Sunday, July 12, 2015


Manchester United wamekamilisha usajili wa mchezaji wa Torino Matteo Darmian

Darmian akipata picha na Jezi pamoja na Meneja Louis van Gaal (kulia)

Darmian amesajiliwa na kusaini mkataba wa kumweka  Old Trafford kwa miaka 4

Van Gaal akipeana mkono na Jembe lake jipya na akimtakia safari njema ya kuanza kashkashi za Ligi kuu England msimu mpya 2015/2016

Darmian ni mchezaji wa Kitaifa kutoka Italy na aliiwezesha Nchi yake kutwaa makombe 13

Darmian akitua mjini  Manchester Uwanja wa ndege kwa Ndege binafsi ijumaa Tayari kwa  kukamilisha upimwaji wa Afya yake.
WWW.BUKOBASPORTS.COMManchester United imetangaza rasmi kumpata Beki wa Kulia wa Torino Matteo Darmian na kumpa Mkataba wa Miaka Minne. Darmian, mwenye Miaka 25, ameichezea Torino Mechi 146 tangu mwaka 2011 na kufunga Bao 5 za Ligi.
Pia, Beki huyo ambae anaweza kucheza nafasi zote za nyuma, ameichezea Italy mara 13 na alikuwepo huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia na kucheza mechi zote 3 za Kundi lao.
Vile vile, aliiwakilisha Italy kwenye Timu za Vijana za U-17 hadi U-21.

Akiongea na Tovuti ya Man United, Darmian alisema: "Ni ndoto iliyotimia kujiunga na Manchester United. Nilifurahia muda wangu na Torino napenda kuishukuru Klabu na Mashabiki wake. Nina hakika wanaelewa ilipotokea nafasi hii ya kujiunga na Klabu kubwa kabisa Duniani ni kitu lazima nikifanye. Kufanya kazi na Meneja Louis van Gaal mwenye mafanikio makubwa kwenye Soka ni kitu cha kuvutia sana."
Darmian, mzaliwa wa Legnano, Milan, amenunuliwa kwa Ada inayoaminika kuwa Pauni Milioni 13.
 
Akiongelea kuhusu Darmian, Van Gaal alisema: "Matteo ni Beki wa Kulia ambae huweza kucheza Kushoto. Ni mwenye nguvu na anaweza kushambulia na hivyo anaweza kasi ya Ligi Kuu England."
Darmian alianzia Soka lake huko AC Milan tangu 2001 hadi 2010 alipohamia Palermo. 
Beki huyu anakuwa Mchezaji wa Pili baada ya Memphis Depay kusainiwa na Man United hivi sasa huku Bastian Schweinsteiger akingojea kumaliza upimwaji Afya na kuafiki Maslahi yake binafsi.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog