Maelfu ya watu
wanaendelea kuwasili katika uwanja mkubwa wa FNB mjini Johanessburg kwa
ajili ya misa ya wafu ya hayati Nelson Mandela,
Unahitaji toleo sahihi la Flash Player kucheza sauti/video
Misa ya kitaifa ya wafu kumuaga Hayati Nelson Mandela, inaendelea mjini Johannesburg Afrika Kusini.
Rais wa Marekani Barack Obama na katibu mkuu wa
Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon watakuwa miongoni mwa viongozi wa dunia
watakaohutubia muhadhara huo.Viongozi hao pia watahutubia wananchi sawa na wajukuu wanne wa Mandela .
Maelfu ya watu wamehudhuria misa hiyo katika uwanja wa FNB.
Afrika Kusini imeandaa shughuli mbali mbali za kumuenzi Mandela kabla ya siku ya kuzikwa kwake nchini Afrika Kusini siku ya Jumapili.
Misa ya leo ni moja ya mikusanyiko mikubwa ya viongozi wa kimataifa iliyoshuhudiwa nchini humo katika miaka ya hivi karibuni.
Viongozi wengine Watakaohudhuria misa ya wafu ya Mandela:
Viongozi wanaohudhuria misa ya wafu ya Mandela
- Rais wa Marekani Barack Obama
- Katibu mkuu wa Umoja wa Mataifa Ban Ki-moon
- Rais wa Cuba Raul Castro
- Rais wa Ufaransa Francois Hollande
- Waziri mkuu wa Uingereza David Cameron
- Rais wa Brazil Dilma Rousseff
- Rais wa Zimbabwe Robert Mugabe
Waliohudhuria misa hiyo wamesemekana kuwa wenye furaha wakiimba nyimbo na kutaja jina la Mandela kwa shangwe unaweza kudhani ni mkutano wa kisiasa.
Misa hiyo itafanyika katika uwanja ambako Nelson Mandela alionekana kwa mara ya mwisho hadharani.
Misa hiyo itaonyeshwa kwenye skrini kubwa nje ya uwanja ili kuzuia msongamano wa watu.
Mandela alifariki akiwa na umri wa miaka 95 na kwa wengi yeye ni shujaa na mkombozi wa Afrika Kusini.
0 maoni:
Post a Comment