TIMU ya soka ya Taifa ya Wanawake, Twiga Stars, jana ilijiweka kwenye nafasi nzuri ya kufuzu kucheza fainali za Afrika baada ya kuichapa Zambia mabao 4-2 katika mechi ya awali iliyochezwa mjini Lusaka.
Kutokana na ushindi huo, Twiga Stars sasa inahitaji sare ya aina yoyote timu hizo zitakaporudiana wiki mbili zijazo kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.
Habari kutoka Zambia zimeeleza kuwa, katika mechi hiyo, Twiga Stars ilicheza soka ya kiwango cha juu na kuwazidi wapinzani wao katika kila idara.Kocha Mkuu wa timu hiyo, Rogasiun Kaijage, alisema kwa njia ya simu kutoka Lusaka kuwa, ushindi huo ulitokana na vijana wake kucheza kwa kufuata maelekezo yake.
Kaijage alisema ushindi huo hautawafanya wabweteke, badala yake watacheza mechi ya marudiano kwa lengo la kuibuka na ushindi mwingine mkubwa zaidi
0 maoni:
Post a Comment