Sunday, September 20, 2015



Timu ya West Ham United sasa wamekuwa mafundi wa kuzibomoa Timu kubwa Nyumbani kwao Msimu huu baada ya Jana kuwatandika Vinara wa Ligi Kuu England Manchester City Bao 2-1 wakiwa kwao Etihad na kuwaonjesha kipigo chao cha kwanza kwenye Ligi Msimu huu.
Kipigo hiki pia ni cha pili mfululizo kwa City ambao Kati-Wiki walichapwa 2-1 na Juventus hapo hapo Etihad kati Mechi ya Kundi lao la UEFA CHAMPIONS LIGI.
Katika Mechi yao ya kwanza Msimu huu, West Ham, wakicheza Ugenini huko Emirates, waliifunga Arsenal 2-0 na kisha huko Anfield kuibamiza Liverpool 3-0.
Jana huko Etihad, West Ham, chini ya Meneja wao mpya kutoka Croatia Slaven Bilic, walitangulia kwa Bao 2 zilizofungwa na Mchezaji wa Mkopo kutoka Chelsea Victor Moses katika Dakika ya 6 na Diafra Sakho katika Dakika ya 31.
Bao la City lilifungwa na Mchezaji wao mpya Kevin De Bruyne katika Dakika ya 46.
Hadi Mapumziko City 1 West Ham 2.
Kipindi cha Pili, City, waliocheza bila ya Mastaa wao Majeruhi, Vincent Kompany na David Silva, walikuja juu lakini West Ham walisimama kidete kulinda Bao zao.

BAO la Victor MosesKocha wa West Ham United















FULL TIME: CHELSEA 2 vs 0 ARSENAL

Chelsea Leo wameanza kufufua matumaini ya kutetea Taji lao baada ya kuwafunga Mahasimu wao wa Jijini London Mtu 9 Arsenal Bao 2-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England iliyochezwa Uwanjani Stamford Bridge.
Baada ya kuanza Hovyo kwa kufungwa Mechi 3, Sare 1 na Kushinda 1 tu na kujikuta wako Nafasi ya 17 wakiwa Pointi 11 nyuma ya Vinara Man City, Leo Chelsea walikamia ushindi na Diego Costa alihakikisha hilo baada ya kuwachokoza Mabeki wa Arsenal na kusababisha Sentahafu wao apande jazba na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Katika Dakika ya 44 ilizuka purukushani kati ya Diego Costa wa Chelsea na Laurent Koscielny wa Arsenal na Costa kuonekana kumpiga Koscielny kisha kumusukuma kwa Kifua hadi chini lakini, kwa mshangao mkubwa, Refa Mike Dean hakumwadhibu Costa kama ilivyotegemewa na badala yake kuwapa Kadi za Njano Costa na Sentahafu wa Arsenal anaetoka Brazil Gabriel. Dakika moja baadae Gabriel alitolewa nje kwa Kadi Nyekundu baada ya kumrushia teke Costa.
Hadi Haftaimu, Chelsea 0 Arsenal 0.
Kipindi cha Pili Dakika ya 53, Frikiki ya Fabregas iliunganishwa kwa Kichwa na Kurt Zouma na kuwapa Chelsea Bao.
Dakika ya 79, Arsenal walibaki Mtu 9 baada ya Kiungo wao Santi Cazorla kupewa Kadi ya Njano ya Pili na kutolewa nje kwa Kadi Nyekundu.

Eden Hazard aliipa Chelsea Bao lao la pili katika Dakika ya 91 baada ya Shuti lake kumbabatiza Alex Oxlade-Chamberlain na kutinga.Eden HazardKurt Zouma aipatia bao la kuongoza Chelsea kipindi cha pili dakika ya 53, Bao la kichwa.Gabriel nje kwa kadi nyekundu!

Friday, September 18, 2015



Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akishuka kutoka kwenye Helkopta anayoitumia kwa ziara zake za Kampeni, wakati akiwasili kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa pamoja na Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye, wakiwasalimia wananchi wa Mji wa Muleba, wakati walipowasili kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015, kulikofanyika Mkutano wa Kampeni za Mgombea huyo.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa akisalimiana na Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muleba Kusini kupitia CHADEMA, Kashasira Alistides, wakati wa Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, Mjini Muleba, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015. Katikati ni Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye.

Waziri Mkuu wa Zamani, Mh. Fredrick Sumaye akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Aliekuwa Mbunge wa Jimbo la Nyamagana Jijini Mwanza, Mh. Ezeckiel Wenje akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni za Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akihutubia wananchi kwenye Mkutano wa Kampeni zake za kuwania nafasi hiyo, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, katika Jimbo la Muleba Kusini, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.

Mgombea Urais wa Tanzania wa UKAWA kupitia Chama cha Demokrasia na Maendeleo (CHADEMA), Mh. Edward Lowassa, akimnadi kwa wananchi, Mgombea Ubunge wa Jimbo la Muleba Kusini kupitia CHADEMA, Kashasira Alistides, katika Mkutano wa Kampeni, uliofanyika kwenye Uwanja wa Fatuma, Mjini Muleba, Mkoani Kagera leo Septemba 15, 2015.



LIGI KUU ENGLAND
RATIBA:
Jumamosi Septemba 19

14:45 Chelsea vs Arsenal
17:00 Aston Villa vs West Brom
17:00 Bournemouth vs Sunderland
17:00 Newcastle vs Watford
17:00 Stoke vs Leicester
17:00 Swansea vs Everton
19:30 Man City vs West Ham
Jumapili Septemba 20
15:30 Tottenham vs Crystal Palace
18:00 Southampton vs Man United
18:00 Liverpool vs Norwich
Jose Mourinho v Arsene Wenger


FIFA imetangaza kuwa ile Hafla ya kumtangaza Mchezaji Bora Duniani kwa Mwaka 2015 ambae hutunukiwa Tuzo ya FIFA Ballon d’Or itafanyika Jumatatu Januari 11, 2016 huko Zurich Nchini Uswisi.
Siku hiyo pia hutangazwa Mchezaji Bora kwa upande wa Kinamama pamoja na Kocha Bora kwa pande zote mbili za Wanaume na Wanawake.
Pia, Goli Bora la Mwaka, ambalo hutunukiwa Tuzo ya Puskas, litajulikana baada ya Kura kutoka kwa Wadau wote inayofanyika Mtandaoni.
Tuzo nyingine ambazo zitatolewa Siku hiyo ni ile ya Uchezaji wa Haki na pia, kwa kushirikiana na FIFPro, Chama cha Wachezaji wa Soka la Kulipwa, kitatangazwa Kikosi Bora cha Mwaka kijulikanacho kama FIFA FIFPro World XI.
Tuzo ya mwisho itakayotolewa Siku hiyo ni ile Tuzo ya Rais wa FIFA ambayo humwendea Mtu au Taasisi iliyotoa mchango bora katika Soka.

FIFA Ballon d’Or
WASHINDI WALIOPITA:

2014 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2013 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2012 Lionel Messi [Argentina]
2011 Lionel Messi [Argentina]
2010 Lionel Messi [Argentina]
2009 Lionel Messi [Argentina]
2008 Cristiano Ronaldo [Portugal]
2007 Kaká [Brazil]



Kufuatia safari ya vijana watano wa U15 Asaad Ali Juma, Maziku Aman, Issa Abdi, Kelvin Deogratias, Athumani Maulid waliokwenda kufanya mazoezi kwenye klabu ya Orlando Pirates kufuatia mwaliko uliotolewa na TFF na klabu hiyo, safari hiyo ilikamilika na vijana wamerejea nyumbani.
Vijana hawa waliongozana na Mkurugenzi wa Ufundi wa TFF, Salum Madadi wakiwa Afrika Kusini walifanya mazoezi ya wiki moja kuanzia Septemba Mosi mpaka tarehe 7 Septemba, 2015 chini ya uangalizi wa Augusto Placious ambaye ni Mkurugenzi wa Ufundi wa Orlando Pirates.
Idara ya ufundi ya Orlando Pirates imejiridhisha na kiwango kilichoonyeshwa na vijana hao.

waliotembelea blog