Kikosi cha wachezaji 22 wa timu ya Taifa ya vijana
wenye umri chini ya miaka 15 (U-15) kilichopo kambini mjini Morogoro,
kimeendelea na mazoezi kujiandaa na mchezo wa kirafiki dhidi ya kombaini ya
Morogoro mwishoni mwa wiki.
U-15 inayonolewa na kocha Bakari Shime, imeingia
kambini mkoani Morogoro ikiwa ni sehemu ya vijana hao kukutana kila mwisho wa
mwezi na kucheza michezo ya kirafiki na kombaini za mikoa kwa lengo la mwalimu
kutazama uwezo wa vijana wake na kuongeza vijana wengi atakaowabaini katika
michezo hiyo.
Ikiwa mkoani Morogogoro, timu hiyo ya vjiana itacheza
michezo miwili na kombaini ya mkoa huo ya vijana wneye umri chini ya miaka 15
siku za jumamosi na jumapili kabla ya kuvunjwa kwa kambi yao sikuya jumatatu.
TFF iliandaa utaratibu wa timu hiyo ya vijana kucheza
michezo ya kirafiki kila mwisho wa mwezi ndani ya nchi, kabla ya mwezi Disemba
kwenda katika nchi za Malawi, Zambia, Zimbabwe, Botswana na Afrika Kusini
kucheza michezo ya kirafiki ya kimataifa.
Lengo la kambi hiyo ni kuandaa kikosi bora cha vijana kitachoshiriki kuwania kufuzu kwa fainali za Mataifa Afrika kwa vijana wneye umri chini ya miaka 17 (U17) zitakazofanyika nchini Madagascar.
0 maoni:
Post a Comment