Tuesday, August 19, 2014


Latest transfer insights of “Big 5” football markets revealed in new report from FIFA TMS
MFUMO wa usajili wa elekroniki wa Shirikisho la soka duniani FIFA,  ‘FIFA TMS’ leo ametoa ripoti mpya ukionesha hali halisi ya soka la usajili la kimataifa likizihusisha klabu kutoka nchi za England, Ufaransa, Ujerumani, Italia na Hispania katika majira haya ya kiangazi ya usajili .

Dirisha la usajili litafungwa septemba 1 mwaka huu. Na kwa mataifa haya matano yaliyopo katika soka la usajili kwa kiasa kikubwa, FIFA TMS imetoa ripoti baada ya kupata usajili kwa kiasi kikubwa mpaka sasa.

Ripoti mpya ya sasa inalinganisha usajili wa majira ya kiangazi mwaka huu na miaka mitatu iliyopita katika hatua zilezile. Taarifa kwa kifupi ni kama hapa chini.
·        Ada ya uhamisho ya jumla iliyotumiwa na mataifa matano makubwa majira haya ya kiangazi (mpaka Agosti 12, 2014) ni Dola za kimarekani Bilioni 1.36, ikionekana kukaribiana na mwaka jana (Dola za kimarekani bilioni 1.35).
·        Wastani wa ada ya uhamisho kwa kila mchezaji wa mataifa haya matano inaendelea kukua (Dola za kimarekani milioni 12.1 mwaka 2014 kutoka dola za kimarekani milioni 10.1 mwaka 2013).
·        Klabu za England na Hispania zinaongoza katika soko la usajili, zikichukua asilimia 74 ya matumizi ya jumla ya usajili uliorekodiwa kwa mataifa matano majira haya ya kiangazi.
·        Klabu za Hispania zimezidisha matumizi kwa zaidi ya mara 3.5 kulinganisha na kipindi cha mwaka jana (Dola za kimarekani 491 kutoka dola za kimarekani 139 mwaka 2013).

·        Matumizi ya usajili kwa Ufaransa na Italia yamekuwa yakishuka mwaka kwa mwaka ambapo yameshuka kwa wastani wa 64% kwa mataifa yote mawili.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog