Saturday, October 4, 2014


Akiandika katika ukurasa wake maalumu katika gazeti la EVENING STANDARD la huko nchini Uingereza kocha mkuu wa klabu ya wagonga nyungo wa London, West Ham United, Sam Allardyce amesema alisikitishishwa sana na kitendo cha kocha mpya wa klabu ya Manchester United Louis Van Gaal cha kutompatia kinywaji (mvinyu) baada ya mechi kama alivyokuwa akifanya Sir Alex Ferguson 
Louis van Gaal greets Sam Allardyce (R) before the game, but there was no meeting afterwards
Kulia ni kocha mkuu wa West Ham akipongezana na kocha wa Man U Van Gaaal baada ya mechi yao ya Jumamosi iliyopita, Sep 28, 2014
Allardyce alisema enzi za kibabu Fergie mambo yalikuwa burudani Old Trafford kwani kibabu alikuwa akitenga muda mfupi wa kuteta na kocha wa timu pinzani baada ya mechi huku wa wakipata kinywaji.
"Baada ya mechi kama nilivyozoea nilielekea katika chumba ambacho Ferguson zamani alikuwa akipenda kukutana na makocha wa timu pinzani  kupata kinywaji baada ya mechi kwa  siku husika huku wakibadilishana mawazo, lakini nilishangaa sana kuambiwa ule utaratibu haupo tena, kiukweli nilitoka na aibu kubwa ukizingatia nimefungwa magoli 2-1 siku hiyo!" Allardyce alisema.
Baada ya kupoteza mchezo huo dhidi ya Man U wikiendi iliyopita, West Ham sasa wako katika nafasi ya 13 katika msimamo wa ligi kuu Uingereza huku Mashetani Wekundu wakiendelea kuienzi mtaa wa saba (nafasai ya saba)  ambayo ndiyo ilikuwa nafasi yao mpaka ligi ya msimu wa 2013/2014 inamalizika

Tuesday, September 30, 2014


Paris St-Germain watatinga Mechi hii ya Nyumbani kwao ya Kundi F dhidi ya FC Barcelona bila ya Straika wao mahiri Zlatan Ibrahimovic ambae ameumia kifundo cha Mguu.
Katika Mechi za kwanza za Kundi lao, PSG ilitoka Sare na Ajax na Barcelona kuichapa Apoel Nicosia Bao 1-0.

Wakati PSG hawajafungwa hata Mechi moja katika Mechi 9 Msimu huu, ingawa 6 kati yake ni suluhu, Barcelona wamekuwa hatari mno huku Mastraika wao Messi na Neymar wakicheka na nyavu kila mara na Juzi waliibamiza Granada 6-0 huku Neymar akipiga Hetitriki na Messi Bao 2.

Mechi hii inawakutanisha Mameneja wa Timu hizi mbili, Laurent Blanc wa PSG na Luis Enrique wa Barca, ambao waliwahi kucheza pamoja wakiwa Barcelona katika Msimu wa 1996/97 na kuiwezesha kutwaa Kombe la Washindi wa Ulaya, Copa del Rey na Spanish Super Cup.



RATIBA MECHI ZA LEO JUMANNE
Mechi zote kuanza Saa 21:45

Jumanne Septemba 30
KUNDI E
19:00 CSKA Moscow vs Bayern Munich
Manchester City vs Roma

KUNDI F
APOEL Nicosia vs Ajax
Paris St-Germain vs Barcelona

KUNDI G
FC Schalke 04 vs NK Maribor
Sporting Lisbon vs Chelsea

KUNDI H
BATE Borisovs vs Athletic Bilbao
Shakhtar Donetsk vs FC Porto


Dakika ya 15 Peter Crouch aliifungia bao la kwanza la kichwa na kuifanya Stoke City kuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Newcastle baada ya Victor Moses kutoa krosi safi kwa Crouch ambaye ameunga kwa kichwa hadi langoni mwa Newcastle.Kibarua mashakani kwa kocha Pardew! 
Mpaka mapumziko Stoke ndio ilikuwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Newcastle United.Ushindi wa kwanza wa Nyumbani kwa Stoke City msimu huu wakimtungua Newcastle, bao likifunhgwa na Peter Crouch kipindi cha kwanza dakika ya 15 kwa kichwa.
Kocha wa Newcastle Pardew akiwa kwenye Mawazo mazito kipindi cha pili na hapa akiwa nyuma ya bao 1-0 kwenye Uwanja wa Stoke City Britannia.VIKOSI:
Newcastle XI: Krul, Janmaat, Coloccini, Williamson, Dummett, Tiote, Colback, Sissoko, Cabella, Gouffran, Riviere
Stoke XI: Begovic, Bardsley, Shawcross, Wilson, Muniesa, Whelan, Nzonzi, Diouf, Adam, Moses, Crouch



Wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania (kutoka kushoto), Kema Mabango, Abdallah Gunda na Jackson Mmbando wakishiriki katika shindano la kukuna nazi wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Washindi wa shindano la kukuna nazi wakishow love. Kutoka
(kushoto), Mshindi wa Kwanza, Abdallah Gunda, Mshindi wa Pili, Jackson
Mmbando na Mshindi wa Tatu, Kema Mabango.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakiogelea wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Watoto wa wafanyakazi wa kampuni ya Airtel Tanzania wakishiriki katika michezo wakati wa Siku ya Wanafamilia ya Airtel, iliyofanyika katika viunga vya Fun City Kigamboni jijini Dar es salaam jana.

Wafanyakazi wa Airtel na familia zao wakijisevia maakuli.

Afisa Uhusiano na Matukio wa Airtel, Dangio Kaniki (kulia) akiwahudumia chakula wafanyakazi wa Airtel na familia zao.
Airtel Family day yalenga kuongeza hamasa kwa wafanyakazi kujituma katika kazi zao Imeelezwa kuwa ufanisi wa watumishi katika ngazi mbali mbali za kiutendaji unaweza ukaongezeka pindi wafanyakazi wanapokutana pamoja na kubadilishana mawazo na viongozi wao katika hali ya kiurafiki.

Wednesday, September 24, 2014

Edu Albácar ndie aliyeanza kuifunga Real bao dakika ya 15 bao la mkwaju wa penati.
Gareth Bale hakuchukua muda dakikia 20 alisawazisha bao la hilo kwa kichwa na kufanya 1-1.
Cristiano Ronaldo alifunga bao la pili dakika ya 28 na kufanya 2-1 na baadae dakika ya 32 akaifungia bao tatu na kufanya 3-1 dhidi ya Elche kwenye Uwanja wa Nyumbani Bernabeu na ukishuhudiwa na Mashabiki 65,000.
Bao zote tatu zikifungwa katika kipindi cha kwanza cha dakika 45.
Kipindi cha pili dakika ya 80 Cristiano Ronaldo alifunga hat-rick kwa kufunga bao la nne na kufanya bao kuwa 4-1 dhidi ya Elche.

Ronaldo tena katika dakika za majeruhi alitupia bao lingine la tano na kuhitimisha mpira huo Real wakiwa na bao 5-1 dhidi ya Elche baada ya Ronaldo kupata pasi kutoka kwa Gareth Bale.


Fowadi wa Elce  Edu Albscar akishangilia bao lake la mkwaju wa penati

Bale aliweka sawa mambo kwa kufanya 1-1 nyumbani Bernabeu

Ronaldo akaipachikia bao la pili na kufanya 2-1

Ronaldo akishangilia bao lake la kuhitimisha Hat-trick yake leo hii usiku 
Ronaldo akifunga moja ya bao lake leo hii kwa kichwa

Ronaldo akishangilia bao lake

Sergio Ramos kwenye patashika!

Baadhi ya Wachezaji wa Real wakimpongeza mwenzao Staa Ronaldo


Wachezaji wa Southampton wakipongezana baada ya kuifunga bao la pili Arsenal kwenye Uwanja wao wa Emirates, Bao lililofungwa na Nathaniel Clyne dakika ya 40 kipindi cha kwanza.Nathaniel Clyne akifunga bao la pili.2-1Kipindi cha Kwanza dakika ya 14 Alexis Sánchez aliwapatia bao la kwanza Arsenal kwa frii kiki na kufanya bao kuwa1-0 dhidi ya Southampton.

Dakika ya 20 Dusan Tadic aliisawazishia bao Southampton kwa mkwaju wa penati na kufanya 1-1. Dakika ya 40 Nathaniel Clyne aliongeza bao la pili kwa shuti kali na kufanya 2-1 dhidi ya wenyeji Arsenal.Southampton wameenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 2-1 dhidi ya Arsenal.

MATOKEO TIMU NYINGINE:
Arsenal 1 v 2 Southampton
Cardiff 0 v 3 Bournemouth
Derby 2 v 0 Reading
Leyton Orient 0 v 1 Sheffield United
Liverpool 2 v 1 Middlesbrough
MK Dons 2 v 0 Bradford
Shrewsbury 1 v 0 Norwich
Sunderland 1 v 2 Stoke
Swansea 3 v 0 Everton 

Fulham 2 v 1 Doncaster

Tuesday, September 23, 2014



Warembo 15 kati ya 30 wanaoshiriki shindano la Redds Miss Tanzania 2014 wakisindikizwa na mkali wa Bongo Fleva kutoka Jijini Dar es Salaam, Tunda Man, wametoa burudani kali wakati wa shindano dogo la awali la kumtafuta mrembo mwenye kipaji lililofanyika Babati Mkoani Manyara. Pichani juu ni washindi wa tano waliofanikiwa kuingia fainali ya shindano hilo la vipaji litakalofanyika jijini Dar es Salaam baada ya wengine 15 kufanyika Arusha mjini.


Warembo hao walishindana vikali katika kucheza na kuimba miziki ya aina mbalimbali.

Jopo la majaji likifuatilia kwa makini shindano hilo



Kila aina ya stile za uchezaji zilioneshwa na warembo hao jukwaani...

Warembo wenzao waliobakia wakishangilia burudani ya vipaji kutoka kwa washiriki wenzao.

wadau wa sanaa ya Urembo Babati wakifuatilia shindano hilo.

Mkuu wa Wilaya ya Hanang, Christina Mndeme aliye mwakilisha Mkuu wa Mkoa wa Manyara, akiwa na waratibu wa show hiyo, Mzee Ally Sumaye (kushoto) na Mfanyabiashara Mohamad Bajwa.

Msanii wa Bongo Fleva Tunda Man akitoa burudani kwa wadau wa urembo Babati.


Tunda Man aliburudisha vilivyo ukumbini hapo.

Ilikuwa ni shwangwe kwa warembo hao ambao wapo Mikoa yua Kaskazini kwa ziara ya kimafunzo katika hifadhi za Taifa.

waliotembelea blog