Tuesday, August 19, 2014

 

BEKI wa Kimataifa wa Argentina anaechezea Klabu ya Sporting Lisbon ya Ureno, Marcos Rojo, amethibitisha kuhamia Manchester United.
Akiongea na Redio ya Nchini kwao Argentina, Kituo cha Radio Continental, Marcos Rojo, mwenye Miaka 24, amesema ameshakamilisha Uhamisho wa ‘Ndoto yake’ kwenda Man United.

Jana iliripotiwa kuwa Man United ilikubali kulipa Ada ya Uhamisho ya Euro Milioni 20
kwa ajili ya Rojo na pia kumtoa Winga wao Nani kwenda kwa Mkopo wa Msimu mmoja huko Sporting Lisbon.
Nani alihamia Man United kutoka Sporting Lisbon Mwaka 2007.
Rojo amekaririwa akisema: “Ni kama ndoto kuwa Mchezaji wa Manchester United! Kuhama Sporting haikuwa rahisi!”

Wiki iliyopita mzozo mkubwa ulizuka kuhusu mgao wa Fedha kwa Wamiliki wa Mchezaji huyo mara baada ya Man United kutoa Ofa yao.
Rojo alihamia Sportung Lisbon Mwaka 2012 akitokea Spartak Moscow na Kampuni ya Doyen Sport ililipa Asilimia 75 na Sporting Lisbon kulipa Asilimia 25 ya Ada ya Uhamisho wake.

Nae Rojo aligoma kufanya Mazoezi, na kuadhibiwa na Sporting Lisbon, alipotaka kuruhusiwa kuhamia Man United.

Rojo alicheza Mechi zote za Argentina huko Brazil kwenye Fainali za Kombe la Dunia ambapo Argentina ilifungwa kwenye Fainali Bao 1-0 na Germany na Meneja wa Man United, Louis van Gaal, anamwona Beki huyo ni kiraka kwenye Mfumo wake wa 3-5-2 kutokana na uwezo wake wa kucheza Sentahafu au Fulbeki wa Kushoto.
Beki huyo yumo kwenye Timu ya FIFA ya Fainali za Kombe la Dunia za Brazil 2014.

Kabla kuhamia Spartak Moscow na kisha Sporting Lisbon, Rojo aliichezea Estudiantes ya Argentina na kutwaa Copa Libertadores Mwaka 2009.
Giggs na Van Gaal wakiteta jamboKijana Jesse Lingard tayari ni mgonjwa aliumia Mguu kwenye mechi yao na Swansea juzi

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog