Friday, July 4, 2014

MESSI-ARGENTINA2014DIEGO ARMANDO MARADONA, Lejendari wa Argentina, amesema Nchi yao inacheza chini ya kiwango, wanamtegemea sana Lionel Messi na lazima waongeze juhudi ikiwa watataka kuifunga Belgium kwenye Robo Fainali ya Kombe la Dunia ambayo watakutana Jumamosi Usiku.
Maradona amesema: “Bado hatujaanza! Lazima watambue wazi, waweke vichwani mwao, si kumtegemea Messi tu. Labda anaweza kufunga Bao safi…lakini kama hakuweza, wasimrukie Kijana huyu na kumfanya ndie mwenye hatia ya maafa ya Argentina!”
Maradona, ambae ndie alikuwa Kocha wa Argentina kwenye Fainali za Kombe la Dunia za Mwaka 2010 huko Afrika Kusini walikotolewa Robo fainali, alikuwa akihojiwa na TV ya Venezuela mara baada ya Argentina kuitoa kwa mbinde Switzerland kwa Bao 1-0 la mwishoni la Dakika za Nyongeza 30 lililofungwa na Angel Di Maria baada kazi njema ya Messi.
Akizungumzia Mechi hiyo, Maradona alisema: “Mtu kwa Mtu, na kwa pamoja, Argentina walikuwa bora, Wao [Uswisi] wanatengeneza Saa nzuri sana lakini wana Wanasoka wachache.”
Huko Brazil, Argentina wameshinda Mechi zao zote 4 hadi sasa na kufunga Bao 7 huku Messi akifunga Bao 4 kati ya hizo lakini ushindi wote huo ulikuwa wa tofauti ya Bao 1 tu.
Katika Mechi zote hizo 4, Messi ndie alieibuka na Tuzo ya Mchezaji Bora wa kila Mechi.
Maradona aliongeza “Huyu Kijana [Messi] yuko mpweke..Timu haibadilishi kasi yake, Mastraika hawazunguki. Nasikia uchungu, hasira, fedheha, kwa sababu Argentina inaweza kucheza vizuri zaidi, tena zaidi…Kocha lazima alazimishe hili! Kama hawataongeza ubora dhidi ya Belgium, basi tuko mashakani! ”
Argentina wameshatwaa Kombe la Dunia mara mbili na wakitwaa kwa mara ya 3, tena nyumbani kwa Mahasimu wao Wakuu Brazil, hiyo itakuwa starehe kubwa kwa Mashabiki wa Argentina ambao Maelfu yao wamefurika Brazil kushangilia Timu yao.

RAIS mpya wa Klabu ya Simba, Evans Aveva, ameanza kazi yake rasmi kwa kuteua Kamati mbalimbali za Klabu hiyo na pia kusimamisha Wanachama 69 waliofungua Kesi Mahakamani.
Aveva alitinga madarakani Simba baada ya kushinda Uchaguzi Mkuu uliofanyika Jumapili iliyopita Jijini Dar es Salaam kwa kuzoa Kura 1455 na kumshinda Andrew Tupa aliepata Kura 388.
Makamu wa Rais alichaguliwa Geoffrey Nyange ‘Kaburu’ aliepata Kura 1046 na kuwabwaga Jamhuri Kihwelo ‘Julio’ aliepata Kura 412, Swedi Nkwabi, Kura 373 na Bundala Kabula. 25.
Wajumbe wa Kamati Kuu waliochaguliwa kwenye Uchaguzi huo ni Idd Kajuna, Said Tully, Collins Frich, Ally Suru na Mwanamama Jasmine Badour.

Mbali ya Wajumbe hao, Rais Aveva, akitumia mamlaka yake Kikatiba, ameteua Watu watatu kuingia kwenye Kamati Kuu ambao ni Mohammed Nassor, Musleh Al Ruwaih na Salim Abdallah.
Kikao cha kwanza kabisa cha Kamati Kuu kiliamua kuwasimamisha Wanachama 69 ambao waliwasilisha Kesi Mahakamani kutaka kusimamisha Uchaguzi Mkuu na uamuzi wa hatima yao pamoja na ya Michael Wambura, aliezuiwa kugombea kwenye Uchaguzi, utatolewa na Mkutano Mkuu wa Simba utakaofanyika Agosti 3.



KAMATI ALIZOTEUA RAIS AVEVA:
KAMATI YA USAJILI

-Zacharia Hans Pope

- Mwenyekiti
-Kassim Dewji
-Dr Rodney Chiduo
-Musleh Al Ruwaih
-Crescentius Magori
-Said Tully

KAMATI YA VIJANA
-Said Tully - Mwenyekiti
-Ally Suru
-Patrick Rweyemamu
-Mulamu Nghambi
-Amina Poyo
-Madaraka Suleiman

KAMATI YA MASHINDANO

-Mohammed Nassor 

– Mwenyekiti
-Iddi Kajuna
-Jerry Yambi
-Hussein Simba

 -Mohammed Omar


 Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli (kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa kumtambulisha Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo. Pembeni ni Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli na Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier (katikati) ambaye yuko nchini Tanzania kwa ziara maalum ya kimichezo akifafanua machache mbele ya waandishi wa habari mara baada ya kutambulishwa. Pembeni yake kulia ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Mohn's John Ntuli, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi na Msimamizi wa shughuli hiyo Sam Odera.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha staili mbali mbali za kucheza mpira mbele ya waandishi wa habari.
 Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana huku ukiwa unacheza mziki staili mbali mbali.
  Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa Sean Garnier akionyesha jinsi ambavyo unaweza kupiga danadana na kupita katika tundu dogo huku ukiendelea na mchezo. Picha zote na Cathbert Kajuna wa Kajunason Blog.
Na Mwandishi Wetu, Dar es Salaam.
Mwanamichezo kutoka nchini Ufaransa leo anatarajiwa kuonyesha shoo ya bure ambapo ataonesha umahiri wa kucheza mpira wa mitaani, sarakasi na kucheza dansi.
Mfaransa huyo Sean Garnier ambaye yuko nchini kwa ziara maalum ya kimichezo jana usiku alianza ziara hiyo kwa kuonesha umahiri wake wa kucheza mpira wa mtaani katika viwanja vya ufukwe wa Coco (Coco Beach) jijini Dar es Salaam.
Garnier ambaye anakipaji cha kupiga danadana mpira huku akiweka mapozi mbalimbali alionekana kuwa kivutio mbele ya mkutano na waandishi wa habari ambao walikuwepo kwenye mkutano huo huku akionesha umahiri wake wa kupiga danadana na kucheza na mpira katika barabara ya Alli Hassan Mwinyi baada ya mkutano huo.
Mwenyeji wa ziara ya Garnier, Mkurugenzi wa Masoko Kampuni ya Mohan’s Vijay Joshi alisema kwamba huyu ni mwanamichezo mwenye kushikilia taji la kipaji cha kucheza ‘Free Style’ duniani.
“Ameletwa kwa udhamini wa ‘Redbull Street Sytle’ na atakuwa nchini kwa siku tano ambapo ni kati ya Julai 2 hadi Julai 7 ataondoka.
Aidha mbali ya kumudu kucheza na mpira pia nacheza sarakasi katika mitindo mbalimbali huku akiwataka watanzania kuiga baadhi ya michezo ambayo ataionyesha akiwa atakapokuwa mtaani.
Baadhi ya mitaa atakayo pita ni Kariakoo, Mlimani City, Posta, Viwanja vua Sabasaba, Chuo Cha Biashara (CBE) na Sea Clif Jijini Dar es Salaam.

Thursday, July 3, 2014

JUMATANO Klabu za Liverpool na Barcelona zilifanya mazungumzo kuhusu Uhamisho wa Luis Suarez ambae kwa sasa yuko kwenye Kifungo cha Miezi Minne alichopewa na FIFA kwa kumuuma Meno Beki wa Italy Giorgio Chiellini wakati wa Mechi ya Kombe la Dunia kati ya Uruguay na Italy huko Brazil.
Mtendaji Mkuu wa Liverpool, Ian Ayre, alikutana na Maafisa kutoka Barcelona na mazungumzo zaidi yamepangwa.

Huku pande zote zikitarajia kukamilika majadiliano yao haraka, inaaminika Dau la kumuuza Suarez kutoka Liverpool kwenda Barcelona huenda likagonga Pauni Milioni 70 kwani Liverpool wanataka Pauni Milioni 80 na Barca wanadaiwa kukubali Pauni Milioni 60.
Chanzo kutoka Anfield kilikaririwa kikisema: “Mazungumzo yalikuwa mazuri yenye mafanikio na kila upande ulifikia matarajio yake. Mazungumzo zaidi yatafanyika. Kwa sasa hakuna kilichokubaliwa.”
Inaaminika Barca wako tayari kumtoa Winga wao kutoka Chile, Alexis Sanchez, kwa Liverpool kwenye Dili ya kumchukua Suarez lakini pia mazungumzo hayo ya Jana yaligusia kutoka Dau lote bila kuweka Mchezaji juu.
Lakini, hata kama Barca watamnunua Suarez, Mchezaji huyo haruhusiwi kufanya nao Mazoezi na hata kukanyaga Uwanjani kama Mtazamaji hadi baada ya Oktoba 26 atakapomaliza Kifungo chake cha Miezi Minne kilichoanza Juni 26.

Pamoja na Kifungo hicho, Suarez pia amefungiwa kucheza Mechi 9 za Nchi yake Uruguay na pia kutwangwa Faini Dola 111,000.
Baada ya kukanusha kumuuma Chiellini, Juzi Suarez alimwomba radhi Mchezaji huyo wa Italy pamoja na Ulimwengu wa Soka kitu ambacho kilikubaliwa na Chiellini na Barca kukiita ni ‘unyenyekevu.’

Sunday, June 22, 2014


Xabi Alonso, Kiungo wa Real Madrid, ametangaza kustaafu kuichezea Nchi yake Spain.
Alonso, Miaka 32, amekuwa mmoja wa kiini cha mafaniko ya Spain iliyotwaa EURO 2008 na EURO 2012 pamoja na Kombe la Dunia huko Afrika Kusini Mwaka 2010.
Juzi Alonso aliichezea Spain Mechi yake ya 112 ilipofungwa 2-0 na Chile kwenye Mechi Kundi B na kutupwa nje ya Fainali za Kombe la Dunia huko Brazil.

Kwenye Mechi hiyo, Alonso alibadilishwa wakati wa Mapumziko baada kupwaya na kupokonywa Mpira uliozaa Bao la Kwanza la Chile.
Lakini Alonso ndie Mchezaji pekee aliewafungia Spain Bao pekee kwenye Mashindano haya huko Brazil alipofunga kwa Penati kwenye Mechi ya Kwanza ya Kundi B waliponyukwa Bao 5-1 na Netherlands.

Mara baada ya Spain kutupwa nje ya Fainali ya Kombe la Dunia, Alonso alisema: “Vitu vinabadilika. Zama zinaisha kwa kufungwa…na hiki kilikuwa kipigo kichungu. Hatukutegemea lakini ndio mchezo. Hivi vitu vinatokea. Hatukutegemea lakini ni lazima tuyakabili majonzi yetu vile vile kama tunavyofurahia, kama Wanaume.”

Aliongeza: “Tumecheza dhidi ya Timu zilizojitayarisha vyema na sasa tunarudi nyumbani. Inauma lakini huu ndio mpira. Kama nilivyosema, tulijua namna ya kushinda, sasa inabidi tujue namna ya kushindwa!”

Mbali ya Alonso kutangaza kustaafu pia kuna wasiwasi kuwa Kiungo Xavi na Kipa Iker Casillas, ambao wote wamecheza ovyo huko Brazil, wanaweza kufuata nyayo zake.
Zipo habari kuwa Kocha wa Spain, Vicente del Bosque, hasa kwa vile Shirikisho la Soccer la Spain, RFEF, linaunga mkono aendelee na kazi yake.


KUHUSU REKODI YA XABI ALONSO
BORN: Tolosa, Spain, November 25, 1981

1999-2000: Real Sociedad B (39 apps, 2 gls)
1999-2004: Real Sociedad (114 apps, 9 gls)
2000-2001: Eibar (loan) (14 apps, 0 gls)
2004-2009: Liverpool (143 apps, 15 gls)
2009-NOW: Real Madrid (158 apps, 4 gls)



2003-NOW: Spain (112 caps, 16 gls)
CLUB HONOURS:

LIVERPOOL - FA Cup (2006), FA Community Shield (2006), Champions League (2005), UEFA Super Cup (2005)
REAL MADRID - La Liga (2012), Copa del Rey (2011, 2014), Supercopa de Espana (2012), Champions League (2014)
SPAIN - World Cup (2010), European Championship (2008, 2012)

WORLD CUP 2014: NIGERIA 1 vs BOSNIA-HERZEGOVINA 0, PETER ODEMWINGIE AWAPATIA USHINDI NIGERIA..

1-0, Peter Odemwingie kushoto akishangilia bao lake lililotosha kuwapatia alama 3 muhimu na kuwawezesha kuwa na jumala ya pointi 4 na wako nafasi ya pili kwenye kundi lao na mtanange ujao kwa Nigeria ni jumatano tarehe 25 saa moja kamili.Peter Odemwingie dakika ya 29 aliifungia bao timu yake baada ya kazi nzuri ya Emenike kwa kuwakacha mabeki wa Bosnia na kumpa pasi Odemwingie na kufunga bao huku wachezaji wa Bosnia wakishindwa kuamini bao hilo.
Mchezaji wa Bosnia midfielder Izet Hajrovic akipitwa na mchezaji wa Nigeria difenda Juwon Oshaniwa na kwenda eneo la hatari la kipa na kugawa pasi kwa Peter Odemwingie

Friday, June 20, 2014


Warembo wanaowania taji la mkoa wa Tanga, Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakijiaandaa kufanya usafi katika ofisi ya Mkuu wa Mkoa wa Tanga, ikiwa ni moja ya kampeni ya kuendelea kulifanya jiji hilo liwe safi muda wote. Washiriki wa Nice & Lovely Miss Tanga 2014 wakitupa takataka katika gari maalum la kubeba taka. Mshindi wa kwanza katika shindano hilo atapata zawadi ya gari dogo aina ya Toyota Vitz. Zoezi la usafi limepamba moto na kuliacha eneo hilo safi kabisa. Mgeni rasmi katika shindano hilo atakuwa Mkuu wa Mkoa wa Tanga, Mheshimiwa Chiki Gallawa.

waliotembelea blog