Saturday, February 8, 2014
3:15 AM
Unknown
Bw. Obama alikuwa akizungumza Alhamis
wakati wa dhifa ya kila mwaka ya maombi ya kitaifa jijini Washington,
ambako alisema yeyote anayemdhuru mwingine kwa kutumia imani ya dini
anadhulumu uhusiano wake mwenyewe na Mwenyezi Mungu.
Aliwasihi walioshiriki katika mamombi hayo kuwaombea wote waliokamatwa na kuzuiliwa kutokana na imani zao za kidini, akiwemo Kenneth Bae aliyezuiliwa Korea Kaskazini na Saeed Abedini aliyezuiliwa huko Iran.
Maombi ya kitaifa ya kila mwaka huandaliwa na wabunge wa Marekani katika majengo ya bunge. Na kila rais wa Marekani amehudhuria maombi hayo tangu yalipoanza mwaka wa 1953. Chanzo: voaswahili

3:11 AM
Unknown
Kocha David Moyes alikuwa tayari
kumbakiza Nahodha wake huyo Old Trafford, lakini Vidic, anayemaliza
Mkataba mwishoni mwa msimu, ameamua kuondoka baada ya kuitumikia
Manchester kwa miaka minane.
Mserbia huyo ameshinda mataji 15 tangu awasili klabu hiyo akitokea Spartak Moscow ya Urusi kwa ada ya uhamisho ya Pauni Milioni 7, Januari mwaka 2006, na baadayekuwa Nahodha chini ya kocha Sir Alex Ferguson.
Katika taarifa yake, Vidic amesema: "Ni mwaka wa mwisho wa Mkataba wangu na nimekuwa na miaka minane mizuri hapa. Chanzo: binzubeiry

3:10 AM
Unknown
Nafasi ya kikosi cha Arsene Wenger kumaliza ukame wa miaka minane bila ya taji itajulikana vizuri mwisho wa mwezi huu.
Wana mechi ya nyumbani ya Ligi Kuu dhidi ya Manchester United, na Kombe la FA dhidi ya Liverpool pamoja na mechi mbili za hatua ya 16 bora za Ligi ya Mabingwa dhidi ya Bayern Munich zitafutia baada ya mechi ya leo, na endapo watapoteza basi watakosa nafasi ya kutwaa moja ya mataji hayo matatu.
Arsenal wanaongoza ligi kwa tofauti ya pointi mbili kwa Manchester City, ambao wenyewe watacheza na Norwich City na Chelsea walio nafasi ya tatu watakuwa nyumbani kucheza dhidi ya Newcastle United na kipigo cha Gunners ndani ya Anfield kitawashusha hadi nafasi ya tatu.
Kama Liverpool watafungwa leo wataachwa nyuma kwa pointi 11 na vinara hao.
Wapinzani wa Liverpool katika kuwania nafasi ya nne, Tottenham Spurs, Everton na Manchester United watashuka uwanjani kesho.
Manchester United watakuwa na kibarua kizito mbele Fulham. Huku Spurs watawakaribisha Everton katika mechi za kusaka kucheza Ligi ya Mabingwa msimu ujao. Chanzo: mwananchi

3:09 AM
Unknown
Kamati ya Ufundi ya Marefa Hispania
(CTA) limemfungia kwa mwezi mmoja Miguel Angel Ayza Gamez na
hataruhusiwa kabisa kuchezesha mechi za Real msimu huu.
Kwa mujibu wa taarifa kutoka Hispania, kuna hatari zaidi akaondolewa kabisa katika orodha ya marefa wa La Liga kutokana na madudu aliyoyafanya katika mechi hiyo.
Ronaldo alitolewa nje kwa mara ya saba katika historia yake ya soka dakika ya 75 siku hiyo timu hizo zikifungana 1-1 Uwanja wa San Mames baada ya kumuinulia mkono Nahodha wa Bilbao, Carlos Gurpegi, ambaye alijiangusha.
Pia alimvaa kiungo wa Bilbao, Ander Iturraspe wakati akiwa na hasira za tukio hilo.
Inafahamika taarifa ya awali ya Ayza Gamez ilisema alimtoa nje Ronaldo kwa tulio alilolifanya kwa Gurpegi, lakini baadaye akabadilisha na kusema alimtoa nje kwa kosa la kumsukuma Iturraspe - maneno ambayo yalisemwa na mchezaji huyowa Bilbao. Chanzo: binzubeiry

3:07 AM
Unknown
Mnyika ambaye alikuwa akizungumza kama
Mjumbe wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira,
alitoa mapendekezo hayo juzi baada ya kutembelea Hifadhi ya Tarangire.
"Tatizo hili (la ujangili) ni kubwa ni vizuri Tanzania ikaiga nchi nyingine duniani...Tupige marufuku kwanza kwa muda uwindaji wa tembo ili kuziba kabisa mianya na visingizio," alisisitiza Mnyika.
Mnyika amewaambia waandishi wa habari kuwa, kwa hali ilivyo sasa, wapo tembo wanaowindwa kwenye vitalu na hiyo inaleta mkanganyiko kati ya uwindaji haramu na uwindaji halali.
Halikadhalika Mnyika ametumia fursa hiyo kuitaka Serikali kuwataja na kuwashtaki kortini vigogo wa ujangili kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ya Operesheni Tokomeza Ujangili (OTU II).
"Kabla ya kuanza kwa awamu ya pili ni vizuri wale vigogo wa ujangili waliotajwa kwa ujangili wakatajwa kwa majina ili wachukuliwe hatua...Tunataka itakapoanza awamu ya pili isiwalenge tu wananchi," alisema Mnyika.
Mwenyekiti wa Kamati ya Kudumu ya Bunge ya Ardhi, Maliasili na Mazingira, James Lembeli alisema, wanyama kama Nyumbu wapo hatarini kutoweka kama hatua za makusudi hazitachukuliwa.
Amesema kutoweka kwa wanyama hao kutasababishwa na wimbi kubwa la kuzibwa kwa mapito ya wanyama (corridor) kati ya hifadhi na hifadhi na hivyo wanyama hao kushindwa kwenda kuzaliana.
"Hali hii ni hatari kwa maisha ya hifadhi zetu hasa hizi za kaskazini...Mfano wakati hii Tarangire inaanzishwa kulikuwa na Corridor (mapito) tisa, leo tunapozungumza zimebaki tatu tu,"alisema.
Lembeli amesema endapo ikitokea njia hizo zikazibwa kabisa, wanyama watajikuta wanabakia eneo moja na kushindwa kwenda maeneo ya kuzaliana, hivyo watazeeka na kufa bila kuongezeka. Chanzo: mwananchi

Subscribe to:
Posts (Atom)
RSS Feed
Twitter