Na Andrew Chale, modewjiblog
(Dar
es Salaam)-Ile shoo kubwa yamaonyesho ya mavazi ubunifu ya Tanzania
katika kuibua vipaji vya wanamitindo chipukizi na models lililoandaliwa
na kampuni ya Crown River Fame likijulikana kama Sanaa Fashion Show,
linatarajia kufanyika Ijumaa hii ya Agosti 28, ndani ya ukumbi wa Mbezi
Garden Hotel, ambapo pia kutakuwa na shoo kabambe kutoka kwa msanii wa
THT, Msami.
Akizungumza
na mtandao huu Meneja Mradi wa Crown River Fame, Mr. Rahul anasema
tayari taratibu zote zimeshakamilika na models pamoja na wabunifu wa
mitindo wameshakamilisha kazi zao na kinachosubiriwa na shoo hiyo
kabambe na ya aina yake kwa upande wa fashion show.
"Tunataraji
kuwa na Models zaidi ya 20, watakaonyesha mavazi ya ubunifu katika shoo
hii ya Sanaa Fashion, na pia tunatarajia kuwa na wabunifu zaidi ya 15
wakiwemo wakongwe na wanaochipukia kwa maana 'Upcoming Desgners'.
Ili
kuleta mageuzi katika tasnia hii ya urembo na ubunifu, jukwaa hili la
Sanaa Fashion Show, lina lengo kuu la kuinua models wanaochipukia
'Upcoming models' na pia kuendeleza tamaduni zetu kwa maana hiyo tumeipa
jina la Sanaa.".
Aidha,
anabainisha kuwa, baadhi ya wabunifu wa mavazi watakaoshiriki kwenye
kuvisha Models, katika show hiyo ni pamoja na Mama wa Mitindo nchini,
Asia Idarous, Mohammed Abdul, Joyce na wengine wengi.
Kwa upande wa kiingilio ni V.I.M ni Sh 20,000 huku V.I.P yenyewe ikiwa ni sh 40,000.
Kwa
upande wa wadhamini ni pamoja na MODEWJIBLOG, 8020Fashions, Shear
Illusions, Mbezi Beach Garden, BR Production, MC na wengine wengi.
Husna
Tandika akimfanyia make up, Model, Abdul-Amad katika duka la Shear
Illusions Millenium Tower, jijini Dar es Salaam. Ikiwa tayari kwa
maandalizi ya shoo hiyo ya kesho!
Jonetha-Peter. akipakwa make up na mfanyakzi wa Shear Illusions, Agnes Rafael.
0 maoni:
Post a Comment