Razack Siwa (kushoto) akiwa na
aliyekuwa kocha wa zamani wa Yanga, Mholanzi, Ernie Brandits
Na Mwandishi Wetu, Tanga
ALIYEKUWA
Kocha wa makipa wa timu ya Yanga Razack Siwa hatimaye
ameingia
mkataba wa kuwanoa makipa wa timu ya Coastal Union ya Tanga ambayo inajiandaa na maandalizi ya msimu ujao wa Ligi
kuu Tanzania bara utakaoanza Mwezi
ujao hapa nchini.
Siwa ameingia mkataba wa
mwaka mmoja lengo likiwa kuipa mafanikio makubwa
timu hiyo msimu ujao.
Tayari
Kocha Siwa ameungana na wachezaji wa timu hiyo leo kupanda ndege
kuelekea Visiwani Pemba ambapo timu hiyo inakwenda kuweka kambi ikijiwinda na michuano ya Ligi kuu soka Tanzania bara.
Akizungumza
kabla ya timu hiyo kuondoka ,Katibu Mkuu wa Coastal Union ,Kassim
El Siagi amesema kuwa kocha huyo wa makipa anachukua nafasi iliyokuwa
wazi kutokana na kutokuwa na mwalimu maalumu wa kuwafundisha walinda milango wa Coastal Union.
Akizungumzia
safari ya timu hiyo, El Siagi alisema kuwa safari ya timu hiyo
leo wameondoka wachezaji 27 wakiaambana na walimu wa timu hiyo
ambao wameondoka ambapo watakapofika pemba
watafanya mazoezi kwenye uwanja wa
soka Gombani.
Safari
hiyo imefadhiliwa na wadhamini wa timu hiyo kiwanda cha Pemba Floor
Mils kilichopo mjini Tanga ambao wamedhamiria kuhakikisha wanaipa
mafanikio timu hiyo.
Katibu
huyo amesema wakiwa visiwani humo watacheza mechi nne za majaribio
ambazo zilikwisha kutayarishwa na chama cha mpira wa miguu Pemba
pamoja na kuwataka mashabiki na wapenzi wa timu hiyo kuacha kuwa na wasiwasi na timu hiyo kwa sababu wamefanya usajili
wa nguvu .
0 maoni:
Post a Comment