Croatia ndio waliotangulia kupata Bao kwenye Dakika ya 11 baada ya Krosi ya chini kutoka Winga ya Kushoto kumkuta Fulbeki wa Kushoto wa Brazil Marcelo ambae alitumbukiza Mpira wavuni bila kutegemea.
Supastaa Neymar aliamsha sherehe Uwanja mzima na Nchi nzima ya Brazil baada ya kusawazisha kwenye Dakika ya 29 kwa Shuti la chinichini la Mguu wa Kushoto.
Kipindi cha Pili, Brazil walipewa Penati baada ya Beki wa Croatia, Lovren, kumwangusha Fred na Neymar kupiga Bao la Pili.
Huku Dakika zikiyoyoma na Croatia kujikakamua kutaka kusawazisha, kaunta ataki ya Brazil ilizaa Bao la Tatu kwa kazi njema na ya ufundi ya Oscar.
Hakunaga! Neymar akishangilia...huku macho yote ya Brazil yakiwa kwake.......
Oscar akimpelekesha Vedran
Oscar akifunga bao la tatu katika dakika za lala salama
3-1 Croatia wakijionea wenyewe
RSS Feed
Twitter
11:43 PM
Unknown
0 maoni:
Post a Comment