
2:10 PM

Unknown
Baada
ya tetesi za muda mrefu, hatimaye Mecky Maxime ametua Kagera Sugar.
Maxime ambaye alikuwa akiinoa Mtibwa Sugar, sasa amesaini mkataba wa
kuinoa Kagera Sugar. Meneja wa Kagera Sugar, Mohammed Hussein amesema
Maxime ndiye kocha mkuu akichukua nafasi ya Adolf Rishard.
Awali, kulikuwa na taarifa za kuondoka
kwa Maxime kwenda Kagera, lakini uongozi wa Mtibwa Sugar ulilikataa
hilo. Kuna tarifa Mtibwa Sugar inatarajia kumrejesha Salum Mayanga
ambaye sasa anainoa Prisons.
0 maoni:
Post a Comment