Friday, January 8, 2016

FA CUP, ambalo sasa linaitwa Emirates FA Cup kwa sababu za kiudhamini na ni Kombe kongwe kabisa Duniani, litaanza kurindima Ijumaa Usiku huko England kwa Mechi pekee huko Mjini Exeter kati ya Exeter City FC na Liverpool.
Huu ni mwanzo wa Mechi za Raundi ya 3 FA CUP, inayoshirikisha jumla ya Timu 64, ambayo Klabu za Ligi Kuu England na Daraja la chini yake, The Championship, huanzia kampeni zao na nyingine hufuzu toka Raundi zake za awali kabisa.
Exeter City, Timu ya Ligi 2, ambayo ni Daraja la 4 kwa Mfumo wa England, wamefanikiwa kutinga Raundi ya 3 na sasa ni Wenyeji wa Klabu kigogo Liverpool.

Raundi hii ya 3 imeibua Mechi 5 za Timu za Ligi Kuu England kuvaana wenyewe kwa wenyewe na moja ya hizo ni ile Mechi tamu huko White Hart Lane ambako Tottenham watawavaa ‘Maajabu’ ya Ligi Kuu England Leicester City ambao wako Nafasi ya Pili katika Msimamo wa Ligi hiyo. Arsenal, ambao ndio Mabingwa Watetezi baada ya kulitwaa Kombe hili kwa mara ya pili mfululizo Mwezi Mei Mwaka huu, Jumamosi watakuwa kwao Emirates kucheza na Sunderland wakati Mabingwa Watetezi wa Ligi Kuu England, Chelsea, Jumapili wapo kwao Stamford Bridge kucheza na Timu ya Daraja la chini Scunthorpe United.
Siku ya Jumamosi Manchester United wapo kwao Old Trafford kucheza na Sheffield United wakati Man City wako Ugenini kucheza na Norwich City.

FA CUP
Raundi ya 3
Ijumaa Januari 8

22:55 Exeter v Liverpool

Jumamosi Januari 9
15:45 Wycombe v Aston Villa
[Mechi kuanza Saa 12:00 Jioni]
Arsenal v Sunderland
Birmingham v Bournemouth
Brentford v Walsall
Bury v Bradford
Colchester v Charlton

Doncaster v Stoke
Eastleigh v Bolton
Everton v Dag & Red
Hartlepool v Derby
Huddersfield v Reading
Hull v Brighton
Ipswich v Portsmouth
Leeds v Rotherham
Middlesbrough v Burnley
Newport v Blackburn
Northampton v MK Dons
Norwich v Man City
Nottm Forest v QPR
Peterborough v Preston
Sheff Wednesday v Fulham
Southampton v Crystal Palace
Watford v Newcastle
West Brom v Bristol City
West Ham v Wolves
20:30 Man United v Sheffield United

Jumapili Januari 10
15:00 Oxford United v Swansea
17:00 Carlisle v Yeovil
17:00 Chelsea v Scunthorpe
19:00 Tottenham v Leicester
21:00 Cardiff v Shrewsbury



THE EMIRATES FA CUP 2015/16
TAREHE MUHIMU
Raundi ya 3
Ijumaa 9 Januari 2016
Raundi ya 4

Jumamosi 30 Januari 2016
Raundi ya 5
Jumamosi 20 Februari 2016

Raundi ya 6-Robo Fainali

Jumamosi 12 Machi 2016

Nusu Fainali
Jumamosi 23 Aprili 2016 & Jumapili 24 Aprili 2016
Fainali Jumamosi 21 Mei 2016

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog