Saturday, April 19, 2014


Wakristo duniani kote wanajiandaa kusherehekea Sikukuu ya Pasaka. Ingawa si madhehebu yote ya Kikristo yanayosheherehea kwa uzito sawa, katika kalenda ya Kanisa Katoliki, Pasaka ni furaha ya kusherehekea kufufuka kwa Yesu.
Ijumaa Kuu
Ijumaa Kuu ni siku ambayo wakristo wanaadhimisha kufa, kuzikwa kwa Yesu, tukio lililotokea katika mji wa Yerusalemu siku ya Ijumaa.
Kulingana na Mtume Yohane, kesho yake, yaani baada ya Ijumaa, ilikuwa Sabato na ikafuatia na Pasaka yenyewe siku ya Jumapili. Ijumaa Kuu ni sehemu ya Juma Kuu linaloanza kwa adhimisho la Yesu kuingia mji huo wa Yerusalemu akishangiliwa kama mfalme wa Wayahudi. Ijumaa Kuu pia ni sehemu ya siku tatu kuu za Pasaka zinazoadhimisha mateso na kifo chake, kuzikwa kaburini, na hatimaye kufufuka.
Umuhimu wa Pasaka
Pasaka ni moja ya sikukuu kubwa sana kwa Wakristo. Pamoja na kuwa imeendelea kuchukuliwa kama tukio la kihistoria tu, bado dhana yake ya kuonyesha upendo wa Mungu kwa wanadamu haitapotea. Ni upendo wa kutoa moja ya nafsi za Mungu, iteswe, isulubiwe, ife na kisha ifufuke kudhihirisha utukufu wa Mungu na upendo wake kwa wanadamu.
Lakini kwa sisi wanadamu wa leo Pasaka ni nini?
Kuna umuhimu gani wa kuendelea kukumbuka Sikukuu ya Pasaka? Ni mafundisho gani tunayoyapata juu ya siku hii? Pasaka ni sikukuu ya kufufuka kwa Yesu Kristo na ni sikukuu muhimu kwa Wakristo, watu huenda kanisani na kusherekea sikukuu hii ya kidini.
Wakristo pote ulimwenguni husherekea Pasaka kwa furaha kubwa sana kwa sababu wanaiona ndio siku ambayo mwokozi wao huwa amefufuka. Watu wengi huvalia nguo mpya kwenda kanisani siku ya Pasaka.
Kuna alama nyingi zinazotambulisha siku ya Pasaka, moja ni msalaba ambao Wakristo, huuona kama alama ya ushindi wa Kristo dhidi ya kifo. Msalaba mara nyingi hutokea kama alama ya Pasaka. Watu katika sehemu nyingi ya ulimwengu huoka keki maalumu ziitwazo 'mikate ya moto ya msalaba'.
Mishumaa 
Taa, mishumaa na moto mkubwa wa sherehe inatoa ishara ya kusherekea kwa Pasaka katika baadhi ya nchi.
Wakatoliki katika baadhi ya nchi huzima taa zote katika makanisa yao siku ya Ijumaa kuu. Jioni ya siku inayotangulia Pasaka, hutengeneza moto mpya kuwashia mshumaa mkubwa wa Pasaka kuashiria siku na mambo mapya ndani ya ufufuo mpya wa Yesu.
Hutumia mshumaa huu kuwashia mishumaa mingine yote kanisani. Halafu huwasha mishumaa yao nyumbani ili itumike katika nyakati za sherehe maalumu.
Katika sehemu za Ulaya Kaskazini na Kati,watu huchoma moto mkubwa wa sherehe katika vilele vya milima. Halafu hujikusanya kuzunguka huo moto mkubwa na kuimba nyimbo na mashairi ya Pasaka.
Mwanzo wa Pasaka
Wakristo hufanya ibada ya siku 40; kipindi cha mfungo na sala hujulikana kama Kwaresma.Inakumbusha siku 40 za Kristo kufunga na kwenda jangwani.
Wiki ya mwisho ya Kwaresma iitwayo wiki takatifu hutukuza matukio ya wiki ya mwisho wa maisha ya Yesu Kristo kuwepo duniani, na inaanza katika Jumapili ya Matawi. Imetajwa hivyo kwa sababu ya matawi ambayo watu waliyatawanya kabla Yesu kristo hajaingia Yerusalemu kwa kushangiliwa
kwa shangwe kubwa.
Katika Alhamisi ya wiki ya mwisho ya Kwaresma kabla ya Ijumaa Kuu, Wakristo hukumbuka chakula cha mwisho cha Yesu Kristo cha jioni wakati walipoosha nyayo za miguu yao.
Waliiona Ijumaa Kuu ya kusulubiwa kwa Yesu kristo katika namna au njia ya huzuni na majonzi na kutumia Jumamosi takatifu katika fikra ya mambo yatakayotokea mbeleni katika Jumapili ya Pasaka. 

Saturday, March 22, 2014


Wataalamu wanaendelea na juhudi za kuchunguza iliko ndege ya Malaysia
China imeanza kuchunguza picha mpya za setilite zinazoonyesha kitu kama mabaki ya ndege kwenye eneo la kusini mwa bahari ya Hindi.
Picha hizo ni muhimu kwa ndege ya Malaysia MH370 iliyopotea, maafisa wa Malaysia wanasema.
Kaimu Waziri wa Usafirishaji Hishammuddin Hussein amesoma taarifa hiyo baada ya kukabidhiwa ambapo amesema kuna kitu kama mabaki ya ndege chenye ukubwa wa mita 30 kwa 22 kilichoonekana.
Amesema serikali ya China itaendelea kutoa taarifa zaidi hapo baadae.
Ndege MH370 mali ya Shirika la ndege la Malaysia ilipotea kwenye masiliano ilipokuwa imeondoka kutoka Kuala Lumpur kwenda Beijing march 8 ikiwa na abiria 239.


Respected: Ferguson poses with Nesbitt and Vice-Chancellor Professor Richard Barnett on Thursday
Sir Alex Ferguson (katikati) akiwa amesimama na viongozi wa chuo cha Ulster Ireland baada ya kupewa degree ya heshima kutokana na mchango mkubwa aliyoutoa kwenye soka hususani Man utd. Katika maneno yake mbele ya wanachuo 500 Sir Alex alisema ' Najivunia kupokea degree hii ya heshima kutoka kwenye chuo kikubwa kama hiki. Ninayo furaha sana kuona hata chuo kimeona mchango wangu na kufikiria kunipa tuzo. Hii ni ishara tosha kuwa mafanikio yangu katika soka yatawahamasisha pia wanachuo ambao wana ndoto ya kutimiza mambo makubwa kwenye maisha yao kwa kudumisha yale niliyokuwa nayaamini kama chachu ya mafanikio ambayo ni bidii na tabia njema'.
Proud moment: Sir Alex Ferguson has received an honorary degree for his outstanding contribution to football Proud moment: Sir Alex Ferguson has received an honorary degree for his outstanding contribution to footballSpeech: Ferguson speaks to students after receiving his honorary degree from the University of Ulster


Unhappy ending: Robin van Persie was carried off on a stretcher after scoring three against Olympiacos
Matokeo ya vipimo vya majeraha aliyoyapata Van Persie kwenye mechi dhidi ya Olympiacos yameonesha mchezaji huyu atakuwa kwenye matibabu kwa wiki sita. Majibu ya vipimo hivi yamekuwa tofauti ya fikra za wengi akiwemo kocha Moyes waliofikiri RVP amepata majeraha madogo. Kutokana na majeraha haya RVP ataweza kukosa mechi zifuatazo;

Mar 23: West Ham (A)
Mar 25: Man City (H)
Mar 29: Aston Villa (H)
Apr 1: Bayern Munich (H)
Apr 5: Newcastle (A)
Apr 9: Bayern Munich (A)
Apr 20: Everton (A)
Apr 26: Norwich (H)


Ronaldo, Pepe na wapenzi wao wakiangalia mechi ya basketball kati ya Real Madrid na CSKA Moscow
Keen eye: Cristiano Ronaldo and model girlfriend Irina Shayk watched Real Madrid's basketball teamPepe was also in the capital Cristiano Ronaldo and Irina Shayk
Game for a laugh: Pepe (right) shares a joke with Ronaldo and Irina during a break in play
The look of love: Ronaldo and Irina Shayk Interested? The Russian super model takes her eyes off the action
Pretty in pink: Arsenal stars are focused on the pool table
Alex Oxlade-Chamberlain, Keiran Gibbs na  Aaron Ramsey wakicheza pool.

No diggity: Rio Ferdinand posted a video of him singing along to Blackstreet's 'No Diggity'
Rio Ferdinand akiwa mwenye furaha huku akiimba ndani ya gari yake siku ya alhamisi asubuhi siku moja baada ya United kuipiga Olympiacos. 
Spectator: Ramsey was at Twickenham to see Wales beaten by England in the Six Nations
 Kiungo wa Arsenal, Aaron Ramsey akiwa uwanjani kuangalia mechi ya Ragbi wakati Wales ikiifunga England. 
All smiles: Pique poses with his partner Shakira at the launch of her self-titled new album in Barcelona
Pique akiwa na mke wake Shakira siku ya uzinduzi wa album ya kumi ya Shakira jijini Barcelona 
Barca star: Pique was happy tot take time away from his team's preparations for Sunday's El Clasico
Neymar relaxes in Disneyland Paris before the Clásico
Neymar na Silva wakiwa Disneyland jijini Paris wiki hii.  

Standing tall: Brazilian team-mates Thiago Silva (left) and Neymar (right) pose with The Invincibles
Happy Father's Day, Messi!
Messi akitekeleza majukumu ya ubaba akiwa amembeba mtoto wake Thiago

Thursday, March 20, 2014

SAM_2237  
Hawa jamaa wanapokuja na njiwa au kuku uwanjani wanamaanisha nini?, au ndio mikwara kwa wapinzani?. Lakini njiwa hawa huwa hawaonekani pale timu inapofungwa.SAM_2239 SAM_2240Unaanzaje kumwambia shabiki kama huyu, mwenye mapenzi makubwa na klabu yake ahamie timu nyingine. Lakini wapo watu wanaendesha klabu watakavyo, wanasahau kuwa kuna uwepo wa watu wenye hisia kali kama huyu jamaa. 
Unamtesa sana unapoleta longolongo nyingi kwenye mambo ya msingi yahusuyo timu. Usishangae kumuona kazimia au kazirai kwasababu ya mtu mmoja kuharibu mambo.


KINYANG`ANYIRO cha ubingwa wa ligi kuu soka Tanzania bara msimu wa 2013/2014, bado kinabaki kuwa kitendawili kwa timu zilizopo juu katika msimamo.
Sare ya bao 1-1 jana uwanja wa Taifa jijini Dar es salaam baina ya vinara Azam fc dhidi ya Yanga imezidi kuweka mazingira magumu kwa mabingwa watetezi, Young African.
Katika mchezo huo  uliovuta hisia za mashabiki, Yanga walikuwa wa kwanza kufunga bao kipindi cha kwanza kupitia kwa Didier Kavumbagu, lakini Azam fc walisawazisha dakika za lala salama kupitia kwa kinda, Kevin Friday.
Hiyo ilikuwa mechi ya 19 kwa Yanga, wakati kwa Azam fc ilikuwa ya  20, huku wakijikusanyia pointi 44, wakati Wanajangwani wakivuna pointi 40 katika nafasi ya pili.
Yanga SC wamebakiza mechi 7, wakati Azam fc wamebakiza mitanange  6.
PICHA YA PG.24 
Mtatwaa Ubingwa? : Wachezaji wa Yanga wakishangilia bao la Didier Kavumbagu jana uwanja wa Taifa
Wikiendi hii timu zote zitashuka dimbani. Yanga watasafiri mpaka mkoani Tabora kuwafuata maafande wa Rhino Rangers, wakati jumapili machi 23, Azam fc watawakaribisha JKT Oljoro,  uwanja wa Azam Complex Chamazi.
Rhino Rangers ndio wanaoburuza mkia katika msimamo wakiwa wameshacheza mechi 21 na kujikusanyia pointi 13 tu kibindoni.
Kwa asilimia kubwa, maafande hawa wa Tabora, wameshachungulia kushuka daraja na inawezekana hakuna muujiza wa kubaki ligi kuu msimu huu kwasababu ya mazingira yao.
_DSC0044 
Mchezo dhidi ya Yanga utakuwa mkali endapo bado Rhino wanahitaji ushindi.
Lakini imani yao imeshuka na wanacheza bora liende na wameshapoteza matumanini ya kuendelea kucheza ligi kuu.
Pointi 13 kwa mechi 21 ni chache sana, zinahitajika nguvu za ziada kushinda mechi zote 5 walizobakiza, hapo sasa tunaweza kuzungumza mengine.
Yanga wataingia uwanjani wakiwa ma matokeo ya sare ya jana na suluhu ya Mtibwa Sugar wiki iliyopita uwanja wa Jamhuri.

waliotembelea blog