Tukiwa tunaelekea kufungwa kwa dirisha la usajili wa Ligi Kuu Uingereza,
nimeona nikukumbushe wachezaji watano waliowahi kusajiliwa kwa fedha
nyingi saa chache kabla ya dirisha la usajili halijafungwa.
Mesut Ozil – 2013
Ikiwa saa kadhaa zilikuwa zimesalia kabla ya dirisha la usajili kufungwa Uingereza mwaka 2013, klabu ya Arsenal iliridhia kutoa pound milioni 42.4 kumsajili kiungo wa Kijerumani aliyekuwa katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Mesut Ozil na kuvunja rekodi ya usajili ya klabu hiyo.
Fernando Torres na David Luiz 2011
Baada ya misimu mitatu ya mafanikio katika klabu ya Liverpool Fernando Torres mwaka 2011 alijiunga na klabu ya Chelsea ya London kwa pound milioni 50 kwa wakati huo ilikuwa ni rekodi kubwa ya usajili kwa vilabu vya Ligi Kuu Uingereza. Lakini Torres alishindwa kuonyesha makali yake Chelsea kwani alicheza mechi 110 na kufunga goli 20. Siku hiyo hiyo aliyosajiliwa Torres ndio siku aliosajiliwa beki wa Kibrazil David Luiz akitokea Benfica ya Ureno.
Dimitar Berbatov 2008
Mwaka 2008 klabu ya Manchester United ilikamilisha uhamisho wa pound milioni 30.75 kwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Bulgaria Dimitar Berbatov kutokea klabu ya Tottenham Hotspur, hata hivyo uhamisho huo ambao ulifanywa na Man United ilikuwa ni sawa na wao walivyozidiwa kete na Chelsea kwa Pedro kwani Berbatov alikuwa ajiunge na Man City kabla ya Ferguson kumdaka Uwanja wa ndege.
Andy Carroll na Luis Suarez – 2011
Mwaka 2011 kocha wa zamani wa klabu ya Liverpool Kenny Dalglish aliwasajili kwa pamoja Andy Carrol kutokea klabu ya Newcastle United na Luis Suarez akitokea klabu ya Ajax ya Uholanzi.
Andrei Arshavin – 2009
Andrei Arshavin mshambulaiji wa kimataifa wa Urusi aliyetua katika klabu ya Arsenal ya Uingereza kwa pound milioni 15 Zenit, licha ya Arshavin kushindwa kutamba katika klabu ya Arsenal na kitu pekee kikubwa alichowahi kufanya ni kuifunga Liverpool magoli manne.
Hiyo ndio kumbukumbu ambayo
nimekukumbusha mtu wangu kwani hadi sasa tunategemea kuona lolote
likitokea katika masaa machache yaliosalia ili kufungwa kwa dirisha la
usajili la Ligi Kuu Uingereza.
0 maoni:
Post a Comment