Wengi
walioipata hii taarifa wanashangaa imekuaje ni viungo tu vya binadamu
vimepatikana kwenye kontena zima vikiwa vinaingizwa Kenya? vinakwenda
wapi? kazi yake ni nini?
Taarifa
iliyoripotiwa na Citizen TV Kenya inasema Shehena hii iliyokamatwa
baada ya kupitishwa kwenye bandari ya Mombasa inasemekana imesafirishwa
na Mwanasiasa maarufu ambae kabla ya kukamatwa alisema ilikua na bidhaa
za nyumbani ambapo ilipofika kwenye kituo cha ukaguzi wa mashehena cha
Changamwe ilipatikana na vikaragosi vya mafuvu na mifupa ya binadamu
ndipo amri ikatoka kontena likamatwe.
Baadhi
ya mifupa ya binadamu iliyopatikana ni pamoja na mafuvu, miguu na
mikono pamoja bidhaa za nyumba ambapo vyote kwa pamoja vilikua
vinasafirishwa ambapo Afisa wa maswala ya Uhusiano mwema wa KRA Fatuma
Yusuf alithibitisha kwamba hii shehena iliingia kutoka China siku ya
pili ya October 2013 kabla ya kugundulika ilikua na vikaragosi vya
kutisha ikiwemo mifupa ya binadamu.
Mpaka
sasa uchunguzi wa shehena hili unaendelea lakini baadhi ya wakazi wa
Mombasa wameonyesha wasiwasi wao na kusema kuna haja ya Serikali kutoa
ripoti ya ibada za kishetani ambayo inasemekana kubuniwa na Rais Mstaafu
Daniel Arap Moi miaka kadhaa iliyopita.
0 maoni:
Post a Comment