.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(kushoto) akisoma hotuba
yake fupi mbele ya Balozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya Nchini Tanzania,
Mhe. Filiberto Sebregondi(aliyeketi mbele) pamoja na Mabalozi wa Jumuiya
ya nchi za Ulaya wanaoonekana katika picha kabla ya kutembelea sehemu
mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini Dar es Salaam.
Mabalozi
wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya wakiwasilikiza kwa makini Wafungwa wa
Gereza Kuu Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliohukumiwa Adhabu ya
Kunyongwa(hawapo pichani) ambapo wameiomba Jumuiya ya Ulaya kuendelea
kupaza sauti na kuishauri Serikali ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania
ili Adhabu hiyo hapa Nchini Tanzania iweze kuondelewa(wa pili kulia) ni
Balozi wa Uingereza Nchini Tanzania, Mhe. Dianna Melrose.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja( wa tatu kushoto mstari
wa pili) akiongozana na Mabalozi mbalimbali wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya
kuelekea sehemu ya Zahanati ya ndani inayohudumia Wafungwa wa Gereza Kuu
Ukonga, Jijini Dar es Salaam waliopotembelea leo Oktoba 10, 2013.
Kamishna
Jenerali wa Magereza Nchini, John Casmir Minja(wa pili kushoto) akiwa
katika picha ya pamoja na Mabalozi wa Jumuiya ya Nchi za Ulaya mara
baada ya kutembelea sehemu mbalimbali za Gereza Kuu Ukonga leo Jijini
Dar es Salaam(wa tatu kushoto) ni Balozi wa Jumuiya ya Ulaya Nchini
Tanzania, Mhe. Filiberto Sebregondi ambaye aliongoza Ujumbe wa Mabalozi
hao(Picha zote na Lucas Mboje wa Jeshi la Magereza).
Friday, October 11, 2013
2:36 AM
Unknown
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
RSS Feed
Twitter
0 maoni:
Post a Comment