Wakati
Simba ikiwa kambini Zanzibar, watani wao Yanga nao wameamua kwenda
visiwani humo kwa kambi ya mwisho kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu Bara.
Hilo
limezua mjadala kwa nini timu hizo kongwe zenye upinzani mkubwa
zimeamua kufuatana Zanzibar na imekuwa ikionekana kama huko ni maeneo ya
Simba.
Mkurugenzi
wa Habari na Mawasiliano wa Yanga, Jerry Muro amezungumza na SALEHJEMBE
na kuelezea sababu muhimu za Yanga kwenda Zanzibar.
"Tulichoangalia
sisi ni utulivu wa kambi na uhakika wa sehemu za mazoezi. Lakini
tumeangalia zaidi suala la kusogeza timu karibu na Wanayanga.
"Zanzibar ni sehemu yenye wanachama na mashabiki wengi wa Yanga, kihistoria Yanga ina mengi yanasomeka kutoka Zanzibar.
"Hata
ukiangalia katika kikosi chetu tuna zaidi ya wachezaji wanne kutoka
Zanzibar. Hivyo Zanzibar ni nyumbani kwa Yanga, kuweka kambi huko si
tatizo hata kidogo," alisema Muro.
Yanga itafungua Ligi Kuu Bara Septemba 13 ambayo ni Jumapili kwa kuwa mwenyeji wa Coastal Union.
0 maoni:
Post a Comment