Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akizungumza na ujembe wa watu kutoka Congo hawapo pichani waliomtembelea
ofisini kwake kuwaalika wasanii kutoka Tanzania kushiriki katika
sherehe za fiesta nchini Congo kwa lengo la kudumisha amani na
mshikamano katika nchi za maziwa makuu. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe
za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
akifafanua jambo kwa wajumbe wa maandalizi ya fiesta kutoka Congo
walipomtembelea ofisini kwake, kulia ni mratibu wa sherehe za fiesta
kutoka Congo Bw. Faso Mushigo Celestin na katikati ni Mwenyekiti wa
sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Waziri
wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
wapili kushoto akipokea zawadi kutoka kwa wajumbe kutoka Congo waliokuja
nchini kuwaalika wasanii wa Tanzania kushiriki fiesta nchini Congo,
kushoto ni Mkurugenzi Idara ya Utamaduni Profesa Hermas Mwansoko.
Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Dkt. Fenella Mukangara akiangalia CD iliyorekodiwa matukio mbalimbali ya
fiesta ya mwaka jana ilivyokuwa nchini Congo. Kulia ni Mwenyekiti wa sherehe za
fiesta kutoka Congo Bi. Anne Gizenga.
Picha
na: Genofeva Matemu – Afisa Mawasiliano Serikalini WHVUM
Na: Genofeva Matemu
Wasanii wa muziki
nchini waalikwa kushiriki katika sherehe za fiesta nchini Congo zinazotarajiwa
kufanyika julai 16 hadi 26 mwaka huu.
Mwaliko huo umetolea
na wajumbe kutoka Congo walioshiriki katika siku ya Uanuwai wa Utamaduni
duniani iliyoadhimishwa kitaifa katika Viwanja vya Mnazi Mmoja leo jijini Dar
es Salaam na baadaye kumtembelea Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo
Mhe. Dkt Fenella Mukangala ofisini kwake
ambapo walimuomba wasanii wa muziki kutoka Tanzania kushiriki sherehe fiesta
zitakazofanyika nchini Congo mwaka huu.
Akitoa ufafanuzi
kuhusiana na sherehe hizo Mwenyekiti wa sherehe za fiesta kutoka Congo Bi. Anne
Gizenga amesema kuwa lengo la sherehe za fiesta mwaka huu ni kuwakutanisha
wasanii wa Afrika wanaoishi nchi za maziwa makuu ili waweza kupata nafasi ya
kupanda mti wa amani ikiwa na lengo la kuziwezesha nchi hizo kuwa na mazungumzo
ya amani.
Bi. Gizenga amesema
kuwa wanatarajia kupata wasanii wa muziki kutoka nchini Tanzania, Kenya,
Uganda, Rwanda, Burundi pamoja na wasanii wa Congo watakaoshiriki fiesta ndani
ya mikoa miwili nchini Congo katika mkoa wa Kivu ya Kaskazini Goma pamoja na
Kivu ya Kusini Bukavu.
“Tumezunguka nchi
zilizopo katika maziwa makuu tukiwaomba wasanii wa nchi hizo kushiriki katika
sherehe za fiesta nchini Congo ambazo mwaka huu tutahusisha upandaji wa mti wa
amani tukizitaka nchi hizo ziwe na mazungumzo ya amani na mshikamano” alisema
Bi. Gizenga.
Kwa upande wake
waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Mhe. Dkt. Fenella Mukangara
amewashukuru wajumbe hao kwa mwaliko na kuwahaidi kuwa wasanii kutoka nchini
Tanzania watapata fursa ya kipekee hivo ni muhimu kwao kushiriki ili waweze
kuiwakilisha Tanzania na kuweza kupata uzoefu kutoka nchi jirani.
Aidha Dkt. Mukangara
amesema kuwa ni muhimu kwa Tanzania kushiriki katika sherehe hizo kwani
Tanzania ilishiriki kwa kiasi kikubwa katika kuleta amani ya nchi ya Congo
hivyo aina budi kushiriki na kuendeleza amani na mshikamano wa nchi hizo mbili.
0 maoni:
Post a Comment