Rais
wa Kenya Uhuru Kenyatta ameizawadi kwa kuifadhili timu ya taifa ya soka
Harambe Stars ziara ya kwenda Brazil kutazama michuano ya kombe la
dunia Hafla ya kuikabidhi rasmi ufadhili huo timu hiyo, ilifanyika
katika ikulu ya Rais Ijumaa ambapo wachezaji kumi na moja wa timu hiyo
walikabidhiwa tiketi za ndege kwenda Brazil. Kitendo cha Rais bila
shaka ni jambo la kutaka kuwatia motisha wachezaji wa timu ya taifa
ambao hivi karibuni waliicharaza Djibouti mabao mawili kwa moja katika
duru ya kwanza ya michuano ya kuwania kombe la taifa bingwa Afrika
baadaye mwakani.
Rais Kenyatta akiongea na Wachezaji wa Timu hiyo.

Hapa Akigawa tiketi huku akishuhudiwa na mkewe Bi. Margaret Kenyatta na seneta wa Nairobi Mike Sonko (kushoto).

Picha ya Pamoja.
0 maoni:
Post a Comment