Maelfu wamekaidi hali mbaya ya
hewa na kufurika uwanja wa FNB kuhudhuria misa ya wafu ya rais mstaafu
wa Afrika Nelson Mandela. Je una ujumbe wowote kwa watu wa Afrika
Kusini?
Unaweza
kuutuma kwenye ukurasa wetu wa na kisha nitauweka hapa kwenye mtandao
wetu wa Je uko Afrika Kusini? nini kinajiri huko mbali na misa hii
kufanyika?
12:00 Obama: ''Hatutawahi kuwa na kiongozi kama Mandela duniani tena. Lakini nataka kuwashauri vijana kote Afrika na duniani kote kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo zake Mandela.''
11:51 Obama :'Kumbukumbu za Mandela hunifanya kila siku kutaka kuwa mtu mwema na nataka kuwashauri vijana kuhakikisha kuwa wanafuata nyayo za Mandela'
1135 Obama: ''Asanteni sana kwa kuturuhusu kumuenzi Nelson Mandela, alikuwa mkombozi aliyetetea demokrasia na anaweza tu kufananishwa na marehemu Mahatma Ghandi. Ni vyema kumkumbuka Mandela kama mtu aliyejitolea sana na hakuogopa kushauriana nasi kuhusu maoni yake na hisia zake na kwa sababu Mandela aliweza kukubali kuwa mtu wa kawaida mtu ambaye aliweza kufanya makosa kama mwanadamu mwengine yeyote ule.''
11:15.....Dlamini Zuma, 'Tunamuenzi Madiba, alikuwa shujaa aliyekuwa tayari kusikiliza maoni ya watu wengine licha ya kukinzana na yake. Ni shujaa wa Afrika ambaye alijitolea kuikiomboa Afrika na juhudi hizo hazikuwahi kumuondoka daima hadi kifo chake.''
11:12 am Mwenyekiti wa tume ya Muungano wa Afrika Dr Nkosazana Dlamini Zuma anahudhuria umati wa watri kwenye misa hiyo
11:09 am: Denis bazira kutoka kahama Tanzania ameandika kwenye ukurasa wa facebook amesesma Mungu aiweke pahala pema roho ya shujaa na mkombozi wa Afrika. R.I.P MADIBA
11:05 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon amemaliza kuhutubia umati wa watu waliokusanyika kwenye misa ya wafu ya Mandela
11:00 Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki Moon anahutubia umati wa watu waliokusanyika katika uwanja wa FNB
0 maoni:
Post a Comment