Wednesday, January 8, 2014


Leo zipo Mechi nyingine kadhaa za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ikiwa pamoja na ile ya Mabingwa wa Spain Barcelona wakiwa kwao Nou Camp kucheza na Getafe huku Duniani ikitarajia kumuona Nyota Lionel Messi akirejea dimbani baada kuwa Majeruhi kwa Miezi miwili.
 
Valencia jana walifanikiwa kutoka Sare ya Bao 1-1 na Mabingwa Watetezi wa Copa del Rey Atletico Madrid katika Mechi ya Kwanza ya Raundi ya Mtoano ya Timu 16 iliyochezwa Nyumbani kwa Valencia.
Timu hizi zitarudiana hapo Januari 14 huko Vicente Calderon Nyumbani kwa Atletico Madrid.
Bao la Atletico lilifungwa na Raul Garcia katika Dakika ya 72 na Valencia kusawazisha kwenye Dakika ya 90 kwa Bao la Helga Postiga.
Leo zipo Mechi nyingine kadhaa za Kwanza za Raundi ya Mtoano ya Timu 16 ikiwa pamoja na ile ya Mabingwa wa Spain Barcelona wakiwa kwao Nou Camp kucheza na Getafe huku Duniani ikitarajia kumuona Nyota Lionel Messi akirejea dimbani baada kuwa Majeruhi kwa Miezi miwili.
 
 
VIKOSI:
Valencia: Guaita; Guardado, Mathieu, Costa, Pereira; Fuego, Parejo; Bernat (Canales 73'), Míchel (Feghouli 63'), Fede (Piatti 77'); Postiga.
Goals: Postiga (93').
Atlético Madrid: Courtois; Felipe Luis, Alderweireld, Miranda, Juanfran; García, Gabi, Guilavogui (Arda 59'), Koke (Tiago 81'); Diego Costa, Adrián (Rodríguez 67').
Goals: García (72').

COPA del REY
Raundi ya Mtoano ya Timu 16
RATIBA/MATOKEO:
Jumanne Januari 7
Valencia 1 v Atletico de Madrid 1
Jumatano Januari 8
22:00 Real Betis v Athletic de Bilbao
22:00 Alcorcon v RCD Espanyol
24:00 FC Barcelona v Getafe CF
24:00 Real Racing Santander v UD Almeria
Alhamisi Januari 9
21:30 Real Sociedad v Villarreal CF
23:30 Real Madrid CF v Osasuna
23:30 Rayo Vallecano v Levante
Jumanne Januari 14
21:30 UD Almeria v Real Racing Santander
23:30 Atletico de Madrid v Valencia
Jumatano Januari 15
21:30 Athletic de Bilbao v Real Betis
21:30 RCD Espanyol v Alcorcon
23:30 Osasuna v Real Madrid CF
23:30 Levante v Rayo Vallecano
Alhamisi Januari 16
22:00 Villarreal CF v Real Sociedad
24:00 Getafe CF v FC Barcelona


 
Dakika za nyongeza za kipindi cha kwanza 45+2 Giggs anafanya makosa anajifunga bao, Sunderland wanaenda mapumziko wakiwa mbele ya bao 1-0 dhidi ya Manchester United. Kipindi cha pili dakika ya 52 Nemanja Vidic anawasawazishia bao United kwa kufanya 1-1 baada ya kona kupigwa na Vidic kujituma kwa kufunga bao la kichwa. Dakika ya 65 United wanafungwa goli la pili kwa mkwaju wa penati wa utata na kufanya bao kuwa 2-1. mfungaji wa penati hiyo akiwa ni Fabio Borini. Ushindi huu wa Sunderland unawaweka pazuri wakija kurudiana huko Old Trafford mwezi huu  januari siku ya jumatano tarehe 22.
Up high: Nemanja Vidic powers his header past Vito Mannone to bring his side level
Nemanja Vidic akisawazisha bao na kufanya 1-1 hapa
 
 
 
 

Kocha wa Manchester United David Moyes akiwa amesimama kidete kuwaangalia vijana wake  
 
!. Subdued: Bryan Robson, Alex Ferguson and Bobby Charlton watch on in front of Anderson
 

N
 

 
 
Fabio Borini akichonga penati
 
 

VIKOSI:
Sunderland: Mannone, Bardsley, O'Shea, Brown, Alonso, Larsson, Cattermole, Ki, Borini, Fletcher (Altidore 72), Giaccherini (Johnson 56).
Subs: Gardner, Celustka, Colback, Ji, Dixon.

Booked: Bardsley, Giaccherini, Altidore.
Goal: Giggs, 45+2og, Borini 65pen
Man United: De Gea, Rafael Da Silva, Vidic, Evans (Smalling 61), Evra, Carrick, Cleverley (Fletcher 75), Valencia (Hernandez 87), Giggs, Januzaj, Welbeck.
Subs: Lindegaard, Kagawa, Buttner, Zaha.

Booked: Evra, Rafael, Smalling.
Goal: Vidic 52.
Referee: Andre Marriner


CAPITAL ONE CUP
NUSU FAINALI
[Saa 4 Dakika 45 Usiku]
Jumanne Januari 7

Sunderland 2 v Manchester United 1
Jumatano Januari 8
Manchester City v West Ham United
Marudiano
Jumanne Januari 21

West Ham United v Manchester City
Jumatano Januari 22
Manchester United v Sunderland

 HONGERA: Wakili wa CHADEMA Tundu Lisu (kulia) akilazimika kumpongeza aliyekuwa Naibu Katibu Mkuu wa CHADEMA, Zitto Kabwe baada ya Jaji wa Mahakama Kuu ya Tanzania Kanda ya Dar es Salaam, John Mkamwa, kuridhia zuio la Zitto asijadiliwe na ngazi yoyote ya maamuzi ya Chadema, hadi kesi ya msingi aliyofungua dhidi ya chama hicho itakapomalizika. Jaji huyo amekubali kesi ya msingi iungurume na itaanza kusikilizwa Februari 13, mwaka huu.
 Zitto akitoka kwa msaada wa mabaunsa wake katika chumba cha mahakama kuu baada ya uamuzi huo wa  Mahakama kuu leo jioni.
Tundu Lisu na wapambe wake wakionekana kutoka kwa aibu Mahakamani baada ya kubwagwa

 Tundulisu aklizungumza na waandishi nje ya mahakama
 Wakili wa Zitto akizungumza na waandishi nje ya mahakama kuu
 Wafuasi wa Chadema wanaomuunga mkono Zitto wakishangilia abaada ya ushindi wa kiongozi huyo

Tuesday, January 7, 2014


David Moyes, meneja wa Manchester United
Kocha Mkuu wa Klabu ya Manchester United ya England, David Moyes amesema angependa kusajili baadhi ya wachezaji kuimarisha kikosi chake lakini ana wasi wasi huenda asiweze kuwapata wachezaji hao katika usajili wa dirisha dogo mwezi huu wa Januari.
Kiungo Marouane Fellaini ndiye mchezaji pekee aliyesajiliwa tangu kuwasili kwa David Moyes katika kikosi cha Manchester United kinachoshikilia nafasi ya saba kwenye msimamo wa ligi kuu ya Kandanda ya England inayoendelea.
Kocha huyo amenukuliwa akisema kuwa "Tungependa kuongeza wachezaji lakini swali la kujiuliza,ni Je wanaweza kupatikana wachezaji hao"?
Akizungumza Jumapili baada ya kichapo cha mabao 2-1 dhidi ya Swansea kwenye kombe la FA, Kocha huyo amekiri kuwa kuna mahitaji makubwa ya wachezaji wapya ndani ya kikosi cha Manchester United, lakini hakuna umuhimu wa kutangaza jambo hilo kwa sababu wachezaji ambao angependa kuwasajili hawawezi kupatikana katika usajili wa dirisha dogo mwezi Januari.
Kocha huyo amekiri kuwepo kwa hali ya wasi wasi klabuni hapo msimu huu baada ya timu ya Manchester United kupoteza mechi nne kati ya sita zilizochezwa kwenye uwanja wa nyumbani wa Old Traford.
Kichapo cha Jumapili cha mabao 2-1 dhidi Swansea kilikuwa cha pili katika kipindi cha miaka thelathini kwa Manchester United kuondolewa katika raundi ya tatu ya michuano ya Kombe la FA, huku mwanasoka Wilfried Bonny akitia kambani bao la ushindi katika dakika ya 90, ushindi ambao ulikuwa wa kwanza kwa Swansea katika uwanja wa Old Traford,baada ya Javier Hernandes kusawazisha bao la kuongoza la Swansea lililotiwa kimiani mapema na Wayne Routledge.
Kipigo cha Jumapili dhidi ya Swansea ambacho ni cha saba katika michuano yote kwa ujumla msimu huu kimekuja kikifuatia kingine ambacho Manchester United ilikipata siku ya mwaka mpya baada ya kupigwa na Tottenham Hostspurs mabao 2-1.
Akizungumzia kipigo hicho kiungo Darren Fletcher amesema kuwa wachezaji wa Manchester waliwaangusha mashabiki na kocha wao huku akielezea kuwa hali hiyo imeleta maumivu na hasira kubwa kutoka kwa mashabiki wa timu hiyo kufuatia mwenendo wa timu nzima msimu huu ambapo imepoteza mechi nne kati ya sita zilizochezwa katika uwanja wa nyumbani wa Old Traford.

Chama cha UKIP kinachopinga swala la uhamiaji kinasemekana kuungwa mkono sana
Zaidi ya robo ya raia wa Uingereza wanataka kuona swala la uhamiaji likikomeshwa.
Hii ni kwa mujibu wa takwimu zilizotolewa na BBC.
Takwimu hizi ni za kustaajabisha. Asilimia 77 ya waliohojiwa wanasema wanataka uhamiaji kupunguzwa kiasi, zaidi ya nusu wanasema inafaa kukomeshwa kabisa.
Tangu mwaka 1997 karibu watu milioni 4 waliingia nchini Uingereza na maoni yanazidi kuonesha kuwa swala la uhamiaji ni tata sana Uingereza kuliko mataifa mengine ya muungano wa Bara Ulaya.
Lakini mgawanyiko wa kisiasa ungali ukishuhudiwa katika muungano wa kisiasa kuhusiana na swala hilo.
Katika mahojiano na BBC, Waziri wa chama cha Liberal Democrat anasema kuwa wale Conservatives wametangaza nia ya kupunguza uhamiaji iwe chini ya watu laki moja kwa mwaka haufai na haina maana.
Mhariri wamaswala ya kisiasa wa BBC anasema kuwa swala la uhamiaji limekuwa midomonmi mwa wengi Uingereza hasa uchaguzi mkuu ukitarajiwa mwaka ujao. Wengi wanaonekana kuunga mkono chama cha kisiasa cha UKIP chenye sera yake kuu ya inayopinga uhamiaji.
Chama tawala cha Conservative nacho kimeahidi kupunguza idadi ya wahamiaji nchini Uingereza.

Monday, January 6, 2014



Kamanda wa Polisi mkoa wa Ilala Dar es Salaam, SACP Marietha Minangi, wakati akiwasili Viwanja vya Mahakama Kuu.

Mmoja wa kijana aliyekamatwa na askari baada ya kuleta fujo eneo la mahakama.
Baadhi ya mabango waliyokuwa nayo wananchi eneo la Mahakama Kuu.
Wafuasi wa Zitto Kabwe.
Kiongozi wa Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) akiwahutubia wananchi waliofika mahakamani hapo baada ya hukumu ya Zitto kuahirishwa mpaka kesho saa nane mchana..
Wanausalama wakipanga mikakati ya kuimarisha ulinzi eneo la Mahakama Kuu jijini Dar.
Polisi wenye mbwa wakipita eneo la mahakama kuimarisha ulinzi.
Mmoja wa wafuasi wa Zitto akiwa na bendera.
Mwanasheria wa Zitto Kabwe, Albert Msando (kushoto) akitoka mahakamani baada ya hukumu kuahirishwa.
Wanahabari wakitoka eneo la mahakama.
Mahakama Kuu Kanda ya Dar es Salaam, imeahirisha kutoa au kutotoa zuio la muda kwa Kamati Kuu ya Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) kutojadili uanachama wa Zitto Kabwe mpaka kesho saa nane mchana

Sunday, January 5, 2014


Rais Jakaya Kikwete na mkewe Mama Salma Kikwete, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa,
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakitoa heshima za mwisho mbele ya Jeneza lenye mwili wa aliyekuwa Waziri wa Fedha, marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga mwili huo zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.
 Rais Jakaya Kikwete, akiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, Mkoani Iringa kwa maziko.
 Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal na mkewe Mama Zakia Bilal, wakiifariji familia ya marehemu Dkt. William Mgimwa, wakati wa shughuli za kuaga na kutoa heshima za mwisho zilizofanyika kwenye Viwanja vya Karimjee jijini Dar es Salaam, leo mchana. Mwili huo umesafirishwa leo kuelekea Mkoani Iringa kwa maziko.

  Mke wa baba  wa TAIFA Maria Nyerere, akitoa heshima za mwisho.
  Mwshimiwa Spika wa Bunge Anne Makinda, akitoa heshima za mwisho.
 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana heshima za mwisho.
  Mweshimiwa wa CHADEMA  Freeman Mbowe akitoa  heshima za mwisho.
  Mawaziriki wakiwa wanaenda kutoa heshima za mwisho
 Baadhi ya viongozi wa vyama vya siasa
  Baadhi ya viongozi wa Serikali waliohudhuria shughuli hiyo ya kuuwaga mwili wa marehemu

waliotembelea blog