Monday, September 15, 2014



Manchester United  wameshinda Mechi yao ya kwanza Msimu huu kwenye Ligi Kuu England wakati Kikosi chao kipya kikiisambaratisha QPR kwa Bao 4-0 ndani ya Old Trafford huku Angel De Maria aking’ara na Wachezaji wapya Marcos Rojo na Daley Blind wakicheza Mechi yao ya kwanza na kuleta uhai mkubwa.Manchester United v QPRJuan Mata akifanya yake..Manchester United v QPR
Bao 3 kabla ya Mapumziko, zilizofungwa na Di Maria, Ander Herrera na Wayne Rooney ziliwaua QPR na kuwamaliza kabisa pale Kipindi cha Pili Juan Mata alipofunga Bao la 4.Manchester United v QPRRadamel Falcao akikimbiza mpira mwishoni kipindi cha pili..Manchester United v QPRRadamel Falcao chupuchupu afunge! Kipa wa QPR aliutema mpira..
Manchester United v QPR
Straika mpya, Radamel Falcao, alikuwa Benchi na kuingizwa Dakika ya 67 na alionyesha matumaini na nusura afunge Bao kama si uhodari wa Kipa wa Robert Green. Bao la nne lilifungwa na Juan Mata katika dakika ya 58 kipindi cha pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Ángel Di María.
Ander Herrera akishangilia bao lake la pili kwa United.Angel Di Maria alifunga Bao la Kwanza kwa frikiki murua na ni yeye alietengeneza Bao la Pili kwa kukokota ngoma Mita 60 na kumpasia Rooney aliepiga Shuti lililookolewa na kumrudia Herrera na kufunga.Manchester United v QPRDakika ya 24 Di Maria anaipachikia bao la kwanza Manchester United..1-0 dhidi ya QPR. Ni Frii kiki ya Di Maria ya umbali wa  yadi  30 na kutinga moja kwa moja hadi langoni mwa QPR.Ander Herrera  alitupia la pili na kufanya 2-0 dhidi ya QPR katika dakika ya 36 kipindi cha kwanza baada ya kupata mpira kutoka kwa Wayne Rooney. Bao la tatu lilifungwa na Wayne Rooney katika dakika ya 44 kwa shuti kali lililomzidi kipa wa QPR Green na kuzama langoni moja kwa moja na ni kwa ushirikiano wa Ander Herrera aliyetoa pasi kwa Rooney.Manchester United v QPRFalcao alichukua nafasi ya Juani Mata kipindi cja pili dakika ya 67Manchester United v QPRRojo kwenye patashika na Matt Philips wa QPRManchester United v QPRFer wa QPR akichuana na Angel Di MariaRio Ferdinand kwenye wasiwasi kutoka kwa timu yake ya zamani UnitedRadamel Falcao kaanzia benchiManchester United v QPRRio Ferdinand akipewa zawadi yake mapema kabla ya mtanange..Louis van GaalVan Gaal kati..Radamel FalcaoTayari kwa kipute...
Daley Blind na Radomel Falcao wakiingia Old Trafford...yasemekana Falcao kuingia kipindi cha pili..dhidi ya QPR.Wachezaji wa Man United wakiwa tayari kwa kipute na QPR jioni hii kwenye uwanja wa Old Trafford. United wanatarajia kuchezesha wachezaji wao wapya katika mtanange huu.
Daley Blind na Radomel Falcao wa  Manchester United wakiwasili kwenye Uwanja wa Old Trafford, Tayari kwa mtanange huo.
Luke Shawna  Ander Herrera wakishuka kwenye basi kuingia Uwanjani Old Trafford.
Meneja wa Man United Louis van Gaal akiwsiliWachezaji wa QPR wakiwa kwenye Uwanja wa  Old Trafford
Mashabiki nao ndio kwanza wanaanza kuingia kuchukua nafasi zao Uwanjani Old Trafford.
VIKOSI:


Kikosi cha Simba sc kilichokwenda Mtwara jumamosi na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana (0-0) dhidi ya wenyeji Ndanda fc

Na Baraka Mpenja, Dar es salaam
WEKUNDU wa Msimbazi , Simba SC, wanaenda kuweka kambi tena Visiwani Zanzibar kwa ajili ya maandalizi ya mwisho ya ligi kuu soka  Tanzania bara inayotarajia kuanza kutimua vumbi septemba 20 mwaka huu.
Simba chini ya kocha Mzambia Patrick Phiri wataanza kampeni za kusaka ubingwa walioukosa kwa misimu miwili dhidi ya Wagosi wa Kaya, Coastal Union, septemba 21 mwaka huu uwanja wa Taifa , Dar es salaam.
Makamu wa Rais wa Simba, Geofrey Nyange ‘kaburu’ Perez amesema:  “Leo timu inaelekea Zanzibar kwa ajili ya mkakati wa mwisho wa kujiandaa na ligi kuu na jumamosi timu itarudi Dar es salaam kwaajili ya mchezo wa jumapili dhidi ya Coastal Union uwanja wa Taifa.”
Hii itakuwa mara ya pili Simba kujificha Zanzibar kwasabababu ilikuwa huko kabla ya kuja Dar es salaam kucheza mechi ya kirafiki dhidi ya Gor Mahia ya Kenya, septemba 6 mwaka huu uwanja wa Taifa.
Katika mechi hiyo ya kimataifa ya kirafiki, mabao mawili ya Paul Kiongera na moja la Ramadhani Singano ‘Messi’ yalitosha kuwapa Simba ushindi wa 3-0.
Baada ya mechi hiyo,  Simba waliendelea kubakia Dar es salaam badala ya kurudi Zanzibar kama ilivyokuwa imeelezwa awali na alikuwa inafanya mazoezi katika uwanja wa Boko Veterani.
Ijumaa ya wiki iliyopita, Simba ilicheza mechi ya pili ya kimataifa ya kirafiki dhidi ya URA ya Uganda na kulala bao 1-0.
Kesho yake (jumamosi) ya wiki iliyopita, Simba ilisafiri kwenda Mtwara ambapo ilicheza mechi ya kirafiki na Ndanda fc katika uwanja wa Nangwanda Sijaona na kutoka suluhu pacha ya bila kufungana.
Baada ya mechi hiyo, jana wachezaji walipewa mapumzikio, na leo jumatatu wanaanza mazoezi kabla ya kuelekea Zanzibar.
Simba wamekuwa wakiijenga timu upya chini ya kocha Phiri na usajili wao unawafanya wapinzani wawe na wasiwasi.
Wachezaji wa kigeni waliopo Simba wameonekana kuwa na ubora wa kutosha, hivyo kujenga imani kwa mashabiki wao.
Warundi, Amissi Tambwe, Pierre Kwizera, Mkenya, Paul Kiongera na Waganda Joseph Owino na Emmanuel Okwi wameonekana kuwa na msaada mkubwa kwa Simba.
Pia wapo wazawa waliosajiliwa kama, kipa Hussein Sharrif, Shaaban Kisiga, Elius Maguli,Joram Mgeveke, Tshabalala, na wengineo.

Wachezaji hawa wameonakana kuelewana na kucheza mpira mzuri kama walivyoonekana kwenye mechi dhidi ya Gor Mahia na URA.

Sunday, September 14, 2014


Na Father Kidevu Blog
Wanyange 30 wanao wanbia taji la Redd's Miss Tanzania 2014 leo wameingia kambini tayari kwa safari ya fainali za Miss Tanzania 2014 zitakazo fanyikia mapema mwezi Oktoba jiji Dar es Salaam.
Warembo hao waliowasdili kwa muda tofauti kuanzaia saa 12 alfajiri ya leo na kupokelewa na waandaaji wa Miss Tanzania katika hoteli ya JB Belmont iliyopo katikati ya jiji la maraha la Dar.
Warembo kutoka Kanda ya Ziwa walitia fora pale warembo hao walipowasili kambini hapo wakiwa ndani ya gari ya Mshindi wa Kanda ya Ziwa ambayo alizawadiwa hivi kjaribuni katika shindano lao.


Warembo wakiwasili kambini


Warembo wa Kanda ya Ziwa wakiteremka katika gari lao baada ya kuwasili na inaelezwa waliendesha kutoka jijini Mwanza.

Warembo wa Kanda ya Ziwa wakijiandikisha baada ya kuwasili kambini.

Warembo wakielekea chumba cha mkutano.


Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.


Warembo wakiwa katika chumba cha semina ambapo maelezo mbalimbali ya ka,mbi yao yalitolewa.

Wadhamini wakijitambulisha kwa warembo na wanahabari.

Mkurugenzi wa Kamati ya Miss Tanzania, Hasim Lundenga 'Anko' (kushoto) akiteta jambo na Katibu wake Bosco Majaliwa 'Mshua'.



Chakula cha mchana kwa warembo.


Na baraka Mbolembole, Dar es Salaam,
Salum Telela alifunga bao pekee kwa kuunganisha krosi ya mshambulizi Didier Kavumbangu na kuisaidia timu yake kupata ushindi wa bao 1-0 katika mchezo wa Ngao ya Jamii, mwaka uliopita.. Kelvin Yondan, Nadir Haroub, Saimon Msuva, ni wachezaji pekee ambao wanaweza kuanza moja kwa moja katika kikosi cha kwanza cha Mwalimu, Marcio Maximo. Mfungaji wa mwaka uliopita Telela na mlinzi wa kulia Juma Abdul ambao wote walianza katika mchezo wa ushindi mwa jana, mmoja wao atasubiri katika benchi ili kupisha utitiri wa viungo katikati ya uwanja.
Aishi Manula, Erasto Nyoni, David Mwantika, kaimu nahodha Aggrey Morris, Himid Mao Mkami, Salum Abubakary, Kipre Tchetche, Kipre Bolou wote hao walianza katika mchezo wa kichapo mwaka jana na wanataraji kuanza katika mchezo wa leo ambao utakuwa watatu mfululizo kwa kikosi chao cha Azam FC katika Ngao ya Jamii. Mabingwa hao wa ligi kuu Bara msimu uliopita, wana safu kabambe ya mashambulizi ambayo ilifunga mabao 12 katika michezo mitano ya Kagame Cup, Mwezi uliopita nchini Rwanda.
Wakati kocha wa Yanga, Maximo akitaraji kumuanzisha mshambulizi mmoja mbele, huku akitegemea safu ya kiungo kama muhimili wa timu, Joseph Omog yeye yupo tofauti , licha ya kumkosa nahodha wake John Bocco, kocha huyo raia wa Cameroon atakuwa na nafasi nzuri ya kujaribu safu yake ya ‘ washambulizi watatu wa kimataifa’. Tchetche, Mhaiti, Lieonel Saint na Mrundi, ‘ Kavu’ ambaye alifunga mabao 22 katika misimu miwili ya ligi kuu Bara akiwa na kikosi cha Yanga. Yanga watapata shinda lakini sehemu yao ya katikati ya uwan ja inatakiwa kuwa ngumu zaidi ya ilivyokuwa katika michezo minne iliyopita ya maandalizi ambayo wameshuhudia timu yao ikifunga mabao matano tu.
AZam ni lazima watafunga, wanaweza kufunga hata mabao mawili kwa sabu safu yao ya mashambulizi ina wafungaji wa uhakika. Kama Leonel ataachana na tabia yake ya kutotoa ushirikiano na kujiona staa zaidi ya wenzake itaendelea Azam itaanguka na wanaweza kupoteza mchezo. Safu ya ulinzi ya Yanga ndiyo ile inayotumika katika timu ya Taifa ya Tanzania, Taifa Stars, golikipa Deogratius Munish ana nafasi kubwa ya kuanza mchezo huo lakini nafasi hiyo inaweza kuangukia kwa ‘ mwalimu wa uwanjani’ Juma Kaseja,  nahodha Nadir, Kelvin a Oscar Joshua katika upande wa kushoto ni nafasi nne ambazo zinapangika kwa urahisi.
Maximo  kama ilivyo kwa Omog naye atakuwa akikuna kichwa, ni mlinzi gani sahihi wa kulia ambaye anatakiwa kumpanga katika mfumo wake na kufanya vizuri. Abdul au Telela? Ogog atakuwa akitafakari nafasi hasa ya kumpanga Nyoni mchezaji ambaye anaingia katika mifumo yote. Nani atamchezesha nafasi ya ulinzi wa kushoto? Ni Nyoni, Said Mourad au kinda Gadiel Michael ambaye alifanya vizuri katika michuano ya Kagame?. Makocha wote wanapasuka vichwa, hiyo ni kutokana na wachezaji wa timu pinzani jinsi wanavyocheza na u-fit wao walionao sasa.
Maximo amekuwa akitumia mfumo wa  4-5-1 ambao huwapanga viungo watano, Hasan Dilunga upande wa kulia,  Mbuyu kama kiungo wa kwanza wa ulinzi-namba 6,  Andrey Coutinho kama kiungo wa mashambulizi akitokea upande wa kushoto, Niyonzima kama kiungo ‘ mchezesha timu mkuu’ –namba 8, Msuva amekuwa akitumika kama mshambulizi wa pili. Kwa nini imekuwa hivyo? Mbuyu ni mkabaji hasa na mchezaji anayeanzisha pasi nzuri kwa viungo wa mbele. Dilunga ni mchezaji mwenye nguvu katika miguu na mwili wake , ni mwepesi hivyom ni rahisi kwake kucheza kama kiungo wa kulia, wakati mwingine upande wa kushoto, kama ataendelea kupiga pasi zinazofika bila shaka ni chaguo ambao Maximo hatajutia. Vipi kuhusu nafasi ya Mrisho Ngassa? Maximo anaweza kumpanga Nassa kama mshambulizi wa pili nyuma ya GEilson Santos ‘ Jaja’ na ikiwa hivyo itamaanisha Dilunga arudi katika benchi na Msuva acheze kama kiungo wa kulia. Itafaa zaidi , Ngassa akicheza, kwa sababu viungo wa Azam ni ‘ wagumu na hawachoki’ mapema. Himid, Salum, na Bolou itakuwa safu nzuri ya kiungo kwa upande wa kikosi cha Omog, lakini anaweza kumtumia Nyoni katika eneo hilo ikiwa atachezesha timu yake katika mfumo wa 4-4-2.
Azam wana safu nzuri ya ulinzi ambayo kwa kiasi kikubwa ilichangia mafanikio ya timu hiyo katika ligi kuu Bara msimu uliopita waliporuhusu mabao 15 katika michezo 26. Morris, Mwantika ni chaguo zuri la kwanza katika safu ya ulinzi wa kati. Jaja atafunga katika mchezo wa leo ikiwa viungo wake watamiliki mchezo. Shomari Kapombe atakutana na kiungo mwenye maarifa, Couinho na upande wa kulia wa Azam umekuwa na mchezo usioridhisha sana kwani upande huo upitika kiurahisi, ili kuziba nafasi ya Yanga kutumia upande wao wa kushoto Omog ni lazima amuanzishe nje mshambulizi wake mmoja ili kumpatia nafasi Nyoni katika eneo la kiungo kuwasaidia, Himid, Salum na Bolou.
Said Mourad atakuwa na nafasi finyu ya kuanza katika safu ya ulinzi wa kati, lakini ili kuleta usawa na nguvu zaidi katika ngome, Omog anaweza kupata faida kubwa akimpanga mchezaji huyo katika eneo la ulinzi wa kushoto.  Ni mechi ngumu lakini inaweza kuwa ya mabao mengi, 3-2, 2-1 au 3-1 ni matokeo ambayo yanaweza kutokea. Ipi timu bora zaidi katika mchezo wa leo? Yanga? Ubora wao uko wapi?
Azam ikiimaliza sehemu ya kiungo ya Yanga watashinda, ila watafungwa wakiruhusu vipaji vya Yanga kutawala katikati ya uwanja. Kavumbagu atafunga, Jaja atafunga ila ningempanga Telela katika eneo la kiungo la Yanga ili kuwamudu Azam FC ‘ mwanzo-mwisho’. Ningempanga Nyoni katika kiungo na Mourad katika safu ya beki tatu ili kupunguza krosi za Yanga. Yanga ina nafasi ya kushinda kwa mara nyingine….AZam FC ililazwa na Simba SC kwa mabao 3-2, 2012, wakapoteza mbele ya Yanga kwa bao 1-0, 2013, 2014 itakuwaje, Ngao ya Jamii si bahati yao?



Bondia Elick Mwenda kushoto wa Malawi akikwepa ngumi  wakati wa mpambano wake na bondia Allybaba Ramadhani   uliofanyika mwishoni mwa wiki iliyopita Allybaba alishinda kwa pointi mpambano huo 
Bondia Raymond Mbwago kushoto akipambana na Iddi Pialali wakati wa mpambano wao uliofanyika Moshi katika ukumbi wa YMCA Hall Pialali alishinda kwa K,O ya raundi ya Nne
Allybaba Ramadhani
Bondia Raymond Mbwago kushoto akipambana na Iddi Pialali wakati wa mpambano wao uliofanyika Moshi katika ukumbi wa YMCA Hall Pialali alishinda kwa K,O ya raundi ya Nne
Bondia Shomari Milundi kushoto akipambana na Saimoni Zabron wakati wa mpambano wao uliofanyika Moshi mpambano huo walitoka Droo ya kufungana 


Bondia Said Yazidu kushoto akipigwa ngumi na Djamal Dahou wa Algelia Dahou alishinda kwa K,O ya raundi ya kwanza ya mpambano huo



Wachezaji wa Simba na Ndanda FC wakiingia Uwanjani wakati wa mchezo wa maalum wa kusherehekea Ndanda Day uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara na kudhaminiwa na Shirika la Taifa la Hifadhi ya Jamii (NSSF), kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme. Timu hizo zilitoka suluhu. (Na Mpiga Picha Wetu)

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akisalimia na timu ya Ndanda FC kabla ya mchezo wao na timu ya Simba uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Mkuu wa Mkoa wa Mtwara Kanali mstaafu Joseph Simbakalia akikagua timu ya Simba wakati wa mchezo wa kirafiki na timu ya Ndanda FC uliofanyika leo kwenye Uwanja wa Nangwanda Sijaona mjini Mtwara.

Kikosi kamili cha timu ya Simba kilichopambana na Ndanda FC.
Kikosi cha Ndanda FC kikiwa klatika picha ya pamoja kabla ya pambano lao na Simba.

Wachezazaji wa Simba na Ndanda wakichuana katika uwanja wa Nangwanda Sijaona.

Mashabiki wa soka wakifuatilia pambano la Simba na Danda FC.NSSF kupitia mpango wake wa Wakulima Scheme yadhamini mechi ya kujipima nguvu kati ya Simba ya Dar es Salaam na Ndanda FC ya Mtwara kwenye uwanja wa CCM wa Nangwanda Sijaona na kuhudhuriwa na maelfu ya washabiki wa soka mkoani Mtwara.

Mchezo huo pia ulikuwa ni sehemu ya sherehe za Ndanda Day ulihudhuriwa na viongozi mbali mbali wakiwemo wa Serikali uliisha kwa matokeo ya timu hizo kutoka suluhu.
NSSF kupitia mpango maalum wa wakulima schemes wenye lengo la kuandikisha na kuhudumia wakulima kwenye mfuko ya hifadhi ya jamii nchini ili kuwawezesha wakulima wote nchini wawe kwenye mfuko huo kupata pensheni ya uzeeni pindi watakapo fikisha umri wa miaka 55 na kuendelea wakulima hao wataweza kulipwa penshion zao hadi watakapo fariki.

waliotembelea blog