Sunday, May 25, 2014


  • Mkutano kuonyeshwa moja kwa moja na Star TV
 Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikagua jukwaa la wageni waalikwa kwenye uwanja wa People's Singida.
 Katibu wa NEC itikadi na Uenezi Nape Nnauye akikagua jukwaa la kuhutubia ,wengine pichani ni Maafisa wa Chama Makao Makuu Nyakia Ally (kushoto) na Octavian Kimario(kulia)
 Magari ya kurushia matangazo yakiwa tayari kwenye eneo la mkutano.
 Mafundi mitambo wa Star TV wakiweka sawa mitambo yao, mkutano huu utaenda live mnamo muda wa saa tisa mchana.
 Star TV wakiendelea kufunga vyombo vya kurushia matangazo ya mkutano moja kwa moja kutoka viwanja maarufu vya People's Singida.
 Uwanja wa People's unavyoonekana wakati wa maandalizi.




Nahodha wa Real Madrid, Iker Casillas akiwa ameinua Kombe la Ligi ya Mabingwa Ulaya baada ya kuwafunga jirani zao, Atletico mabao 4-1 usiku huu Uwanja wa Luz mjini Lisbon, Ureno. Hilo linakuwa taji la 10 la michuano hiyo kwa Real.
Uplifting: Ronaldo gets his hands on the trophy in Lisbon after Real's extra time victory
Mfungaji wa bao la nne la Real, Cristiano Ronaldo akiwa ameinua Kombe
Landmark: Real Madrid's players celebrate their 10th European Cup triumph
Kikosi cha Real Madrid kikifurahia na Kombe hilo.

Wednesday, May 21, 2014



01_a939d.jpg
1_90ea0.jpg
2_a9106.jpg
3_0dd77.jpg
4_b7898.jpg
5_a1af1.jpg



 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akizungumza na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,[
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akifuatana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,baada ya mazungumzo 
 Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dkt.Ali Mohamed Shein akiagana na Balozi mteule wa Tanzania nchini Sweden Mhe,Dora Msechu , aliyefika Ikulu Mjini Zanzibar leo,baada ya mazungumzo

Shirika la kutetea haki za binadamu Human rights watch limeishutumu serikali ya Somalia kwa kuwanyima wafungwa haki za uakilishi wa wakili na kuwashitaki raia wa kawaida chini ya mahakama za kijeshi.
Shirika hilo limesema kuwa mamia ya raia wanahukumiwa kwa sheria kali wasizoelewa. Human rights watch pia imesema kuwa raia wengi wamejikuta matatani baada ya kukamatwa katika msako wa kitaifa unaofanywa na mashirika ya kijasusi ya Somalia na mara nyingie wanazuiliwa kwa muda mrefu bila kufunguiwa mashtaka.
Kuzuiliwa kwa muda mrefu ni tatizo ndogo sana kwa raia hao wa Somalia ikilinganishwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na kutishia usalama wa nchi. Ukipatikana na hatia, hukumu ni kifo.
Licha ya kuwa mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakipinga kutolewa hukumu hii, Somalia ni mojawepo ya nchi chache Afrika ambayo bado inatoa huku hiyo.
Wasiwasi mkubwa ni kwamba, washukiwa hawapewi fursa ya kujitetea. Na wala mahakama hizi za kijeshi hazihitaji ushahidi mwingi kuamua kuwa una hatia.(P.T)
Human rights Watch imetaja katika ripoti yao kisa kimoja ambapo zaidi ya kesi 24 zilisikilizwa na kuamuliwa kwa chini ya siku 4.
Mahakama yajitetea
Lakini akijibu madai hayo, mwenye kiti wa mahakama za kijeshi wa Somalia Liban Cali Yarow ameambia BBC kuwa ni upuuzi mtupu na mwingilio wa jamii ya kimataifa katika mambo yasiyowahusu.
''Haya mashirika ni ya nje, na hayajui mambo yanayofanyika nchini kwetu. Inasikitisha kwamba hawazungumzii matatizo yetu ila wanapiga kelele tunapojaribu kujitatulia wenyewe. Ripoti hiyo imejaa madai yasiyo kweli.''
Human rights watch iliwahoji zaidi ya watu 30 na familia za watu walio shutumiwa, na wengi wao wamesema kuwa mahakama hizo haziwapi wafungwa nafasi ya kujitetea.
Mara nyingine hata kuwalazimisha kukiri mashtaka ambayo hawakufanya na hakuna ruhusa ya kukata rufaa. Hapa ndipo mwisho wa kesi.
Jamii ya kimataifa
Sasa shirika hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa na hasa wafadhili kushinikiza Somalia kurejesha haki za wafungwa na kuzuia raia kushtakiwa katika mahakama za kijeshi.
Lakini mwenyekiti wa mahakama hiyo Liban Cali Yarow amepuuzilia mbali ripoti ya shirika hilo akisema kuwa imejaa madai ya uongo.
''Ningependa kumsihi yeyote ambaye ana malalamiko juu yetu awasilishe kwetu badala ya kuandika kwenye magazeti. Kuandika tu bila kutushauri ni sawa na kutuwekelea madai ya uongo.'' Amesema Liban Yarow.
Maafisa wa Somalia wametetea hatua ya kuwashtaki washukiwa wa ugaidi katika mahakama za kijeshi wakisema kuwa mahakama za kiraia hazina ulinzi wa kutosha na uwezo wa kusikiliza kesi zenye uzito mkubwa kiasi hicho.



 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akizungumza na ujembe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea ofisini kwake kuwaalika wasanii kutoka Tanzania kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo kwa lengo la kudumisha amani na mshikamano katika nchi za maziwa makuu. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akifafanua jambo kwa wajumbe wa maandalizi ya fiesta kutoka Congo walipomtembelea ofisini kwake, kulia ni mratibu wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bw. Faso Mushigo Celestin na katikati ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara wapili kushoto akipokea zawadi kutoka kwa wajumbe kutoka Congo waliokuja nchini kuwaalika wasanii wa Tanzania kushiriki fiesta nchini Congo, kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiangalia CD iliyorekodiwa matukio mbalimbali ya fiesta ya mwaka jana ilivyokuwa nchini Congo. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Picha na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM

Na: Genofeva Matemu 
Wasanii wa muziki nchini waalikwa kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo zinazotarajiwa kufanyika julai 16 hadi 26 mwaka huu.
Mwaliko huo umetolea na wajumbe kutoka Congo walioshiriki katika siku ya Uanuwai wa Utamaduni duniani iliyoadhimishwa kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar es Salaam na baadaye kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt Fenella Mukangala  ofisini kwake ambapo walimuomba wasanii wa muziki kutoka Tanzania kushiriki sherehe fiesta zitakazofanyika nchini Congo mwaka huu.
Akitoa ufafanuzi kuhusiana na sherehe hizo Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga amesema kuwa lengo la sherehe za fiesta mwaka huu ni kuwakutanisha wasanii wa Afrika wanaoishi nchi za maziwa makuu ili waweza kupata nafasi ya kupanda mti wa amani ikiwa na lengo la kuziwezesha nchi hizo kuwa na mazungumzo ya amani.
Bi. Gizenga amesema kuwa wanatarajia kupata wasanii wa muziki kutoka nchini Tanzania, Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na wasanii wa Congo watakaoshiriki fiesta ndani ya mikoa miwili nchini Congo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini Goma pamoja na Kivu ya Kusini Bukavu.
“Tumezunguka nchi zilizopo katika maziwa makuu tukiwaomba wasanii wa nchi hizo kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo ambazo mwaka huu tutahusisha upandaji wa mti wa amani tukizitaka nchi hizo ziwe na mazungumzo ya amani na mshikamano” alisema Bi. Gizenga.
Kwa upande wake waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara amewashukuru wajumbe hao kwa mwaliko na kuwahaidi kuwa wasanii kutoka nchini Tanzania watapata fursa ya kipekee hivo ni muhimu kwao kushiriki ili waweze kuiwakilisha Tanzania na kuweza kupata uzoefu kutoka nchi jirani.
Aidha Dkt. Mukangara amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kushiriki katika sherehe hizo kwani Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuleta amani ya nchi ya Congo hivyo aina budi kushiriki na kuendeleza amani na mshikamano wa nchi hizo mbili.



 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akiwa katika mazungumzo na Katibu Mkuu Kiongozi wa Japan, Yoshihiro Suga, wakati alipofika ofisini kwake Jijini Tokyo Japan leo Mei 21, 2014, akiwa katika ziara ya kikazi. Picha na OMR



Serikali ya Japan imeelezea nia yake ya kuendelea kuchangia bajeti ya Tanzania na kufafanua kuwa, inafanya hivyo kwa kutambua kuwa Tanzania ni mshirika mkubwa wa maendeleo na kwamba ni nchi yenye kutia matumaini katika kupiga hatua za kimaendeleo.
Akizungumza jana katika Ofisi yake jijini Tokyo, Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan Mheshimiwa Yoshihide Suga alisema, serikali ya Japan inaifahamu Tanzania kama mshirika wa maana katika maendeleo na kwamba inafahamu mchango wa Tanzania katika kuendeleza ushirikiano wa nchi za Afrika Mashariki. Katibu Mkuu huyo pia aliongeza kuwa, Tanzania imemudu kudumisha amani kwa kipindi kirefu huku ikipiga hatua za kimaendeleo na kwamba watu wake wamebakia wamoja kwa miaka mingi licha ya kuwa na tofauti za kitamaduni, kijiografia na kidini.
Kauli hiyo ya Katibu wa Baraza la Mawaziri wa Japan, imetolewa kufuatia mkutano wake na Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt. Mohammed Gharib Bilal ambaye yupo jijini Tokyo kwa ziara ya kikazi. Katibu huyo alisema, “tunaifahamu Tanzania kama nchi muhimu inayodumisha amani. Nchi yenu imeweza kudumisha Muungano kwa miaka 50, Japan inawapongeza sana. Tunafahamu mnafanya kazi kubwa katika kuwaendeleza wananchi wenu na sisi kama ndugu na rafiki zenu tuko tayari kabisa kushirikiana nanyi.”
Katibu Mkuu Suga alieleza pia kuwa, Tanzania ni nchi iliyo thabiti katika ukanda wa Afrika Mashariki na inayo nguvu katika kuhakikisha ukanda huu unaendeleza utengamano hali ambayo inachangia kuwepo maingiliano ya wananchi wa ukanda wa Afrika Mashariki sambamba na kutanua fursa kwa wawekezaji kutoka nje ya Afrika.
“Mko thabiti katika mambo mengi na hasa kuweza kumudu kuwa na amani na utulivu, mnategemewa sana na nchi za Afrika Mashariki na kwa hali hii sisi tupo tayari kuendelea kutenga fedha katika bajeti yetu kwa ajili ya kusaidia miradi mbalimbali ya Tanzania katika ushirikiano wa serikali na sekta binafsi (PPP),” alisema.
Kwa upande wake Mheshimiwa Makamu wa Rais Dkt. Bilal alimueleza Katibu Mkuu Suga kuwa, Tanzania inapokea kwa heshima kubwa mchango wa Japan kwa kutambua hali yake ya utulivu na kwamba anatumia ziara yake Japan kuhamasisha wawekezaji kuja kuwekeza Tanzania.

“Tuna kazi kubwa mbele yetu katika kuwaendeleza Watanzania. Hatuwezi kufanya kazi hiyo peke yetu, hivyo basi nitumie nafasi hii kukuomba Mheshimiwa Katibu Mkuu kutusaidia kuhamasisha wawekezaji kutoka Japan ili waje kushirikiana nasi katika kuiendeleza Tanzania. Urafiki kati yenu na sisi ni wa siku nyingi na tungetegemea sasa tuubadili na utazame fursa za kuchangiana kiuchumi na hasa katika kuwekeza kwa kubadilishana teknolojia pamoja na mtaji,” Makamu wa Rais alisema.
Mheshimiwa Makamu wa Rais yuko nchini Japan kwa ziara ya kikazi na tayari amefanikiw akukutana na wakuu wa makampuni mbalimbali makubwa duniani yenye makao yake makuu nchini Japan na kisha kutumia nafasi hiyo kuelezea fursa za uwekezaji nchini Tanzanja sambamba na kubainisha umuhimu wa sekta binafsi kushiriki katika kusaidia maendeleo ya nchi zinazoendelea zilizopo Afrika, Tanzania ikiwa ni kipaumbele.

waliotembelea blog