Sunday, April 19, 2015


Alexis Sanchez celebrates his goalRaha ya Ushindi!Alexis Sanchez ndie aliyeipa ushndi Gunners leo dhidi ya Timu ya ReadingAlexis Sanchez celebrates scoring the first goal with team mates
Mabingwa Watetezi wa FA CUP, Arsenal, Leo hii Uwanja wa Wembley Jijini London, wameichapa Timu ya Daraja la chini la Championship, Reading, Bao 2-1 katika Nusu Fainali ya FA CUP.
Pasi safi ya Mesut Ozil ndiyo iliyompa nafasi Alexis Sanchez kuipa Bao la kwanza Arsenal Dakika ya 30 Bao ambalo lilidumu hadi Mapumziko.
Alexis Sanchez celebrates with team mates after scoring
Reading walisawazisha katika Dakika ya 54 kwa Bao la McCleary alieunganisha krosi ya Pogrebnyak kutoka kushoto kwa Goli.
Hadi Dakika 90 kumalizika Gemu ilikuwa 1-1 na kuongezwa Dakika za Nyongeza 30.
Alexis Sanchez aliipa Arsenal Bao la Pili na la ushindi katika Dakika ya 106 baada ya Shuti lake kumpenya Kipa Federici.
Nusu Fainali nyingine itachezwa Kesho, pia Uwanjani Wembley, kati ya Aston Villa na Liverpool.
Alexis Sanchez celebrates with Mesut Ozil after scoringAlexis Sánchez dakika ya 39 kipindi cha kwanza aliip Arsenal bao la kuongoza kwa kufanya 1-0 dhidi ya Readinng na kwenda mapumziko wakiwa wanaongoza kwa bao 1-0.

Kipindi cha pili dakika ya 54 Garath McCleary aliwasawazishia bao Reading na kufanya 1-1. 
Garath McCleary celebrates scoring his side's first goal
Kwenye muda wa ziada dakika 30 ili kuhitimisha dakika 120 dakika ya 105 Sánchez aliwaongezea bao la pili Arsenal na kufanya bao kuwa 2-1Olivier Giroud battles with Alex PearceGiroud akifanya yakeOlivier Giroud has a shot stopped by Adam FedericiKipa wa Reading akiuweka kwapani mpira uliopigwa na GiroudreadingOlivier Giroud heads the ballPatashika Aaron Ramsey reacts after a missed chanceAaron akipagawa baada ya kukosa nafasi ya wazi leo hiiAaron Ramsey has a shot saved by Adam FedericiKipa wa Reading akiwa kwenye kibarua Garath McCleary celebrates with team mates after scoringGarath McCleary aliposawazisha bao dakika ya 54Mesut Ozil and Danny Welbeck look dejected after Garath McCleary equalisedGunners wakijiuliza baada da ya Reading kusawazisha baoPer MertesackerReading players have a team talk before the matchKikosi cha Reading kikipanga jinsi ya kufanya Wembley usiku huu dhidi ya ArsenalVIKOSI:
Arsenal: Szczesny, Debuchy, Mertesacker, Koscielny, Gibbs, Coquelin, Ramsey, Cazorla, Ozil, Alexis, Welbeck
Akiba: Ospina, Gabriel, Monreal, Flamini, Wilshere, Walcott, Giroud

READING:
Federici, Gunter, Obita, Pearce, Hector, Williams, Chalobah, McCleary, Robson-Kanu, Mackie, Pogrebnyak
Akiba: Anderson, Kelly, Cooper, Karacan, Norwood, Cox, Yakubu


Luis Suárez(kulia) Akishangilia bao lake la dakika ya mapemaLuis Suárez leo kafanya maajabu kwa kuifungia Timu ya Barca bao ndani ya dakika 1 na kuipa bao la kuongoza 1-0 dhidi ya Valencia.
Dakika za majeruhi Lionel Messi alifunga bao lake la 400 na kufanya mchezo kumalizika kwa bao 2-0.2-0

 


WEKUNDU wa Msimbazi Simba wamefungwa magoli 2-0 na Mbeya City katika mechi ya ligi kuu soka Tanzania bara iliyochezwa uwanja wa Sokoine Mbeya jioni ya leo.
Kwa matokeo hayo Simba imeendelea kubaki nafasi ya tatu kwa pointi zake 35 baada ya kucheza mechi 22 nyuma ya mabingwa Azam fc wenye pointi 42 baada ya kushinda mechi yao leo mabao 2-1 dhidi ya Kagera.Azam nao wamecheza mechi 22.
Vinara bado wanabaki kuwa Yanga kwa pointi 46 baada ya kucheza mechi 21.
Magoli ya Mbeya City yalifungw ana Paul Nonga dakika ya 45 kipindi cha kwanza akipokea pasi kutoka kwa Deus Kaseke.
City walifunga goli la pili dakika ya 69 kupitia kwa Peter Mwalyanzi.


Simba ilipata pigo dakika ya 23 baada ya beki wake na nahodha, Hassan Isihaka kuumia na nafasi yake kuchukuliwa na Mganda Joseph Owino










Dakika 90 zimemalizika Mbeya City 2-0 Simba Sc, Simba wamekubali kichapo!!
Peter M. anaipatia bao la pili Mbeya City kwa kufanya 2-0 dhidi ya Simba

Saturday, April 18, 2015

MSIMAMO ULIVYO KWA SASA: CHELSEA KILELENI.
English Premier League
#
Team
GP
W
D
L
GF
GA
GD
PTS
1
Chelsea
31
22
7
2
64
26
38
73
2
Arsenal
32
20
6
6
63
32
31
66
3
Man United
32
19
8
5
59
30
29
65
4
Man City
32
18
7
7
65
34
31
61
5
Liverpool
32
17
6
9
47
36
11
57
6
Southampton
32
17
5
10
44
22
22
56
7
Tottenham
32
16
6
10
50
46
4
54
8
Swansea City
32
13
8
11
38
40
-2
47
9
West Ham
32
11
10
11
42
40
2
43
10
Stoke City
32
12
7
13
36
40
-4
43
11
Crystal Palace
32
11
9
12
42
43
-1
42
12
Everton
32
9
11
12
40
43
-3
38
13
Newcastle
32
9
8
15
33
51
-18
35
14
West Brom
32
8
9
15
30
46
-16
33
15
Aston Villa
33
8
8
17
24
45
-21
32
16
Sunderland
32
5
14
13
25
48
-23
29
17
Hull City
32
6
10
16
29
45
-16
28
18
QPR
33
7
5
21
38
59
-21
26
19
Burnley FC
32
5
11
16
26
50
-24
26
20
Leicester City
31
6
7
18
32
51
-19
25



Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi.

MSHITUKO wa matukio ya mfululizo ya ajali, umeendelea kugubika nchi, baada ya watu 20 kupoteza maisha katika ajali ya basi dogo aina ya Toyota Hiace, iliyotokea jana wilayani Rungwe mkoani Mbeya.

Ajali hiyo ambayo taarifa na picha zake zilisambaa kwa kasi katika mitandao ya kijamii, imesababisha taharuki kutokana na ukaribu wake na matukio mengine ya ajali yaliyotokea wiki hii.


Baadhi ya wakazi wa jirani na eneola tukio wakitazama gari lilivyopata ajali kando kando ya mto Kiwira.

Tangu Jumapili iliyopita mpaka jana, siku zisizozidi sita kumetokea ajali kubwa tatu zilizohusisha mabasi ya abiria na kuteketeza maisha ya watu 40.

Mbali na ajali hizo, wiki hii Kamanda wa Jeshi la Polisi Kikosi cha Usalama Barabarani, Mohamed Mpinga alitoa takwimu zilizosababisha huzuni kwa Watanzania, kwamba kati ya Januari mosi na Aprili 12 sawa na siku 102, watu 969 walipoteza maisha katika ajali za barabarani.

Wananchi wa Kiwira wakiangalia baadhi ya Miili ya Watu waliopoteza maisha kwenye ajali hiyo.

Ajali za wiki
Jumatano wiki hii, basi la Air Jordan lililokuwa likitokea mkoani Mwanza kwenda Arusha, lilipata ajali na kusababisha kifo cha mtu mmoja na majeruhi 20.

Ajali hiyo ilitokea wakati Watanzania wakiwa na kumbukumbu ya ajali iliyotokea Jumapili ya wiki jana, ambapo watu 19 waliteketea kwa moto, baada ya basi la Kampuni ya Nganga Express na lori aina ya Fuso kugongana uso kwa uso na kuwaka moto katika eneo la Iyovi, Milima ya Udzungwa, mkoani Morogoro.

Ajali ya Mbeya
Akizungumza na gazeti hili jana, Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mbeya, Mohamed Msangi, alisema ajali hiyo mpya imetokea katika eneo la Ilongo ambalo limebatizwa jina la Uwanja wa Ndege karibu na Kiwira, ambapo watu 18 walipoteza maisha papo hapo.

“Watu wanne waliojeruhiwa, mmoja alikuwa katika hali mbaya na kwa bahati mbaya alifia njiani wakati akipelekwa Hospitali ya Wilaya ya Rungwe kwa matibabu,” alisema Kamanda Msangi.
Kamanda Msangi alisema chanzo cha ajali hiyo ni mwendo kasi na dereva kutokuwa makini katika uendeshaji wake. Taarifa zilizotufikia baadae, zilieleza kuwa abiria mwingine aliyekuwa akipatiwa matibabu, alifariki akiwa hospitalini.

Mashuhuda
Mashuhuda wa ajali hiyo walidai kuwa chanzo cha ajali ni mwendokasi uliosababisha dereva ashindwe kumudu gari hilo katika mteremko wenye kona, akajikuta gari likimshinda na kutumbukia katika Mto Kiwira.
Walidai kuna uwezekano dereva huyo alikuwa akikimbizwa na baadhi ya madereva wa mabasi aina ya Toyota Coaster, yanayofanya safari zake kati ya Mbeya, Tukuyu na Kyela.


Ilikua mishale ya saa kumi kamili jioni ujumbe wa harakati za Imetosha ulipowasili katika kituo cha Buhangija cha kulea watoto wenye mahitaji maalumu mjini Shinyanga. Sauti za furaha za watoto zilisikika zikiimba nyimbo za kukaribisha ujumbe wa wana harakati hao ambao wako Mwanza kutambulisha harakati za Imetosha ambazo ni kupambana na kupinga unyanyapaa, ukatili na mauaji kwa watu wenye Ulemavu wa ngozi.

Balozi wa Imetosha Henry Mdimu akinunua mahitaji ya watoto waliopo kituoni hapo kabla ya kufika kituoni hapo.

Huyu ni Irene wa NHIF Shinyanga


Wajumbe wa Imetosha
Akiongea na watoto kituoni hapo Mwenyekiti wa harakati za Imetosha Masoud Ali (Kipanya) alisema Imetosha inatambua umuhimu wa haki ya kuishi kwa kila binadamu ndio maana Imetosha imeanzisha harakati za kutokomeza mauaji na unyanyapaa kwa watu wenye ulemavu wa ngozi. “Tunatambua hapa kati yenu kuna vipaji vya aina mbalimbali hivyo pamoja na kupambana na harakati za kupinga na kutokomeza mauaji ya watu wenye ulemavu wa ngozi tupo hapa kuwatia moyo kuwa mna uwezo mkubwa ndani yenu hivyo msijidharau” alisema Masoud.


Wachezaji wa Coastal Union wakipata darasa kutoka kwa Kiongozi (Meneja) wa Klabu hiyo ya Tanga Jamhuri Kihwelo wakati wa Mazoezi yao.

Kocha Mkuu wa Coastal Union, Jamhuri Kihwelo
‘Julio’ amewaambia wachezaji wake wanatakiwa kufanya kila linaliwezekana kuhakikishaw anashinda mechi yao inayofuata.
Coastal Union itakipiga dhidi ya Polisi Moro ikiwa ugenini kwenye Uwanja wa Jamhuri mjini Morogoro.
Julio amewaambia wachezaji wake mara tu baada ya kumaliza mazoezi kwamba ni lazima washinde na hawatakuwa na sababu ya kujitetea.
“Hatuna cha kusema kama sababu ya kupoteza, kikosi chetuni imara na ushirikiano tunaopata ni mkubwa. Hivyo tupambane na kuibuka na ushindi.

waliotembelea blog