Mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa anayeichezea klabu ya Arsenal ya Uingereza Oliver Giroud ambaye wengi wamekuwa wakimlaumu kocha wa Arsenal Arsene Wenger kuwa hawezi kutwaa ubingwa akiwa na mshambuliaji huyo pekee, wengi walikuwa wakishinikiza Wenger amsajili Karim Benzema.
August 31 Oliver Giroud amekutana na maswali ya waandishi wa habari kuhusu klabu yake ya Arsenal kuhusishwa kutaka kusajili mshambuliaji mpya. Oliver Giroud ana majibu haya kuhusiana na Arsenal kutaka kumsajili mfaransa mwenzake Karim Benzema na yeye mtazamo wake kuhusu usajili huo.
“Ni kweli
kila mwaka huwa kuna tetesi za kusajiliwa mshambuliaji mpya, kuna msimu
ambao tulimsajili Sanchez, Welbeck na wengine lakini tulikuwa
tukizungumza kuhusiana na Suarez, ni kawaida kwa klabu kuna mengi ya
kutarajiwa, najua mashabiki wanataka tusajili kwa fedha
nyingi”>>> Giroud
“Hilo sio
swali ninalopaswa kujibu mimi, kocha anajua vizuri nini anafanya, wakati
mwingine hutakiwi usajili tu ili mradi na wakati mwingine kuna kuwa
hakuna mchezaji unaye muhitaji, tukiachana na hayo itakuwa vizuri kama
Karimu angesajiliwa”>>> Giroud
Klabu ya Arsenal ya Uingereza ilikuwa ikihusishwa kumsajili mshambuliaji wa kimataifa wa Ufaransa ambaye anakipiga katika klabu ya Real Madrid ya Hispania Karim Benzema, ambapo Arsenal
walikuwa wapo tayari kutoa pound milioni 50 ili kumpata staa huyo kabla
ya siku kadhaa nyuma, staa huyo kuthibitisha kuwa hayupo tayari
kuondoka Real Madrid.
0 maoni:
Post a Comment