Shirika
la kutetea haki za binadamu Human rights watch limeishutumu serikali ya
Somalia kwa kuwanyima wafungwa haki za uakilishi wa wakili na
kuwashitaki raia wa kawaida chini ya mahakama za kijeshi.
Shirika
hilo limesema kuwa mamia ya raia wanahukumiwa kwa sheria kali
wasizoelewa. Human rights watch pia imesema kuwa raia wengi wamejikuta
matatani baada ya kukamatwa katika msako wa kitaifa unaofanywa na
mashirika ya kijasusi ya Somalia na mara nyingie wanazuiliwa kwa muda
mrefu bila kufunguiwa mashtaka.
Kuzuiliwa
kwa muda mrefu ni tatizo ndogo sana kwa raia hao wa Somalia
ikilinganishwa na kufunguliwa mashtaka ya ugaidi na kutishia usalama wa
nchi. Ukipatikana na hatia, hukumu ni kifo.
Licha ya
kuwa mashirika ya haki za binadamu yamekuwa yakipinga kutolewa hukumu
hii, Somalia ni mojawepo ya nchi chache Afrika ambayo bado inatoa huku
hiyo.
Wasiwasi
mkubwa ni kwamba, washukiwa hawapewi fursa ya kujitetea. Na wala
mahakama hizi za kijeshi hazihitaji ushahidi mwingi kuamua kuwa una
hatia.(P.T)
Human rights Watch imetaja katika ripoti yao kisa kimoja ambapo zaidi ya kesi 24 zilisikilizwa na kuamuliwa kwa chini ya siku 4.
Mahakama yajitetea
Lakini
akijibu madai hayo, mwenye kiti wa mahakama za kijeshi wa Somalia Liban
Cali Yarow ameambia BBC kuwa ni upuuzi mtupu na mwingilio wa jamii ya
kimataifa katika mambo yasiyowahusu.
''Haya
mashirika ni ya nje, na hayajui mambo yanayofanyika nchini kwetu.
Inasikitisha kwamba hawazungumzii matatizo yetu ila wanapiga kelele
tunapojaribu kujitatulia wenyewe. Ripoti hiyo imejaa madai yasiyo
kweli.''
Human
rights watch iliwahoji zaidi ya watu 30 na familia za watu walio
shutumiwa, na wengi wao wamesema kuwa mahakama hizo haziwapi wafungwa
nafasi ya kujitetea.
Mara nyingine hata kuwalazimisha kukiri mashtaka ambayo hawakufanya na hakuna ruhusa ya kukata rufaa. Hapa ndipo mwisho wa kesi.
Jamii ya kimataifa
Sasa
shirika hilo limetoa wito kwa jamii ya kimataifa na hasa wafadhili
kushinikiza Somalia kurejesha haki za wafungwa na kuzuia raia kushtakiwa
katika mahakama za kijeshi.
Lakini mwenyekiti wa mahakama hiyo Liban Cali Yarow amepuuzilia mbali ripoti ya shirika hilo akisema kuwa imejaa madai ya uongo.
''Ningependa
kumsihi yeyote ambaye ana malalamiko juu yetu awasilishe kwetu badala
ya kuandika kwenye magazeti. Kuandika tu bila kutushauri ni sawa na
kutuwekelea madai ya uongo.'' Amesema Liban Yarow.
Maafisa
wa Somalia wametetea hatua ya kuwashtaki washukiwa wa ugaidi katika
mahakama za kijeshi wakisema kuwa mahakama za kiraia hazina ulinzi wa
kutosha na uwezo wa kusikiliza kesi zenye uzito mkubwa kiasi hicho.
0 maoni:
Post a Comment