Sunday, December 13, 2015


Kila mtu ana kipaji chake katika maisha..wapo waliotamani kufanya hivi lakini mwisho wa siku wakajikuta wanafanya kitu kingine kabisa mbacho hawakudhamiria kufanya.
Kwa mchezaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast Yaya Toure kumbe endapo mambo yasingemnyookea kwenye soka basi angekuwa mcheza karate.
Huo ndio mchezo ambao kiungo huyo alikuwa ameanza kucheza wakati akiwa bado mdogo na huenda mpaka sasa angebaki kwenye mchezo huo endapo baba yake mzazi asingemkataza akihofia angepata majeraha kupitia mchezo huo.
Wakati akiwa mdogo katika kipindi cha wiki moja, alifanya vyema na aliweza kuteuliwa kushiriki katika mashindano makubwa yaliyofanyika Kenya ambayo hata hivyo hakwenda kutokana na baba yake kumzuia.
Kiungo huyo amekuwa na mafanikio makubwa kupitia soka na juzi alifanikiwa kushinda tuzo ya BBC aambayo huyolewa kila mwaka kwa mchezaji bora Afrika.



Michuano ya klabu Bingwa Dunia ilianza December 10 2015 katika ardhi ya Japan, hii ni michuano ambayo inatafuta Bingwa wa Dunia kwa ngazi ya vilabu, kwa upande wa bara la Afrika klabu ya TP Mazembe ya Jamuhuri ya Kidemokrasia ya Kongo ndio ilikuwa inawakilisha bara hili.
Generated by IJG JPEG Library
TP Mazembe ambayo inachezewa na watanzania wawili Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu, ilianza kucheza michuano hiyo December 13 katika hatua ya robo fainali dhidi ya klabu ya Sanfrecce na kukubali kipigo cha goli 3-0, huu ni mchezo ambao watanzania wengi walikuwa wanautazama, kwani Mbwana Samatta na Thomas Ulimwengu  wameweka rekodi ya kuwa watanzania wa kwanza kushiriki michuano hiyo.
Generated by IJG JPEG Library
Sanfrecce walianza kupata goli la kwanza dakika ya 44 kupitia kwa Shiotani ikiwa ni dakika moja imesalia kabla ya kwenda mapumziko. TP Mazembe walijitahidi kutafuta goli la kusawazisha ila dakika ya 56 kipindi cha pili Chiba akapachika goli la pili kwa Sanfrecce, licha ya TP Mazembe kutokata tamaa, goli la dakika ya 78 la Asano ndio lilihitimisha safari ya TP Mazembe kwenda hatua ya nusu fainali.
Generated by IJG JPEG Library
Generated by IJG JPEG Library

Saturday, December 12, 2015



LIGI KUU ENGLAND
RATIBA
Jumamosi Desemba 12

15:45 Norwich v Everton
18:00 Crystal Palace v Southampton
18:00 Man City v Swansea
18:00 Sunderland v Watford
18:00 West Ham v Stoke
20:30 Bournemouth v Man United

Jumapili Desemba 13
16:30 Aston Villa v Arsenal
19:00 Liverpool v West Brom
19:00 Tottenham v Newcastle

Jumatatu Desemba 14
23:00 Leicester v Chelsea


Leicester boss Claudio Ranieri poses with the manager of the month award at the club's training groundVINARA wa Ligi Kuu England Leicester City wamezoa Tuzo zote mbili za Ubora za Ligi hii kwa Mwezi Novemba kufuatia Claudio Ranieri kupewa Tuzo ya Meneja Bora na Straika Jamie Vardy kuwa ndie Mchezaji Bora.
Katika Mwezi Novemba, Vardy, mwenye Miaka 28, alifunga Bao katika Mechi zao zote 3 za Ligi na kuweka Rekodi ya kupiga Bao katika Mechi 11 mfululizo za Ligi.
Hii ni mara ya pili mfululizo kwa Vardy kutwaa Tuzo ya Mchezaji Bora wa Ligi Kuu England baada ya kuitwaa pia kwa Mwezi Oktoba.

It was a double celebration for Leicester as Jamie Vardy picked up the Player of the Month awardNae Ranieri ameiongoza Leicester kutwaa Pointi 7 kati ya 9 kwa Mwezi Novemba kwa kuzishinda Watford 2-1, Newcastle 3-0 na kutoka Sare 1-1 na Man United.
Mechi inayofuata kwa Leicester ni Jumatatu Usiku dhidi ya Mabingwa Watetezi Chelsea.


VARDY'S GOAL SCORING STREAK
Aug 8 - vs Sunderland - 1 goal (4-2 win)
Aug 29 - vs Bournemouth - 1 goal (1-1)
Sep 13 - vs Aston Villa - 1 goal (3-2 win)
Sep 19 - vs Stoke City - 1 goal (2-2)
Sep 26 - vs Arsenal - 2 goals (5-2 defeat)
Oct 3 - vs Norwich City - 1 goal (2-1 win)
Oct 17 - vs Southampton - 2 goals (2-2)
Oct 24 - vs Crystal Palace - 1 goal (1-0 win)
Oct 31 - vs West Brom - 1 goal (3-2 win)
Nov 7 - vs Watford - 1 goal (2-1 win)
Nov 21 - vs Newcastle - 1 goal (3-0 win)
Nov 28 - vs Man United - 1 goal (1-1)

Monthly winners
August: Andre Ayew (Swansea City)
September: Anthony Martial (Man United)
October: Jamie Vardy (Leicester City)
November: Jamie Vardy (Leicester City)



UEFA chief Michel Platini has lost his second appeal against FIFA's 90-day ban. Platini's first appeal against financial wrongdoing was rejected by the FIFA Appeal Committee and the Court of Arbitration for Sport has upheld it.

Friday, December 11, 2015



Mchezaji wa timu ya taifa ya Honduras Arnold Peralta ambaye amewahi kucheza katika vilabu vya Olimpia na Rangers ya Scotland ameuwawa kwa kupigwa risasi wakati akiwa katika Parking za magari jijini La Ceiba Honduras, Arnold Peralta alikuwa likizo nyumbani kwao Honduras.
Kifo cha Arnold Peralta ambaye anamudu kucheza nafasi ya kiungo kwa ufasaha kinachunguzwa na maafisa usalama wa nchi hiyo, ila taarifa za awali zinaonesha kuwa Arnold Peralta alipigwa risasi sio na majambazi ila inasadikika ni watu wenye visasi lakini tukio bado linachunguzwa.
Olympics+Day+2+Men+Football+Spain+v+Honduras+ENz_YKSG4G9l
Headlines za kifo cha Arnold Peralta kupigwa risasi zinakuja ikiwa ni mwaka mmoja umepita toka auwawe kwa risasi golikipa wa timu ya taifa ya Afrika Kusini na klabu ya Orlando Pirates Senzo Meyiwa, ambaye nae alipigwa risasi na majambazi ambao walienda kufanya uharifu katika nyumba ya mpenzi wake.
TL_1081310-602x400
Senzo Meyiwa


Kiungo wa kimataifa wa Ivory Coast na klabu ya Manchester City ya Uingereza Yaya Toure alikuwa ni mmoja kati ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa Afrika inayotolewa na shirika la utangazaji la Uingereza BBC, Yaya Toure amefanikiwa kuibuka na ushindii wa baada ya kupata kura nyingi zaidi ya Pierre-Emerick Aubameyang, Andre Ayew, Yacine Brahimi na Sadio Mane.
86610826_afoty-2015
List ya wachezaji watano waliokuwa wanawania tuzo ya mchezaji bora wa BBC
Kutwaa tuzo hiyo kwa Yaya Toure kunamfanya kuwa mchezaji wa tatu kuingia katika rekodi ya wachezaji wa zamani wa Nigeria Nwankwo Kanu na Jay-Jay Okocha ambaoo kila mmoja katwaa tuzo hiyo mara mbili, rekodi ambayo inashikiliwa na wachezaji watatu kwa sasa ikiwemo Toure.
e
List ya wachezaji waliowahi kutwaa tuzo hiyo
Toure kwa mara ya kwanza alifanikiwa kutwaa tuzo ya mchezaji bora wa mwaka wa BBC mwaka 2013, baada ya ushindi wa tuzo hiyo hii ni moja kati ya sentensi za Yaya Toure “Najivunia kupokea tuzo hii kutoka kwa mashabiki wangu siwezi kuamini”

waliotembelea blog