Manchester United wameshinda Mechi yao
ya kwanza Msimu huu kwenye Ligi Kuu England wakati Kikosi chao kipya
kikiisambaratisha QPR kwa Bao 4-0 ndani ya Old Trafford huku Angel De
Maria aking’ara na Wachezaji wapya Marcos Rojo na Daley Blind wakicheza
Mechi yao ya kwanza na kuleta uhai mkubwa.
Juan Mata akifanya yake..
Bao 3 kabla ya Mapumziko, zilizofungwa
na Di Maria, Ander Herrera na Wayne Rooney ziliwaua QPR na kuwamaliza
kabisa pale Kipindi cha Pili Juan Mata alipofunga Bao la 4.
Radamel Falcao akikimbiza mpira mwishoni kipindi cha pili..

Radamel Falcao chupuchupu afunge! Kipa wa QPR aliutema mpira..

Straika
mpya, Radamel Falcao, alikuwa Benchi na kuingizwa Dakika ya 67 na
alionyesha matumaini na nusura afunge Bao kama si uhodari wa Kipa wa
Robert Green. Bao la nne lilifungwa na Juan Mata katika dakika ya 58
kipindi cha pili baada ya kupata pasi kutoka kwa Ángel Di María.
Ander Herrera akishangilia bao lake la pili kwa United.

Angel
Di Maria alifunga Bao la Kwanza kwa frikiki murua na ni yeye
alietengeneza Bao la Pili kwa kukokota ngoma Mita 60 na kumpasia Rooney
aliepiga Shuti lililookolewa na kumrudia Herrera na kufunga.
Dakika
ya 24 Di Maria anaipachikia bao la kwanza Manchester United..1-0 dhidi
ya QPR. Ni Frii kiki ya Di Maria ya umbali wa yadi 30 na kutinga moja
kwa moja hadi langoni mwa QPR.
Ander
Herrera alitupia la pili na kufanya 2-0 dhidi ya QPR katika dakika ya
36 kipindi cha kwanza baada ya kupata mpira kutoka kwa Wayne Rooney. Bao
la tatu lilifungwa na Wayne Rooney katika dakika ya 44 kwa shuti kali
lililomzidi kipa wa QPR Green na kuzama langoni moja kwa moja na ni kwa
ushirikiano wa Ander Herrera aliyetoa pasi kwa Rooney.
Falcao alichukua nafasi ya Juani Mata kipindi cja pili dakika ya 67

Rojo kwenye patashika na Matt Philips wa QPR

Fer wa QPR akichuana na Angel Di Maria

Rio Ferdinand kwenye wasiwasi kutoka kwa timu yake ya zamani United

Radamel Falcao kaanzia benchi

Rio Ferdinand akipewa zawadi yake mapema kabla ya mtanange..

Van Gaal kati..

Tayari kwa kipute...

Daley Blind na Radomel Falcao wakiingia Old Trafford...yasemekana Falcao kuingia kipindi cha pili..dhidi ya QPR.

Wachezaji
wa Man United wakiwa tayari kwa kipute na QPR jioni hii kwenye uwanja
wa Old Trafford. United wanatarajia kuchezesha wachezaji wao wapya
katika mtanange huu.

Daley Blind na Radomel Falcao wa Manchester United wakiwasili kwenye Uwanja wa Old Trafford, Tayari kwa mtanange huo.

Luke Shawna Ander Herrera wakishuka kwenye basi kuingia Uwanjani Old Trafford.

Meneja wa Man United Louis van Gaal akiwsili

Wachezaji wa QPR wakiwa kwenye Uwanja wa Old Trafford

Mashabiki nao ndio kwanza wanaanza kuingia kuchukua nafasi zao Uwanjani Old Trafford.
VIKOSI:
0 maoni:
Post a Comment