Waziri
wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akizungumza katika
uzinduzi wa mashindano ya magari jijini Dar es Salaam leo.
Waziri
wa Habari, sanaa, Utamaduni na Michezo, Nape Nnaye akiwa amenyanyua
bendera ya Taifa juu kuashiria uzinduzi wa Mashindano ya Mbio za Magari
ya 2016 jijini Dar es Salaam leo .Kulia kwa Nape ni Katibu wa Balaza la
Michezo Tanzania(BMT), Mohamed Kiganja.
Na Zainab Nyamka, Globu ya Jamii.
WAZIRI
wa Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo Nape Nnauye amezindua mashindano
ya magari ya hapa nchini ya 2016 na kuwataka watazania kujitokeza kwa
wingi kushiriki kwenye mchezo huo ambapo amewataka kuacha kujiweka nyuma
na kuitwa kichwa cha mwendawazimu kila siku. Hayo ameyasema wakati
akizindua mashindano hayo ya magari yanayotarajiwa kuanza kutimua vumbi
kesho wilaya ya Bagamoyo ikihusisha magari 25.
Nape
amesema kuwa wanachotaka kuona ni kuwa Tanzania inafanya vizuri kwenye
mashindano hayo na zaidi wanataka kuona wanazidi kuwavutia wageni kwenye
mashindano hayo ili kuongeza utalii wandani na kuongeza pato kwa
serikali pale watakapoamua kutembelea mbuga za wanyama.
“Nawataka
watanzania kuzidi kufanya vizuri kwenye mashindano na zaidi wawavutie
wageni kwani watakapokuja kwa wingi wataongeza pato la taifa pale
watakapotembelea hifadhi za taifa,”amesema.
Naye
Rais wa chama cha Magari Tanzania (AAT), Bwana Nizar Jivani amesema
kuwa mwaka jana waliweza kuondoa kauli ya kichwa cha mwendawazimu na
walilitekeleza kama walivyomuahidi Raisi mstaafu wa awamu ya Pili Ally
Hassan Mwinyi na mwaka huu watazidi kufanya vizuri na watabakisha
ushindi nyumbani. Mashindano hayo yamezingatia viwango vyote ambapo
jumla ya magari 25 yatashiriki ambapo kati ya magari hayo, Magari 4
yatatoka Uganda, 2- Zambia, Kenya (1), Falme za Kiarabu (1). Na kwa
magari ya kutoka Tanzannia ni 17.
Magari
hayo 17 ya Tanzania ambapo Dar es Salaam magari 10, Arusha (3),
Moshi (3), na Tanga (1). Aidha, magari hayo yanatarajiwa kushindana
katika umbali wa kilometa 246 kwa siku ya kwanza na yatakuwa kwa muda wa
siku mbili.
0 maoni:
Post a Comment