Tuesday, August 18, 2015



Meneja masoko na mauzo wa Kampuni ya Mega Trade Edmundi Rutaraka, akimkabidhi hundi ya Ts 1.5 Milioni Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo na burudani mkoa wa Arusha,Mussa Juma kwa ajili ya tamasha la 10 waandishi wa habari mkoa wa Arusha, Manyara na Dar es salam na wadau wa habari ambalo litafanyika Agoust 29 uwanja wa sheikh Amri Abeid, hafla hiyo ilifanyika jana, Palace Hoteli Jijini.habari na libeneke la kaskazini blog
Tamasha la 10 la vyombo vya habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha, linatarajiwa kufanyika Agosti 29 katika uwanja wa Sheikh Amri Abeid kwa kushirikisha timu nane ikiwepo timu ya TASWA kutoka jijini Dar es Salaam.
Akizungumza na waandishi wa habari, Palace Hotel , Katibu wa chama cha waandishi wa habari za michezo mkoa wa Arusha(TASWA-Arusha), Mussa Juma, alisema tayari maandalizi muhimu yamekamilika.
Juma alisema Tamasha hilo linaloandaliwa na TASWA na kampuni ya Arusha Media.mdhamini Mkuu ni Kampuni ya Bia nchini( TBL) kwa miaka 10 sasa, litashirikisha michezo ya Soka, Mpira wa pete, kuvuta kamba na kukimbiza kuku.

"tunapenda kutangaza rasmi tamasha la 10 ya TASWA Arusha litafanyika Agosti 29 na kauli mbiu yetu ni Uchaguzi Mkuu bila vurugu inawezekana"alisema
Alisema katika Tamasha hilo, ambalo litashirikisha pia timu za wafanyakazi wa kampuni ya bia nchini(TBL) Taasisi na Faidika na kampuni ya Pepsi litaandamana na ziara ya wanahabari kutembelea Hifadhi ya Taifa ya Arusha.

Nahodha wa timu ya TASWA Arusha, Ramadhani Siwayombe akikabidhiwa jezi kwa ajili ya tamasha la waandishi wa habari na wadau wa habari mkoa wa Arusha ambalo litafanyika Augosti 29 Sheikh Amri Abeid, anayemkabidhi ni Filbert Masele meneja mikopo ya wafanyakazi wa FAIDIKA na Meneja wa FAIDIKA mkoa wa Arusha Eliya Mlay hafla hiyo, ilifanyika Palace hotel

Wakizungumza katika kikao hicho, Meneja wa Masoko wa kampuni ya Mega Trade Edmund Rutaraka, Meneja masoko wa kampuni ya SBC(T) Lalit Sharma na Meneja wa Faidika Arusha,Eliya Mlay walisema wamedhamini Tamasha hilo ili kuendeleza michezo.

Monday, August 17, 2015


Benteke dakika ya 26 aliiwezesha Liverpool kupata bao la kuongoza katika kipindi cha kwanza, Bao lililowashangaza wapinzani wao AFC Bornemouth wakiduwaa pia wakitegemea refa mshika kibendera wakiona kama ni la kuotea kumbe la!
VIKOSI:
Liverpool XI:
Mignolet, Clyne, Lovren, Skrtel, Gomez, Henderson, Milner, Coutinho, Lallana, Ibe, Benteke
Liverpool Akiba: Bogdan, Toure, Firmino, Moreno, Can, Origi, Ings 


Bournemouth XI: Boruc, Francis, Elphick, Cook, Daniels, Ritchie, O'Kane, Surman, Gradel, King, Wilson 

Bournemouth Akiba: Federici, Smith, Distin, Mings, Gosling, Pugh, Tomlin 
 Generated by  IJG JPEG Library 

Generated by  IJG JPEG Library 



during the Barclays Premier League match between Liverpool and A.F.C. Bournemouth at Anfield on August 17, 2015 in Liverpool, United Kingdom. 

Generated by  IJG JPEG Library 


during the Barclays Premier League match between Liverpool and A.F.C. Bournemouth at Anfield on August 17, 2015 in Liverpool, United Kingdom.
 
 Mwenyekiti wa Klabu ya Bournemouth Jeff Mostyn
 

Katibu mkuu wa Cuf Maalif Seif Shariff Hamad akimlaki mgombea urais kupitia Ukawa Edward Lowassa wakati alipowasiri visiwani Zanzibar kusawaka wadhamini wa kumdhami ikiwa sehemu ya masharti ya kugombea urais katika uchaguzu mkuu oktoba 25 na 26 mwaka huu.
Mwenyekiti mwenza wa Ukawa James Mbatia naye akilakiwa na Katibu mkuu wa Cuf Maalif Seif Shariff Hamad leo.

YANGA SC imesema kwamba imemsainisha Mkataba wa miaka miwili beki wa kati wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou baada ya kufaulu majaribio.
Bossou amefanyiwa majaribio kwa wiki moja katika kambi ya Tukuyu Mbeya, ikiwemo kucheza kwa dakika 45 mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbeya City jana Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Katika mchezo huo ambao Yanga SC ilishinda 3-2, Bossou aliondoka uwanjani Yanga SC ikiwa imefungwa bao moja na ikaongezwa la pili kipindi cha pili baada ya kuingia Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kwamba uongozi umemsaini Bossou, baada ya kupitishwa na kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm- Bossou.
Yanga SC imesema imemsainisha Mkataba wa miaka miwili Vincent Bossou (kulia)

Bossou aliyezaliwa Februari 7, mwaka 1986 mjini Kara, Togo, aliibukia klabu ya Maranatha FC ya kwao, kabla ya kusaini Etoile du Sahel ya Tunisia Januari 15, mwaka 2010 Mkataba wa miaka miwili.
Hata hivyo, Mkataba wa 'sentahafu' huyo Etoile Sportive du Sahel ulivunjwa baada ya miezi mitatu tu naye akarejea Maranatha FC Machi 18, mwaka 2010.
Mei mwaka 2011 akaenda kusaini klabu ya Navibank Saigon FC ya Vietnam, kabla ya kuhamia Becamex Binh Duong, baadaye TDC Binh Duongzote mwaka 2013, An Giang mwaka 2014 na Goyang Hi FC mwaka jana.
Alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kilichojitoa AFCON ya mwaka 2010 Angola baada ya basi la wachezaji kushambuliwa na majeshi ya waasi ikiwa njiani kuelekea kwenye fainali hizo.
Bossou, ambaye ameendelea kuwa mchezaji wa Togo hadi mwaka huu, aliwahi ‘kumvimbia’ Nahodha wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba wakati wa mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika baina ya Ivory Coast na Togo Uwanja wa Royal Bafokeng Januari 22, 2012 mjini Rustenburg, Afrika Kusini.
Nadir Haroub 'Cannavaro' sasa anaweza kupoteza namba kikosi cha kwanza Yanga SC baada ya kusajlliwa beki wa Togo


Kevin Yondan akimtoka kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy'. Beki huyo sasa anatakiwa kuongeza bidii ili kuinusuru nafasi yake kikosi cha kwanza Jangwani

Bossou anaungana na mabeki wengine wa 
kati Yanga SC, wazawa watupu, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati pia kiungo Mbuyu Twite raia wa DRC anaweza kucheza katikati.

Sunday, August 16, 2015


image3Ninayo Good News imenifikia mtu wangu ambayo Watanzania wengi na wakazi wa Dar es salaam tulikua tukiisubiri kwa muda mrefu ni kuhusu kukamilika kwa mradi wa Mabasi yaendayo haraka ambayo zaidi ya mwaka na nusu yaliingia kwenye headlines za kuwa yatatoa huduma hizo.
IMG_0146Habari ikufikie kuwa Mabasi hayo rasmi yanaanza kazi August 17 Jumatatu kuanzia  saa 3 asubuhi nje ya kituo cha Mabasi yaendayo Mikoani Ubungo ambako kutafanyika uzinduzi wa kuanza huduma ya mpito kisha Wananchi wataruhusiwa kupanda mabasi hayo kutoka Ubungo kwenda Kimara na kutoka Kimara hadi Kivukoni Bure.
Kwa bara la Afrika,jiji la Dar es salaam litakua la pili kutekeleza mradi huu mtu wangu baada ya Afrika Kusini na litakua jiji la kwanza kwa nchi za Afrika Mashariki,Kaskazini na Kati.
DeusiDedith Mutasingwa ambaye ni Afisa wa masuala ya fidia katika mradi wa mabasi haya yaendayo haraka yaliyo chini ya ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na serikali za mitaa,amesema yapo mabasi ya aina mbili kuna yale ya mita 18 ambayo yana uwezo wa kubeba abiria 140 na yapo yenye uwezo wa kubeba watu 80.
image1Amesema mabasi hayo pia yamezingatia watu wenye mahitaji maalum kama Walemavu na Wajawazito,pia Wafanyabiashara wanaopanga vitu vyao pembeni ya Barabara na kwenye vituo wameombwa kuviondoa na kwa wale watakaonekana kukaidi amri hiyo faini yake si chini 250,000.

Basi la Simba likiwasili uwanja wa Taifa
Basi la Simba likiwasili uwanja wa Taifa
Kikosi cha Simba SC leo kinacheza mchezo wake wa kirafiki wa kimataifa dhidi ya timu ya URA kutoka Uganda ikiwa ni sehemu ya maandalizi kuelekea msimu ujao wa ligi kuu Tanzania bara 2015-2016 mchezo utakaopigwa kwenywe uwanja wa Taifa. 
Hizi ni baadhi ya picha za wachezaji wa kikosi cha Simba wakati wakiwasili uwanja wa Taifa kwa ajili ya mchezo huo.
Wachezaji wa Simba kabla ya kushuka kwenye gari
Wachezaji wa Simba kabla ya kushuka kwenye gari
Ibrahim Ajibu
Ibrahim Ajibu
Mwinyi Kazimoto
Mwinyi Kazimoto
Justice Majabvi
Justice Majabvi
Awadh Juma
Awadh Juma
Simba

Sergio Aguero akishangilia bao lake la kwanza dhidi ya Chelsea.
Mbele ya Mashabiki 54,331 Uwanjani kwao Etihad, Manchester City Leo wamewabonda Mabingwa wa England Chelsea Bao 3-0 katika Mechi ya Ligi Kuu England.
Wakati huu ni ushindi wa pili mfululizo kwa City wa 3-0 kila Mechi tangu Ligi ianze Wikiendi iliyopita, kwa Chelsea hii ni Mechi yao ya pili bila ushindi baada kuanza kwa Sare ya 2-2 huko kwao Stamford Bridge walipocheza na Swansea City.
Hii Leo City walistahili ushindi dhidi ya Chelsea ambayo kwenye Benchi lake Leo alikosekana Daktari wao Mwanamama maarufu Eva Carneiro ambae amepigwa marufuku na Meneja wa Chelsea Jose Mourinho baada kutofautiana. Ramires katiMatic na Silva wakibananBaada ya Man City kupiga hodi mara kadhaa huku wakisimamishwa na ushujaa wa Kipa wa Chelsea Asmir Begovic ambae alikuwa Golini kuchukuwa nafasi ya Kipa Nambari Wani Thibaut Courtois aliefungiwa Mechi 1 baada ya Kadi Nyekundu katika Mechi iliyopita waliyotoka 2-2 na Swansea City, Man City walifanikiwa kufunga katika Dakika ya 31.
Kweupeee 1-0
1-0Bao hilo lilitokana na pasi safi ya David Silva na kumkuta Sergio Aguero alieachia shuti la chini na kutinga.
Kipindi cha Pili kilianza kwa Chelsea kufanya kitu cha ajabu kwa kumpiga Benchi Nahodha wao John Terry na kumuingiza Kurt Zouma nah ii ni mara ya kwanza kwa Jose Mourinho kuwahi kumpumzisha Nahodha wake kwa staili hiyo.
Kepteni wa Man City, Vincent Kompany aliipa Timu yake Bao la Pili katika Dakika ya 79 kwa kichwa baada ya kuunganisha Kona ya David Silva. Akipata matibabu kutoka kwa daktari wa timu
Diego CostaDiego Costa chini!Dakika ya 84, City wakawa 3-0 mbele kwa Bao la Fernandinho aliefunga kwa shuti kutoka nje tu ya boksi.
Vincent Kompany dakika ya 79 na Fernandinho dakika ya 85Hatari tupu!! 1-0Sergio Agüero dakika ya 31aliipatia bao la kuongoza na mtanange kwenda mapumziko ukiwa 1-0 dhidi ya Chelsea.2-0 Kompany akiwachoma bao ChelseaVicent Kompany akishangilia bao lake la piliBao la pili kwa Kompany msimu huu mpya Ligi Kuu England3-0

waliotembelea blog