Sunday, November 8, 2015



Bao za Kipindi cha Pili za Jesse Lingard na Juan Mata Leo zimewapa Manchester United ushindi wa Bao 2-0 walipocheza na West Bromwich Albion kwenye Mechi ya Ligi Kuu England Uwanjani Old Trafford.
Mapema Kipindi cha Pili, Lingard, mwenye Miaka 22, aliifungia Man United Bao la Kwanza kwa shuti la kupinda na Juan Mata kuongeza Bao la Pili katika Dakika za Majeruhi kwa Penati baada ya Anthony Martial kuchezewa Faulo na Gareth McAuley ambae alitolewa kwa Kadi Nyekundu.Ushindi huu umewabakisha Man United Nafasi ya 4 kwenye Ligi Kuu England ikiwa ni ushindi wao wa kwanza baada ya Mechi 3 za Ligi na Mechi yao inayofuata ni ugenini na Watford hapo Novemba 21.
Mata akichonga penatiBastian ChiniCameron nae leo kacheza na Timu ya wakubwaLingard akipongezwaJesse akiponngezwa kwa bao safiJesse akishangiliaDe Gea nae alifurahia baoShangwe!Martial akichuana na EvansWakiunga UkutaWanajuana: Rooney na Fletcher

Saturday, November 7, 2015



VIKOSI:
Bournemouth:
Federici, Smith, Francis, Distin, Daniels, Ritchie, Surman, Gosling, Stanislas, Arter, King.
Akiba: Boruc, Cook, Rantie, MacDonald, Kermorgant, Tomlin, Bennett.
Newcastle: Elliot, Janmaat, Mbemba, Coloccini, Dummett, Sissoko, Anita, Wijnaldum, Tiote, Mitrovic, Perez.
Akiba: Cisse, De Jong, Gouffran, Lascelles, Thauvin, Woodman, Mbabu.

LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Novemba 7
 

 Bournemouth 0 v 0 Newcastle
18:00 Leicester v Watford
18:00 Man United v West Brom
18:00 Norwich v Swansea
18:00 Sunderland v Southampton
18:00 West Ham v Everton
20:30 Stoke v Chelsea

Friday, November 6, 2015


Klabu ya Chelsea ya Uingereza Jumamosi ya November 7 itasafiri kuifuata Klabu ya Stoke City kucheza mchezo wake wa wa Ligi Kuu Uingereza bila kuwa na kocha wao Jose Mourinho ambaye anatumikia adhabu ya kufungiwa mchezo mmoja sambamba na faini ya pound 40,000/= kwa kosa alilolifanya la kutoa lugha chafu kwa waamuzi wa mechi ya Chelsea dhidi ya West Ham United.
Jose Mourinho ambaye anajulikana kwa tabia yake ya kupenda timu yake ipate matokeo mazuri wakati wote, wengi walitegemea kuona akikata rufaa ya adhabu hiyo licha ya kuwa hakufanya hivyo na sio kawaida yake kukubali kushindwa mapema. November 7 Mourinho amejibu sababu za yeye kutokata rufaa ya adhabu hiyo, ni kweli amekubali alikosea au?
Jose-Mourinho-617546
“Mechi ni kesho na najua majibu ya rufaa kama ningekuwa nimekata, hivyo niliamua kukata tamaa na maamuzi hayo, nafikiri ni ujinga kupambana pambano ambalo tayari unaamini ulishashindwa” >>> Jose Mourinho

Thursday, November 5, 2015

DSC_0168

Mwanamuiki nyota nchini Tanzania, Nassib Abdul ama Diamond Platnumz akiongea na waandishi wa habari
KAMPUNI ya MultiChoice Tanzania mapema jana imezindua ofa kabambe za msimu wa siku kuu huku ikimtambulisha rasmi Mwanamuziki Diamond Platnumz kuwa balozi maalum wa bidhaa za kampuni hiyo ikiwemo kifurushi cha DSTV BOMBA chenye chaneli zaidi ya 65 ikiwemo huduma ya vituo kadhaa vya televisheni za hapa nchini.

Akimtambulusha rasmi Meneja Masoko wa kampuni hiyo, Furaha Samalu, amemtambulisha Nasibu Abdul ‘Diamond Platnumz’ kuwa balozi wa king’amuzi hicho na kutaja gharama zake kuwa ni shilingi 23,500/= kwa malipo ya mwezi na king’amuzi chenyewe kinapatikana kwa shilingi 79,000/= na kuwataka wananchi kuchangamkia huduma hiyo muhimu katika msimu huu wa ofa za sikukuu.

Meneja masoko huyo ameongeza kuwa, kifurushi hicho kimesambaa nchini mbalimbali barani Afrika hivyo wasanii wa filamu, muziki na wengineo ambao watang’aa kwenye vipindi hivyo watakuwa wakionekana pande mbalimbali barani Afrika na hivyo kuwapatia umaarufu na kuwaongezea soko la kazi zao.
DSC_0151
Mwanamuziki Diamond Platinumz akisoma kipeperushi chenye maelezo juu ya ofa mbalimbali za DStv wakati wa utambulisho wa ofa za sikukuu pamoja na kutangazwa kwa balozi huyo wa bidhaa za DSTV. Katikati Afisa Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo.
DSC_0233
Meneja Masoko wa Multichoice Tanzania, Furaha Samalu akifafanua jambo katika mkutano huo na kushoto ni Meneja Mwendeshaji wa Multichoice Tanzania, Ronald Baraka Shelukindo na upande wa kulia ni msanii Diamond Platnumz balozi wa bidhaa za DSTV.
DSC_0159
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum Salum akifafanua jambo juu ya ofa hiyo mpya na mahaala wanapopatikana nchini kwa mawakala wote ambapo amewaomba watanzania kuchangamkia ofa ya kuunganishwa haraka huduma bora zaidi za chaneli za kisasa kupitia DSTV.
DSC_0174
Baadhi ya wanahabari wakifuatilia mkutano huo wa DSTV..

DSC_0176
Mwandishi wa gazeti la Raia Tanzania akiuliza swali juu ya bidhaa za DSTV..
DSC_0171
Mpiga picha wa Magazeti ya Habari leo, Fadhili Akida akiuliza swali katika mkutano huo wa DSTV..
DSC_0185
Ilifika wakati wa zawadi.. Diamond akisoma jina la mwandishi wa habari aliyeshinda zawadi hiyo..
DSC_0190
Diamond Platnumz akimkabidhi mwandishi wa habari, Sangu Joseph king'amuzi alichojishindia katika droo iliyochezeshwa wakati wa mkutano huo.
DSC_0196
Diamond akikabidhi zawadi ya King'amuzi cha DSTV kwa mwandishi wa habari Rajab Musa baada ya kushinda..
DSC_0204
Diamond akikabidhi zawadi ya king'amuzi kwa mwandishi wa habari, Joseph Mchekadone baada ya kushinda..
DSC_0205
Diamond Platnumz akimkabidhi king'amuzi mwanahabari wa ITV, Ester Sangai baada ya kuibuka mshindi..
DSC_0165
Meneja mauzo wa DSTV, Bw. Salum akisisitiza juu ya ofa hiyo ambapo ameeleza kuwa wateja watapa kujionea chaneli mbalimbali zenye mvuto na picha za kuvutia huku bidhaa zake zikiwa ni tofauti kabisa na zingine.

jeff
Mwanamuziki aliyewahi ishi nchini Tanzania na pia mwenye asili ya Congo, Jeff Maximum ambaye anaishi Ughaibuni katika shughuli zake za Muziki katika pozi ambapo kwa sasa ameachia video ya wimbo wake mpya wa "Mama Afrika" ambao wimbo huo unatangaza Utalii wa Tanzania.


Mwanamuziki anayefanya kazi zake nchini Marekani na Dubai, Jeff Maximum tayari ameshaachia video ya wimbo wake mpya uitwao “Mama Afrika” ambao umetayarishwa Bagamoyo Nchini Tanzania hivi karibuni.

Kwa mujibu wa Jeff anaweka wazi kuwa, kuwa video hiyo iliyoachiwa Novemba 2 mwaka huu, tayari imeshaanza kuonekana katika vituo mbalimbali vya televisheni Bara la Afrika ikiwemo nchini, pia katika nchi za Nigeria, Afrika Kusini, Kongo, Ghana, Kenya na kwingineko.

Pia video hiyo inaonekana katika vituo vya televisheni vya nchini Uingereza, Dubai, Amerika na kwingineko huku ikitangaza utalii wa Tanzania kwa asilimia kubwa.Jeff anaweka wazi kuwa, aliamua kuitayarishia video hiyo nchini Tanzania kwa kuwa ni kati ya nchi nyingi anazozipenda zaidi Barani Afrika.

Na kuongeza kuwa, video hiyo imetengenezwa na mwongozaji anayechipukia kutoka Tanzania Hanscana (Wanene Films), huku audio yake ikiwa imetayarishwa katika studio yake iliyopo nchini Dubai



Ushirikina ni jambo ambalo limekuwa likihusishwa kwa kiasi kikubwa katika soka hususani barani Afrika, hata katika timu zetu za Ligi Kuu Tanzania bara zimekuwa zikifanya baadhi ya vitu ambavyo vinahusishwa na imani za kishirikina, millardayo.com ilipata bahati ya kufanya exclusive interview na Gaudence Mwaikimba kuhusu ishu za ushirikina katika soka.
DSC_0008
Kama utakuwa unakumbuka vizuri Gaudence Mwaikimba ni mshambuliaji wa zamani wa klabu ya Dar Es Salaam Young Afrika, Azam FC na timu ya taifa ya Tanzania Taifa Stars, Mwaikimba kwa sasa anachezea klabu ya JKT Ruvu ila ni kweli anaamini ushirikina katika soka yeye kama mchezaji mkongwe?
Mwaikimba amekiri katika soka kuwa na imani za kishirikina ila yeye haamini kama inaweza msaidia mtu kucheza vizuri au kufunga magoli katika mechi, ila amewahi kushuhudia mtu akianguka uwanjani baada ya kuingia na irizi ila baadae alianguka na kuanza kutoa mapovu mdomoni.
m_Atlabara-Azam-Fc-share-spoils
“Ndio maana hadi leo mimi siamini ushirikina katika soka kwani nimewahi kushuhudia mtu akianguka uwanjani sababu ya hivyo vitu ila ilikuwa Ligi daraja la tatu, ilikuwa ni mtu kaweka irizi mguuni, mwisho wa siku akapigana kibuyu na mchezaji wa timu yetu akaanguka na kuanza kutoa povu kumvua soksi akakutwa na irizi” >>> Mwaikimba



Usiku wa November 4 kulichezwa michezo kadhaa ya mechi za Ligi ya Mabingwa Ulaya na tuliona baadhi ya vilabu vikiondoka na point tatu kwa furaha na timu nyingine zikiondoka vichwa chini baada ya kupoteza michezo hiyo, Usiku wa November 5 mechi za UEFA ndogo zilipigwa kama kawaida.
2198682_heroa
Klabu ya Liverpool ya Uingereza ililazimika kusafiri hadi Urusi kucheza na Rubin Kazan katika muendelezo wa mechi za Kundi B, Liverpool wakiwa ugenini wamefanikiwa kuibuka na ushindi wa goli 1-0, licha ya kuwa walikuwa ugenini Liverpool walifanikiwa kuibuka na point tatu mbele ya Rubin Kazan.
3000
Hadi dakika 45 za kwanza zinamalizika hakuna timu iliyokuwa imefanikiwa kuona lango la mpinzani wake, kipindi cha pili kilianza kwa kila timu kucheza kwa tahadhari, kabla ya dakika ya 52 Liverpool walifanikiwa kupata goli la kwanza kupitia kwa Jordon Ibe, goli ambalo lilidumu kwa dakika zote 90.
3000 (1)
Baadhi ya Matokeo ya mechi nyingine za UEFA EUROPA LEAGU November 5
  • Ajax 0 – 0 Fenerbahce
  • Celtic 1 – 2 Molde
  • Sion 1 – 1 Bordeaux
  • Borussia Dortmund 4 – 0 FK Qabala
  • FC Krasnodar 2 – 1 PAOK Thessaloniki FC
  • Club Brugge 1 – 0 Legia Warszawa
  • SSC Napoli 5 – 0 FC Midtjylland
  • Dinamo Minsk 1 – 2 Villarreal
  • Viktoria Plzen 1 – 2 Rapid Wien
Magoli ya Rubin Kazan Vs Liverpool

waliotembelea blog