Alama
ya chaki ya kupulizia (spray) ni moja ya ingizo jipya kwenye michuano
ya Kombe la Dunia nchini Brazil. Tayari refa ameshaitumia mara ya kwanza
kwenye mechi ya ufunguzi kati ya Brazil na Croatia usiku wa kuamkia
leo, pale refa alipochora kwa kupulizia na kuweka alama wapi wachezaji
wasimame wakati wa kupigwa mpira wa adhabu (pichani chini), ili
kuthibiti zogo la wachezaji, ama wapi mpira uwekwe kabla ya kupigwa.
Chaki hiyo, ambayo huyeyuka baada ya dakika chache, ilianza kutumika
mwaka jana kwenye kombe la Klabu Bingwa ya Dunia ambapo huko Argentina
na Brazil ilitumika kwa Misimu kadhaa iliyopita.
0 maoni:
Post a Comment