Wednesday, December 2, 2015


Kipa mkongwe nchini, Ivo Mapunda amejiunga na Azam FC. Ivo atapewa mkataba wa mwaka mmoja na Mtedaji Mkuu wa Azam FC, Saad Kawemba amesema kipa huyo amesajiliwa baada ya pendekezo la Kocha Stewart Hall. “Kocha alisema anataka kipa mzoefu nasi tukampa nafasi hiyo,” alisema. “Lakini mkataba hauwezi kuzidi mwaka mmoja kwa kuwa huenda Ivo atakuwa na mipango yake mingine,” alisema. Ivo aliomba kufanya mazoezi na kikosi cha Azam FC baada ya kuachwa na Simba katika hatua za mwisho kabisa za usajili baada ya uongozi wa Msimbazi, kusema alikuwa akiwasumbua licha ya kuwa wameishampa fedha

Sunday, November 29, 2015


Bale akipongezwa kwa bao lake la kwanza kwa Real Bale na Cristiano RonaldowakipongezanaRonaldo akishangilia PatashikaVuta nikuvute!


Timu ya Taifa ya Vijana wenye umri chini ya miaka 15 (U15) leo hii imekabidhiwa bendera ya Taifa na Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo, Profesa Elisante Ole Gabriel katika hosteli za TFF zilizopo Karume jijini Dar es salaam. Akiongea wakati wa kukabidhi bendera kwa timu hiyo ya vijana, Ole Gabriel amewashukuru TFF kwa kuwekeza katika soka la vijana, na kusema mafaniko yote yanandaliwa chini, hivyo analipongeza Shirikisho kwa kuamua kuwalea na kuwaendeleza vijana hawa wenye vipaji kwa manufaa ya taifa ya baadae.


Tottenham wameikosa nafasi ya kupanda kwenye Ligi Kuu England na kukamata Nafasi ya 4 baada ya kutoka 0-0 na Chelsea kwenye Mechi ya Dabi ya London iliyochezwa White Hart Lane.
Sare hii imewabakisha Tottenham Nafasi ya 5 na kuwaweka Chelsea Nafasi ya 14.
Katika Kipindi cha Kwanza, Kipa wa Chelsea, Asmir Begovic, ndie alisumbuka sana kwa kuokoa michomo kadhaa ikiwepo ile ya out Son Heung-min, kwa Kichwa, na Shuti la chini la Mousa Dembele.
Leo Meneja wa Chelsea Jose Mourinho alimpia Benchi Diego Costa na kumuanzisha Eden Hazard kama Fowadi kitu ambacho kilimkera Costa alieonekana kuvua gwanda lake la juu na kulitupa alipo Mourinho alipoona haingizwi.


Schweinsteiger aliisawazishia bao Man United katika dakika ya 45 kipindi cha kwanza na kwenda mapumziko sare ya 1-1.
Kipindi cha kwanza dakika ya 24 Vardy anaipa bao la kuongoza Timu yake Leicester City na kuongoza bao 1-0 dhidi ya Man United.VIKOSI:
Leicester City wanaoanza XI:
Schmeichel, Simpson, Morgan, Huth, Fuchs, Mahrez, Kante, Drinkwater, Albrighton, Okazaki, Vardy
Akiba: De Laet, King, Schlupp, Ulloa, Dyer, Schwarzer, Inler
Manchester United wanaoanza XI: De Gea, Darmian, Smalling, Blind, McNair, Carrick, Schweinsteiger, Young, Mata, Martial, Rooney
Man Utd akiba: Depay, Romero, Fellaini, Schneiderlin, Rashford, Jackson, Andreas Pereira

Manchester United wametoka Sare 1-1 huko King Power Stadium walipotoka 1-1 na Leicester City na matokeo haya kuiruhusu Man City kutwaa uongozi wa Ligi Kuu England.
Leicester walitangulia kufunga kwa Bao la Jamie Vardy katika Dakika ya 24 na kumfanya avunje Rekodi ya Mchezaji wa zamani wa Man United, Ruud Van Nistelrooy, aliyoiweka Mwaka 2003 ya kufunga katika Mechi 11 mfululizo za Ligi Kuu England.
Man United walisawazisha katika Dakika ya 45 kwa Bao la kichwa la Bastian Schweinsteiger na walistahili kushinda kwenye Kipindi cha Pili kwa jinsi walivyotawala lakini tatizo lao sugu la kutokuwa na Wachezaji wenye kasi na Wafungaji liliwakisha.

Saturday, November 28, 2015


LIGI KUU ENGLAND:
Jumamosi Novemba 28
1800 Aston Villa v Watford
1800 Bournemouth v Everton
1800 Crystal Palace v Newcastle
1800 Man City v Southampton
1800 Sunderland v Stoke
2030 Leicester v Man United

Jumapili Novemba 29
1500 Tottenham v Chelsea
1705 West Ham v West Brom
1915 Liverpool v Swansea
1915 Norwich v Arsenal



Kocha wa klabu ya FC Bayern Munich ya Ujerumani ambaye amewahi kuifundisha kwa mafanikio klabu ya FC Barcelona ya Hispania Pep Guardiola amekuwa akihusishwa kutakiwa kujiunga na klabu ya Manchester City ya Uingereza kwa muda mrefu sasa ila November 27 ameingia tena katika headlines kuhusiana na mpango huo.
2EC81B8E00000578-3336115-image-a-61_1448617745414
Headlines za kocha huyo kuwa njiani kujiunga na Man City zinapata nguvu kutokana na mkataba wake wa kuifundisha Bayern kuwa utamalizika mwishoni mwa msimu wa 2015/2016 na Man City wameahidi kumlipa kocha huyo zaidi ya mshahara wa pound milioni 13.2 ambao analipwa kocha wa sasa wa Chelsea Jose Mourinho.
g
Hawa ndio makocha wanaoongoza kwa kulipwa mishahara mikubwa duniani na Guardiola anashika nafasi ya tatu.
Dalili tatu za kocha huyo kuwa atajiunga na Man City ni kutokana na kutosaini mkataba mpya na klabu ya FC Bayern, kutotokea katika mkutano na waandishi wa habari November 27 na badala yake kuwakilishwa na beki wake Jerome Boateng na yeye kutajwa kuwa na appointment zake binafsi ndio maana hakutokea na tatu kuahidiwa kuwa atakuwa kocha anayeongoza kwa kulipwa mshahara mkubwa duniani.

waliotembelea blog