Kila mtu ana kipaji chake katika
maisha..wapo waliotamani kufanya hivi lakini mwisho wa siku wakajikuta
wanafanya kitu kingine kabisa mbacho hawakudhamiria kufanya.
Kwa mchezaji wa Manchester City na timu ya Taifa ya Ivory Coast Yaya Toure kumbe endapo mambo yasingemnyookea kwenye soka basi angekuwa mcheza karate.
Huo ndio mchezo ambao kiungo huyo
alikuwa ameanza kucheza wakati akiwa bado mdogo na huenda mpaka sasa
angebaki kwenye mchezo huo endapo baba yake mzazi asingemkataza akihofia
angepata majeraha kupitia mchezo huo.
Kiungo huyo amekuwa na mafanikio makubwa kupitia soka na juzi alifanikiwa kushinda tuzo ya BBC aambayo huyolewa kila mwaka kwa mchezaji bora Afrika.
0 maoni:
Post a Comment