Kikosi cha timu ya Taifa ya
Tanzania, (Taifa Stars) kinachodhaminiwa na bia ya Kilimanjaro
kimeendelea kujifua katika uwanja wa Benki ya Biashara ya Ethiopia eneo
la CMC asubuhi na jioni katika uwanja wa Taifa wa Addis Ababa.
Stars ambayo imeweka kambi jijini
Addis Ababa imekua ikijifua mara mbili kwa siku, kuhakikisha wachezaji
wanakua vizuri kuelekea katika mchezo dhidi ya timu ya Taifa Misri
mwishoni mwa wiki hii jijini Alexandria.
Hali ya kambi kiujumla ni nzuri,
wachezaji wote ni wazima, wakiwa wenye ari, na morali ya hali ya juu
katika maandalizi ya mchezo huo wa kuwania kufuzu kwa fainali za AFCON
mwaka 2017.
Kocha mkuu wa Taifa Stars
mholanzi, Mart Nooij amekuwa akiwafundisha vijana wake mbinu mbali mbali
kuelekea kwenye mechi dhidi ya Misri, kuanzia sehemu ya ulinzi, kiungo
na ushambuliaji kuhakikisha wanakua fit katika mchezo unaowakabili.
Ikiwa ni siku ya nne tangu Taifa
Stars kuanza mazoezi yake jijini Addis Ababa, kocha Nooij amesema
anashukuru vijana wake wanamuelewa vizuri anachowaelekeza, sasa timu
inacheza mpira wa kasi na pasi za haraka haraka, vijana wamechangamka na
morali ni ya hali ya juu kambini kuelekea kwenye mchezo unaowakabili.
Hali ya nidhamu kambini ni ya hali
ya juu, wachezaji waanatambua umuhimu wa mchezo huo, na kikubwa
wameahidi kupambana kusaka matokeo mazuri katika mchezo dhidi ya Misri.
“Katika mpira hakuna
kinachoshindikana, sie tumejiandaa vizuri, naamini tutakapofika Misri
tutafanya vizuri na kuwapa furaha watanzania, kikubwa watuombee kwa
mwenyezi mungu, tuwe wazima mpaka siku ya mchezo, naamini tutafanya
vizuri” alisema Nadri.
Stars inatarajiwa kuelekea jijini
Cairo siku ya ijumaa, kisha kuunganisha katika jiji la Alexandria tayari
kwa mchezo dhidi ya Misri utakaochezwa katika uwanja wa Boeg El Arab
siku ya jumapili Juni 14, 2015.
0 maoni:
Post a Comment