yaya Toure (Manchester City)
2013 – Yaya Toure (Manchester City)
2014 – Yaya Toure (Manchester City)
2015 –  ………………………. ?
wpid-twitter-3-600x398
2- Cameroon ndio nchi iliowahi kutoa wachezaji wengi na kushinda tuzo hiyo. Hadi sasa kuna wachezaji sita wa Cameroon ambao wamewahi kushinda tuzo hiyo mara 11. Roger Milla (1976,1990), Thomas Nkono (1979,1982), Jean-Manga Onguene (1980), Theophile Abega (1984), Patrick Mboma (2000) na Samuel Eto’o (2003, 2004, 2005, 2010).
3 – Licha ya kufanikiwa kutwaa Kombe la mataifa ya Afrika mara saba, Misri imewahi kutoa mshindi wa tuzo hiyo mara moja pekee. Mahmoud Al-Khatib ndio mchezaji pekee wa Misri aliyewahi kutwaa tuzo ya mwaka 1983.
4 – Katika historia ya tuzo hizo, takwimu zinaonesha nchi za Afrika Magharibi ndio zinaongoza kutwaa tuzo hiyo. Baadhi ya nchi hizo ni Nigeria, Ghana, Guinea, Mali, Liberia, Togo na Ivory Coast wakifuatiwa na nchi za Afrika Kaskazini Algeria, Misri, Morocco na Tunisia.
23
Hawa ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa ujumla
5 – Hizi ni nchi 5 ambazo zimewahi kutwaa tuzo hiyo lakini hazijwahi kushinda taji la mataifa ya Afrika Guinea (Cherif Souleymane, 1972); Togo (Emmanuel Adebayor, 2008); Liberia (George Weah, 1989, 1995); Senegal (El Hadji Diouf, 2001, 2002); na Mali (Salif Keita, 1970 na Frederic Kanoute, 2007).
6- Morocco ndio nchi inayoongoza kwa kutwaa tuzo hiyo mara nyingi zaidi kwa nchi za Afrika Kaskazini. Morocco imewahi kushnda Kombe ka mataifa ya Afrika mwaka 1976 . Mchezaji wa kwanza wa Morocco kushinda tuzo hiyo alikuwa  Ahmed Faras 1975, Mohamed Timoumi 1985, Badou Zaki 1986 na Mustapha Hadji 1998 alitangazwa kuwa mshindi.
MMWEEEE
Hawa ndio wanaowania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika kwa wachezaji wa ndani
7 – Yaya Toure ndio mchezaji aliyetwaa tuzo hiyo mara nne mfululizo, baada ya kuchukua mwaka mwaka 2011 hadi mwaka 2014 lakini kwa mwaka 2015 bado anawania tuzo hiyo na Andrew Ayew na Pierre-Emerick Aubemayang. January 7 ndio siku ya utolewaji wa tuzo hizo zitakazofanyika Abuja Nigeria.

Wednesday, January 6, 2016


Baada ya kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez, January 6 ndio siku ambayo ameongea kauli yake ya kwanza toka atimuliwe kazi na nafasi yake ichukuliwe na Zinedine Zidane.  Benitez amefunguka na kumshukuru kila mmoja ndani ya Real Madrid.
“Kwa sasa nimeondoka Real Madrid kama kocha, napenda kuaga na kumshukuru kila mmoja ndani ya klabu, nataka kila mmoja ndani ya klabu kuanzia mashabiki, bodi ya uongoz wafahamu kuwa naheshimu na ni heshima kwangu kupewa nafasi ya kuifundisha klabu kama Real Madrid” >>> Benitez
Benite
Kocha huyo ambaye hakufanya vizuri ndani ya Real Madrid, aliwahi kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005 akiwa na Liverpool, Kombe la Laliga akiwa na Valencia na Kombe la klabu Bingwa dunia akiwa na klabu ya Inter Milan ya Italia.

waliotembelea blog