Sunday, July 12, 2015


Meneja wa Arsenal Arsene Wenger amedai mipango yao ya kununua Wachezaji wapya imesimama kwa vile anawapima Wachezaji wake waliokuwa majeruhi kwa muda mrefu Msimu uliopita.Wenger amesema nia yake ni kuwa na Kikosi kamili kilicho na Wachezaji wote fiti na kisha kupima na kuamua wapi waongeze nguvu.
Hadi sasa, kwa ajili ya Msimu mpya, Wenger amenunua Mchezaji mmoja tu ambae ni Kipa Petr Cech kutoka Chelsea kwa Dau la Milioni 11 huku wakihusishwa na kuwanasa kina Gonzalo Higuain, Arturo Vidal na Morgan Schneiderlin
Lakini Wenger amesisitiza kitu muhimu kwake ni kuwa fiti kwa Theo Walcott, Jack Wilshere na Mikel Arteta ambao wote walikuwa majeruhi kwa vipindi virefu Msimu uliopita.
Wenger amenena: "Njia bora ya kuimarisha Timu ni kuwafanya Wachezaji ambao hawakucheza Msimu uliopita wacheze na waendelee kuwa fiti."
Hata hivyo, hali hii inawashangaza wadau wa Arsenal hasa wakikumbuka Msimu uliopita, baada ya kuumia Viungo Arteta, Wilshere na Aaron Ramsey, Wenger alilazimika kumrudisha Emirates Francis Coquelin aliekuwa kwa Mkopo Charlton Athletic na kwa bahati Mchezaji huyo alicheza vyema sana.
Hivi sasa Arsenal wameshaanza Mazoezi kwa ajili ya Msimu mpya ambao wao, kama Mabingwa wa FA CUP, watacheza Mechi ya fungua pazia na Mabingwa wa England Chelsea hapo Agosti 2 huko Wembley, Jijini London kugombea Ngao ya Jamii na kuanza Ligi Kuu England hapo Agosti 9 kwa kucheza na West Ham.
Lakini kabla ya hapo, Arsenal watazuru huko Asia kucheza Barclays Asia Cup na kisha kurejea London na kucheza Kombe lao, EMIRATES CUP, Uwanjani kwao Emirates.

MECHI ZA ARSENAL KABLA MSIMU KUANZA:
BARCLAYS ASIA CUP

15 July Singapore XI (Singapore National Stadium)
18 July Everton or Stoke City (Singapore National Stadium)

EMIRATES CUP
25 July Lyon (Emirates)
26 July Wolfsburg (Emirates)

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog