Wednesday, June 29, 2016


Mgodi wa dhahabu wa Geita ‘GGM’ June 28 umetoa vifaa vya msaada katika hospitali ya Muhimbili vyenye thamani ya shilingi milioni 23 ili kusaidia jitihada za serikali katika kuboresha huduma za afya katika kitengo cha watoto Muhimbili.
Vifaa vilivyotolewa ni pamoja na Bp Mashine 10, Infusion Pump 2, Thermometers 110, Standing weghing scale 6, lying down weghing scale 6, nebulises 3 na pulse oxymeter. GGM imechangia ili watoto na kina mama wanaofika hospitalini hapo kupata huduma hizo muhimu



Baada ya kuwepo na taarifa mbalimbali zinazozagaa kwenye mitandao ya kijamii zinazotokana na habari iliyoandikwa na kuchapishwa kwenye gazeti la Jambo leo la June 24 2016, toleo namba 2482 yenye kichwa cha habari “Sasa ukimwi kupimwa nyumba kwa nyumba”.
June 28 2016 Ofisi ya Taifa ya Takwimu ‘NBS’ imetoa ufafanuzi kwamba UKIMWI hautapimwa nyumba kwa nyumba bali itafanya utafiti wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI Tanzania kuanzia September 2016 ambapo UKIMWI utapimwa kwenye kaya chache ambazo zimechaguliwa kitaalam nchi nzima ili ziweze kuwakilisha kaya nyingine nyingi ambazo hazitahusika moja kwa moja katika utafiti huo.
Taarifa iliyotolewa na NBS imesema utafiti huu utajumuisha kaya zipatazo 16,000 ambazo ni sampuli iliyochaguliwa kisayansi kutoka mikoa yote ya Tanzania Bara na Zanzibar na utahusisha watu wazima wasiopungua 40,000 wakiwemo watoto takribani 8,000.
Aidha, taarifa hiyo imeeleza kuwa katika utafiti huo kutakuwa na kupima homa ya ini, kupima wingi wa chembechembe za damu yaani CD4, kupima wingi wa virusi katika damu na kupima kiwango cha ufanisi wa dawa za kufubaza VVU kwa watu wanaotumia dawa hizo.
Taarifa hiyo imeongeza kuwa, utafiti huo wa viashiria na Matokeo ya UKIMWI wa mwaka 2016 unafanyika nchini kwa mara ya 4 ambapo utafiti wa kwanza ulifanyika mwaka 2003, wa pili ulifanyika mwaka 2007 na wa tatu ulifanyika mwaka 2011.
Hivyo, Ofisi ya Taifa ya Takwimu inapenda kuwatoa hofu wananchi kwakuwa utafiti huu sio mpya katika nchi yetu na watanzania ambao wamekuwa wakipitiwa na utafiti huu, wamekuwa wakitoa ushirikiano kwa zaidi ya asilimia 90.

June 28 2016 klabu ya Dar es Salaam Young Africans ilicheza mchezo wake wa pili wa Kundi A wa Kombe la shirikisho barani Afrika dhidi ya TP Mazembe ya Jamhuri ya Kidemokrasia ya Kongo, katika mchezo huo Yanga ilifungwa goli 1-0, goli amble lilifungwa na Merveille Bope dakika ya 74.

Thursday, February 18, 2016


Klabu ya Manchester United bado ipo katika kinyang’anyiro cha kuwania Kombe laEUEFA Europa, kombe ambalo ni la pili kwa ukubwa barani Ulaya baada ya Kombe la Klabu Bingwa barani Ulaya, Man United usiku wa February 18 walikuwa wageni wa FC Midtjylland, walikubali kipigo cha goli 2-1. Magoli ya FC Midtjylland yalifungwa na Pione Sisto dakika ya 44 na Paul Onuachu dakika ya 77 wakati goli la pekee la Man Unitedlilifungwa dakika ya 37 na Memphis Depay.

Tuesday, January 12, 2016



Mtu wangu wa nguvu January 12 katika pitapita zangu mtandaoni nikakutana na list ya majina ya utani ya mastaa watano wa soka. Katika maisha kila mmoja anaweza akawa na jina la utani ambao huenda kapewa na familia yake au washikaji zake mtaani au kwa sababu ya umahiri wake uwanjani ndio anaweza kujkuta kapewa jina. January 12 naomba nikusogezee majina ya utani ya mastaa hawa wa soka Messi, Ribery, Torres, Robben na Kroos.
5- Toni Kroos huyu kutokana na umahiri wake uwanjani, kocha wa zamani wa klabu ya Real Madrid ya Hispania Carlo Ancelotti aliwahi kumtunga jina na kumuita “The professor” hii inatokana na uwezo na akili yake ya kuumiliki mpira uwanjani.
Kroos1
4- Mshambuliaji wa kimataifa wa Hispania ambaye amewahi kuvichezea vilabu vya Liverpool na Chelsea vya Uingereza Fernando Torres alipewa jina la utani la “El Nino” ambalo lina maana ya kuwa mtoto, Torres ambaye ana umri wa miaka 31 amerudi kwenye klabu yake iliyomlea ya Atletico Madrid, lakini wakati ana umri wa miaka 16 akiwa Atletico alikuwa akicheza mpira kwa kiwango cha juu kutokana na wengi kutokuwa wamelishika jina lake na muonekano wake wa kitoto wakawa wanamuita “El Nino”
Torres4
3- Franck Ribery huyu jina lake la utani anaitwa “Scarface” jina ambalo alipewa kutokana na sura yake kuwa na makovu na mikunjo usoni. Makovu ya Ribery yalitokana na ajali aliyowahi kuipata wakati akiwa na umri wa miaka miwili, makovu ambayo yapo usoni kwake hadi leo.
Ribery1
2- Mshindi wa tuzo ya tano ya Ballon d’Or Lionel Messi yeye jina lake la utani anaitwa “La Pulga” ambalo limetokana na kimo chake ambacho kimekuwa kikiwasumbua  wapinzani, licha ya kuwa hana umbo kubwa sana.
Messi19
1- Winga wa kimataifa wa Uholanzi Arjen Robben yeye kutokana na uwezo na mbio zake uwanjani na uwezo wake wa kujirusha uwanjani pale anapokuwa kafanyiwa faulo uwanjani, alipewa jina la mdachi anayepaa “The Flying Dutchman” .
Robben5

Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta.

BAADA ya kushinda Tuzo ya Afrika kama Mchezaji Bora wa Mwaka 2015 kwa Wachezaji wa Ndani, mchezaji wa Taifa Stars na Klabu ya TP Mazembe ya DRC Congo, Mbwana Samatta anatarajiwa kupongezwa na kuagwa rasmi na mashabiki wake leo ndani ya Uwanja wa Taifa wa Burudani, Dar Live uliopo Mbagala-Zakhem jijini Dar.  Akizungumza na Uwazi, Meneja wa Dar Live, Juma Mbizo alisema kuwa mapema kabla ya saa kumi na mbili jioni kutakuwa na matembezi sambamba na Samatta maeneo ya Temeke na baada ya hapo, saa kumi na mbili atatinga ndani ya Dar Live kuwaaga mashabiki wake. 


“Kutakuwa na red carpet ambapo mashabiki wote watapata fursa ya kupiga picha na Samatta sambamba na kuzungumza naye mawili matatu kisha burudani kabambe itafuatiwa kutoka kwa Khalid Chokoraa ambaye tayari amemtungia wimbo, Twanga Pepeta chini ya Ali Chocky pamoja na Msagasumu,” alisema Mbizo na kumalizia kuwa kiingilio kitakuwa ni 5,000 kwa wote.

 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde ( wa pili kushoto) akiwa na Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso,akifatiwa na Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula kwa pamoja wakionyesha bango kuashiria uzinduzi wa Mradi wa Airtel Fursa msimu wa pili. Akishuhudia (kushoto) ni Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya.
 Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso akiongea na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2. mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24
kupata fursa za kuinua biashara zao, uliyozinduliwa Naibu waziri Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa 2 mradi unaowawezesha vijana kati ya miaka 18 hadi 24  kupata fursa za kuinua
biashara zao. Uzinduzi huo ulifanyika katika ofisi ya Airtel makao makuu Jijini Dar es saalam
 Kijana aliyewezesha kupitia mradi wa Airtel FURSA msimu wa 1, Mohamed Kigumi akipongezwa na  Mkurugenzi mkuu wa Airtel Bw, Sunil Colaso kwa kufanya vizuri katika biashara yake wakati wa uzinduzi wa msimu wa pili wa mradi wa Airtel FURSA , mradi wenye lengo la kuwawezesha vijana kufikia malengo yao na kukuza biashara zao. Wakishuhudia (kushoto) ni Naibu waziri  Wizara ya Kazi Vijana na Ajira Anthony Mavunde  akifatiwa na Mkurugenzi wa mawasiliano wa Airtel, Bi Beatrice Singano Mallya. (kulia) ni Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula
 Mshauri wa Airtel Fursa, Eng George Mulamula akiongea wakati wa uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili
 Wageni waalikwa na waandishi wa habari wakifatilia uzinduzi wa mradi wa Airtel FURSA msimu wa pili uliofanyika katika ofisi za makao makuu ya Airtel Morocco jijini Dar es Saalam 

waliotembelea blog