Monday, August 17, 2015


YANGA SC imesema kwamba imemsainisha Mkataba wa miaka miwili beki wa kati wa kimataifa wa Togo, Vincent Bossou baada ya kufaulu majaribio.
Bossou amefanyiwa majaribio kwa wiki moja katika kambi ya Tukuyu Mbeya, ikiwemo kucheza kwa dakika 45 mchezo wa kirafiki dhidi ya Mbeya City jana Uwanja wa Sokoine, Mbeya.
Katika mchezo huo ambao Yanga SC ilishinda 3-2, Bossou aliondoka uwanjani Yanga SC ikiwa imefungwa bao moja na ikaongezwa la pili kipindi cha pili baada ya kuingia Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’.
Mkuu wa Idara ya Habari na Mawasiliano ya Yanga SC, Jerry Muro amesema kwamba uongozi umemsaini Bossou, baada ya kupitishwa na kocha Mkuu wa timu hiyo, Mholanzi, Hans van der Pluijm- Bossou.
Yanga SC imesema imemsainisha Mkataba wa miaka miwili Vincent Bossou (kulia)

Bossou aliyezaliwa Februari 7, mwaka 1986 mjini Kara, Togo, aliibukia klabu ya Maranatha FC ya kwao, kabla ya kusaini Etoile du Sahel ya Tunisia Januari 15, mwaka 2010 Mkataba wa miaka miwili.
Hata hivyo, Mkataba wa 'sentahafu' huyo Etoile Sportive du Sahel ulivunjwa baada ya miezi mitatu tu naye akarejea Maranatha FC Machi 18, mwaka 2010.
Mei mwaka 2011 akaenda kusaini klabu ya Navibank Saigon FC ya Vietnam, kabla ya kuhamia Becamex Binh Duong, baadaye TDC Binh Duongzote mwaka 2013, An Giang mwaka 2014 na Goyang Hi FC mwaka jana.
Alikuwepo kwenye kikosi cha timu ya taifa ya Togo kilichojitoa AFCON ya mwaka 2010 Angola baada ya basi la wachezaji kushambuliwa na majeshi ya waasi ikiwa njiani kuelekea kwenye fainali hizo.
Bossou, ambaye ameendelea kuwa mchezaji wa Togo hadi mwaka huu, aliwahi ‘kumvimbia’ Nahodha wa zamani wa Ivory Coast, Didier Drogba wakati wa mechi ya Kombe la Mataifa ya Afrika baina ya Ivory Coast na Togo Uwanja wa Royal Bafokeng Januari 22, 2012 mjini Rustenburg, Afrika Kusini.
Nadir Haroub 'Cannavaro' sasa anaweza kupoteza namba kikosi cha kwanza Yanga SC baada ya kusajlliwa beki wa Togo


Kevin Yondan akimtoka kiungo wa Azam FC, Salum Abubakar 'Sure Boy'. Beki huyo sasa anatakiwa kuongeza bidii ili kuinusuru nafasi yake kikosi cha kwanza Jangwani

Bossou anaungana na mabeki wengine wa 
kati Yanga SC, wazawa watupu, Rajab Zahir, Pato Ngonyani, Kevin Yondan na Nahodha Nadir Haroub ‘Cannavaro’, wakati pia kiungo Mbuyu Twite raia wa DRC anaweza kucheza katikati.

0 maoni:

Post a Comment

waliotembelea blog