Wednesday, January 6, 2016


Baada ya kufukuzwa kazi kwa aliyekuwa kocha wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Rafael Benitez, January 6 ndio siku ambayo ameongea kauli yake ya kwanza toka atimuliwe kazi na nafasi yake ichukuliwe na Zinedine Zidane.  Benitez amefunguka na kumshukuru kila mmoja ndani ya Real Madrid.
“Kwa sasa nimeondoka Real Madrid kama kocha, napenda kuaga na kumshukuru kila mmoja ndani ya klabu, nataka kila mmoja ndani ya klabu kuanzia mashabiki, bodi ya uongoz wafahamu kuwa naheshimu na ni heshima kwangu kupewa nafasi ya kuifundisha klabu kama Real Madrid” >>> Benitez
Benite
Kocha huyo ambaye hakufanya vizuri ndani ya Real Madrid, aliwahi kutwaa taji la klabu Bingwa Ulaya mwaka 2005 akiwa na Liverpool, Kombe la Laliga akiwa na Valencia na Kombe la klabu Bingwa dunia akiwa na klabu ya Inter Milan ya Italia.

Tuesday, January 5, 2016


MENEJA wa Liverpool Jurgen Klopp yupo hatua za mwisho kukamilisha usajili wake wa kwanza wa Mchezaji mpya na huyo ni Marko Grujic.
Grujic, mwenye Miaka 19, Leo ametua Anfield kwa upimwaji wake wa afya ili kukamilisha Dili ya Pauni Milioni 5.1 kutoka Red Star Belgrade.
Inatarajiwa baada ya kukamilika kwa Uhamisho wake kwenda Liverpool, Kinda huyo atarudi kuichezea kwa Mkopo Red Star hadi mwishoni mwa Msimu na kujiunga na Liverpool kwa ajili ya Msimu ujao.
Liverpool imelazimika kufanya uamuzi wa kumnunua Grujic hivi sasa kwa sababu alikuwa akiwindwa pia na Klabu za Russia, CSKA Moscow na Zenit St Petersburg, ambazo zilitoa Dau kubwa, ikiaminika kuwa ni zaidi ya Pauni Milioni 7.

Lakini Kijana huyo aliamua mwenyewe kujiunga na Liverpool baada ya Msaidizi wa Klopp, Zeljko Buvac, ambae anatoka Serbia, kuingiliwa kati na kuleta ushawishi mkubwa kumchota Kijana huyo anaechezea Timu ya Taifa ya Serbia ya U-21.



Kamati ya maadili ya FIFA imependekeza katibu mkuu wa shirikisho hilo linalosimamia soka duniani Jerome Valcke asimamishwe kujihusisha na mchezo wa soka kwa miaka tisa.
Katibu huyo anadaiwa kutumia vibaya pesa ikiwemo uuzaji wa tiketi za kombe la duniani lililopita pamoja na kukiuka sheria za Shirikisho hilo.
Awali kamati ya nidhamu alimsimamisha katibu huyo kwa siku 90 kutojihusisha na mchezo wa soka ambapo adhabu yake imemalizika leo lakini ameongezewa adhabu kwa siku nyingine 45 wakati uchunguzi ukiendelea.
Jerome ataungana na viongozi wengine Sepp Blatter aliyekuwa Rais wa FIFA pamoja na makamu wake Michel Platini ambao wote wamesimamishwa tangu mwezi uliopita kwa miaka nane baada ya uchunguzi wa tuhuma za matumizi mabaya ya fedha kukamilika.

Mshambuliaji wa klabu ya Manchester united Wyne Rooney ametangazwa kuwa mchezaji bora kwa mwaka 2015 kwa mara nyingine.
Hii inakuwa mara ya pili staa huyo wa England kuchaguliwa mchezaji bora na mashabiki wa ligi kuu baada ya mwaka 2014 kushinda pia mwaka 2008 na  2009.
Pia kipa wa Stoke City Jack Butland amechaguliwa kuwa kipa bora kwa timu ya vijana chini ya miaka 21.
Rooney amefanikiwa kuibuka na shindi huo kwa mara nyingi baada ya kufunga jumla ya mabao 51 na kuvunja rekodi ya Bobby Charlton aliyefunga magoli 49.
Unataka kutumiwa MSG za habari zote kubwa kutoka kwa Millard Ayo? ukiwa na line ya tiGO andika ‘AYO’ tuma kwenda 15510, msg utayotumiwa jibu OK ili uanze kupokea matukio yote kwa sms, pia ungana na Millard Ayo kwenye Twitter, FB, Instagram na YouTUBE wa kubonyezahapa>>>INSTAGRAM TWITTER FB YOUTUBE.

Kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani Pep Guardiola December 29 aliingia kwenye headlines baada ya kutua Kenya kwa ajili ya mapumziko ya sikukuu ya Christimas na mwaka mpya, ujio wake Kenya uliwashangaza wengi kutokana na kuja kimya kimya. Ninazo pichaz za Pep Guardiola akitalii Kenya wakati ambao vilabu vya Chelsea na Man United vikitajwa kwa kiasi kikubwa kumuhitaji kocha huyo kwa ajili ya msimu ujao.
CXyZFP-WYAAvYTJ
Lakini Man City wanatajwa kuingia nae mkataba wa awali. Pep Guardiola ambaye aliwahi kuifundisha klabu ya FC Barcelona na sasa FC Bayern Munich ya Ujerumani amethibitisha kuwa hatoendelea kuifundisha Bayern Munich baada ya msimu kumalizika, hivyo wengi wanasubiria ataenda kuifundisha klabu gani baada ya FC Bayern Munich?
1919039_621862621288508_8491208548875364896_n
CXuOrMiWYAArySp
CXuOumqWMAASXK9

Monday, January 4, 2016



Baada ya kuwepo na tetesi za muda mrefu kuhusu uongozi wa klabu ya Real Madrid kutoridhishwa na mwenendo wa timu yao January 4, umetangaza rasmi kumfuta kazi aliyekuwa kocha wa klabu hiyo Rafael Benitez. Real Madrid walitangaza kumfuta kazi Benitez na Zidane kutajwa kurithi nafasi hiyo kwa muda hadi mwisho wa msimu.
Kufuatia kuteuliwa kwa Zidane kurithi mikoba hiyo, stori zilimfikia mchezaji mwenzake wa zamani David Beckham na kuonesha furaha yake kwa kupost picha yao ya zamani na ujembe wenye kuoneshwa kufurahishwa na nguli huyo wa kifaransa kuchukua mikoba hiyoo.
“Unaweza kumpata mtu bora zaidi yake? mtu ambaye alikuwa bora kiwanjani na watu wote tunampenda, anachukua nafasi ya kutumikia klabu ambayo mimi na watu wengine tunaipenda, mtu mwenye passion na siku zote huwa hakubali kushindwa kwa namna yoyote ile. Kiukweli ni mtu sahihi kwa hiyo kazi” >>> Beckham
1
David Beckham na Zinedine Zidane waliwahi kucheza pamoja kwa miaka mitatu katika timu ya Real Madrid, baada ya David Beckham kuhama Man United na kuhamia Real Madrid mwaka 2003. Hata hvyo Jose Mourinho anatajwa kuhusishwa na Madrid kutaka kurudi mwishoni mwa msimu.


Pamoja na mabingwa watetezi wa ligi kuu ya England Chelsea kupoteza matumaini ya kutwaa ubingwa kwa mara nyingine lakini kocha wao mpya Guus Hiddink ana mipango mingine ya ushindi.
Baada ya ushindi wa jana wa mabao 3-0 Hiddink amesema klabu yake hiyo inaweza kumaliza ligi hiyo ikiwa katika nafasi nne bora za juu mwishoni mwa msimu huu.
Klabu hiyo ya Stamford Bridge imeenda mechi nne bila kufungwa, kwa mara ya kwanza msimu huu, na kupanda hadi nafasi ya 14 kwenye msimamo wa ligi.
Hata hivyo, bado wanapungukiwa na alama 13 kuweza kufuzu kcheza Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya.
Alisema ligi ni ngumu lakini pia ni rahisi kushinda hivyo watapambana kuhakikisha wanashika nafasi za juu.
Hiddink alichukua nafasi ya kuifundisha timu hiyo kwa muda baada ya kocha wa awali Jose Mourihno kuondolewa kutokana na mwenendo mbaya wa timu.

waliotembelea blog