MECHI ya Nusu Fainali ya Kombe la Mataifa ya Afrika
Mashariki na Kati, CECAFA Challenge kati ya Tanzania Bara ‘Kilimanjaro
Stars’ na Kenya ‘Harambee Stars’ iliyopangwa kuanza Saa 7:00 mchana huu
Uwanja wa Kenyatta, Machakos, imeahirishwa na sasa itachezwa Saa 12:00
jioni Uwanja wa Nyayo, Nairobi, Kenya.
|
Hii ndiyo hali halisi ya Uwanja wa Kenyatta, Machakos
|
Katibu wa Baraza la Vyama vya Soka Afrika Mashariki na
Kati
(CECAFA), Nicholas
Musonye amesema kwamba sababu ya kufikia hatua hiyo
ni hali mbaya ya Uwanja wa Kenyatta
kufuatia mvua kubwa iliyonyesha leo.
Makocha wa timu zote, Kim Poulsen wa Tanzania Bara
na Adel
Amrouche wa Kenya wamekagua
Uwanja na kujiridhisha haufai kuchezewa,
ingawa
Mwenyekiti wa Shirikisho la Soka Kenya (FKF)
alikuwa anashinikiza
mechi hiyo ichezwe hapo hapo.
Lakini pamoja na Musonye kutoa uamuzi huo,
Nyamweya amewaamuru
wafanyakazi wa Uwanja
wachote maji uwanjani aking’ang’aniza mechi
ichezwe hapo.
|
Amrouche kushoto akimbishia Nyamweya mbele ya Musonye |
|
Kim Poulsen ameweka msimamo hachezi Kenyatta |
|
0 maoni:
Post a Comment